Tutaipata Katiba Mpya, kuuzima mjadala wake ni ngumu

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Sasa ni wazi kwamba pamoja na sarakasi zote za kukamata wapinzani wanaoendekeza mijadala juu ya katiba mpya, lengo liko wazi ni kuzima Mjadala ili kuepusha kuiamsha jamii ili isipige kelele juu ya mchakato wake. Sasa ni wazi kua hii siyo CCM tu bado ni mfumo mzima hautaki katiba mpya huenda wana yao tusiyoyajua na wala siyo kuyumba kwa uchumi.

Watawala wetu wanashindwa kuelewa kuwa hakuna mgogoro mbaya duniani kama wa kudai katiba mpya, wamefumba macho hawakuelewa hili,mjadala wa katiba ni mgumu sana kuuzima kuliko kudai haki yeyote ile. Tunakoelekea kila kosa litakalofanyika wananchi watasema ni kwa sababu ya katiba mbovu. Itafika wakati wataona kua hawana haki katika taifa lake na wanufaika ni kikundi cha watu wachache wanaozuia mchakato wa katiba mpya. Hapa ndio watu watachoka na itapatikana kwa kupenda ima kwa kutopenda.

Ni askari gani atakayeweza kukukamata watu kwa sababu ya kuandamana kudai katiba mpya? Ataenda kuwafungulia kesi gani wakati wanachodai ni haki yao? Zaidi zitakua ni kesi za uhujumu uchumi na ugaidi ili kuwanyima dhamana wanaoongoza vuguvugu hili ili wasitoke ambapo nako hakuna ushahidi utakaoweza kumtia mtu hatiani . Huwezi kuondoa uhai wa mtu kwa sababu anaidai haki yake, katika hili itajikuta uko matatani.

Kwahiyo hakuna mwenye uwezo wa kuuzima mjadala wa katiba mpya huu ukishaanza umeanza, hua ni ngumu kuuzima zaidi ya kusikiliza wanaoidai. Kumfunga Mbowe haitakua njia ya kuuzima mjadala huu kwa sababu ni wa kitaifa, zaidi ni kutengeneza mijadala mipya ya wafungwa wa kisiasa.

Walioshauri kuuzima mjadala wa katiba mpya kuna siku watatajana wao wenyewe na watakumbuka maamuzi yao.
 
Wamezoea kura za kwenye mabegi. Neno katiba mpya = uhaini! Chama cha majambazi kweli kweli. Kinategema mabomu na risasi za Zirro.
 
Suala la Zuma kuhukumiwa limewapa hofu sana watawala wetu.

Wanaona kwamba nchi hii ikiwa na katiba mpya watatolewa madarakani na wengi wao watashtakiwa. Ndio maana wanatumia nguvu kubwa kuzima mijadala ya katiba mpya.
 
Lililobaki ni kwa "Maza Mizinguo" kutafuta njia nzuri tu ya kutokea na kubaki na heshima kiduchu.

Hana tena njia wala uwezo wa kuzuia Katiba mpya isitengenezwe.

Labda awe anataka kujiangamiza mwenyewe na chama chake. Lakini sidhani kuwa watamruhusu afanye hivyo.
 
salumu kikeke: "mheshimiwa rais unaweza kuniahidi na kunithibitishia kuwa jambo hilo( la katiba mpya) utalishughulikia?"
Samia:"mmmmh, ngoja tuone jinsi tutakavyo shauriana na wenzangu "
 
Sasa ni wazi kwamba pamoja na sarakasi zote za kukamata wapinzani wanaoendekeza mijadala juu ya katiba mpya, lengo liko wazi ni kuzima Mjadala ili kuepusha kuiamsha jamii ili isipige kelele juu ya mchakato wake. Sasa ni wazi kua hii siyo CCM tu bado ni mfumo mzima hautaki katiba mpya huenda wana yao tusiyoyajua na wala siyo kuyumba kwa uchumi...
Wananchi watanzania katiba mpya haijawa HITAJI LAO.

Hakuna mwananchi mtimilifu asiyefaidika na makundi ya kisiasa anayehitaji katiba mpya.

Wanasiasa ndio wanaotaka katiba mpya kwa ajili ya VYEO.

Wako wa huku Tanzania bara...."G55" IMEFUFUKA.

Wako wa visiwani....nao hawautaki muungano wetu kuntu.

#SiempreSerikaliMbiliZaJMT
#NchiKwanzaKablaYaYeyote
#PundaAfeMzigoUfike
#MzigoNiAmaniYaJMT
#MzigoNiUsalamaWaJMT
 
Lililobaki ni kwa "Maza Mizinguo" kutafuta njia nzuri tu ya kutokea na kubaki na heshima kiduchu.

Hana tena njia wala uwezo wa kuzuia Katiba mpya isitengenezwe.

Labda awe anataka kujiangamiza mwenyewe na chama chake. Lakini sidhani kuwa watamruhusu afanye hivyo.
Unachokiongea wala hakina UHALISIA.

Katiba mpya si hitaji la watanzania walio wengi.

Ni hitaji la makundi "pote" ya wanasiasa....lengo ni VYEO....wako wasioutaka Muungano wa Serikali mbili.....wako wanaoitaka marehemu TANGANYIKA.....wameamua kujifichia katika kivuli cha katiba mpya.

CCM ipo imara.
Kiitwacho KATIBA mpya wala si kitisho kwa mh.Rais SSH na CCM.

ENDELEA KUUFUKUZA UPEPO

#SiempreSerikaliMbiliZaJMT
#NchiKwanzaKablaYaYeyote
#PundaAfeMzigoUfike
#MzigoNiUtulivuWaJMT
#MzigoNiAmaniYaJMT
#KaziIendelee
 
salumu kikeke: "mheshimiwa rais unaweza kuniahidi na kunithibitishia kuwa jambo hilo( la katiba mpya) utalishughulikia?"
Samia:"mmmmh, ngoja tuone jinsi tutakavyo shauriana na wenzangu "
Sasa akengeuke na "ushauri wa hao wenzake"; hapo ndipo atakapoona kwamba hajui kitu!
 
Unachokiongea wala hakina UHALISIA.

Katiba mpya si hitaji la watanzania walio wengi.

Ni hitaji la makundi "pote" ya wanasiasa....lengo ni VYEO....wako wasioutaka Muungano wa Serikali mbili.....wako wanaoitaka marehemu TANGANYIKA.....wameamua kujifichia katika kivuli cha katiba mpya.

CCM ipo imara.
Kiitwacho KATIBA mpya wala si kitisho kwa mh.Rais SSH na CCM.

ENDELEA KUUFUKUZA UPEPO

#SiempreSerikaliMbiliZaJMT
#NchiKwanzaKablaYaYeyote
#PundaAfeMzigoUfike
#MzigoNiUtulivuWaJMT
#MzigoNiAmaniYaJMT
#KaziIendelee
"Linapokuwa hitaji la makundi" kama unavyoweka wewe uliyeko kwenye kundi linalonufaika na katiba mbovu, usiilaze akili yako ukadhani wananchi hao wapo kwenye kundi lako la "kutohitaji". Huu ndio ukilaza unaowasumbua watu kama wewe.

Ni lini wewe umejuwa uhitaji au kutohitaji katiba mpya kwa waTanzania?
 
Haijawahi kutokea duniani watu wakaruhusu hivyo unavyowazia, Kupatikana Katiba bora kote duniani na siku zote huwa ni mchuano mkali wa matabaka na maslahi.
 
Hakuna mtu atakubali umpokonye tonge lake mdomoni kirahisi
 
Back
Top Bottom