Tutafute msuluhishi wa mgogoro wa kidini nje ya nchi,wenyewe hatuna msafi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutafute msuluhishi wa mgogoro wa kidini nje ya nchi,wenyewe hatuna msafi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fikira, Oct 19, 2012.

 1. f

  fikira Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni tumeshuhudia upepo mbaya wa mahusiano ya kidini kufuatia kukojolewa kwa msahafu wa waislamu na kisha kuchomwa moto makanisa na mali zingine kuharibiwa.Kilichofuatia baada ya tukio hilo ni kauli nzito za kimsimamo zilizotolewa na pande mbili zinazohasimiana,waislamuj na wakristo.Nimepata fursa ya kutosha kusoma matamko ya kila upande kwa makini.Kwa jumla wakristo(Maaskofu KKKT) wanalalamikia ukimya wa Serikali kuchukua hatua kufuatia vitendo vya muda mrefu vya wailamu kuingilia mamlaka ya nchi,kama kugomea sensa,kushinikiza waliogomea sensa na kukamatwa waachiwe,kuchomwa makanisa Zanziba,mahakamaya kadhi,kukataa ubalozi fulani nk.

  Kwa upande wa waislamu wanalalamikia Kuonewa kwa muda mrefu na bila Serikali kuchukua hatua,kama,kuchomwa moto misahafu yao,kukamatwa na polisi,kunyimwa mahakama ya kadhi,kubaguliwa nafasi za uongozi na hili la kukojolewa msahafu,nk.Aidha wanaamini kuwa migogoro ya kisiasa ,migomo na maandamano kama ni mbinu za wakristo kumuhujumu Rais kabla hajamaliza kipindi chake,zinazoongozwa na CDM. Ili mradi kila mmoja anaona hatendewi haki na serikali(ya kikwete)

  Kwa muono wangu,ni kweli Serikali imezembea sana kuchukua hatua kukomesha udini mara tu dalili zilipoanza kujitokeza.(Sisemi kuna upande wowote ulioonewa)..Udini na Ukabila ni sumu mbaya inayopaswa kukomeshwa katika hatua za awali kabisa. Kwa Tanzania udini umeshakomaa,tumechelewa,pande zote haziaminiani tena ,na hawaiamini serikali yao.HAKUNA ALIE SAFI MWENYE UBAVU WA KUWAWEKA CHINI PANDE HIZI MBILI NA KUZIKEMEA,ACHILIA MBALI KUSULUHISHA,TWAHITAJI MTU NEUTRAL WA KUFANYA KAZI HIYO.
  MUNGU IREHEMU TANZANIA.
   
 2. B

  Bob G JF Bronze Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Usuluhishi pekee ni kuiondoa ccm ambae wapigakura wake wakutegemewa wameamua kutokutii sheria tena baada ya kuruhusu akili ndogo kuongoza watu wenye akili nyingi
   
 3. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,121
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Mimi mtoa mada kama nimemuelewa vile, lakini tatizo lililopo ni kwamba sisi watanzaniz baadhi ni much know, maana wakati hao tunaowaona hao wenye akili ndogo wanawachagua viongozi wao wewe mwenye akili nyingi ulikuwa wapi? Na kwa style hii ya kuanza kubaguana sidhani kama tutapata yule kiongozi tunayemtegemea, ofcourse as Tanzanians we have long way to go.
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tanzania hatuna mgogoro wa kidini bali ulegelege wa serikali kuwalea wahuni wanaojificha nyuma ya majoho ya dini. Hawa wako pande zote. Kuna mashehena njaa kama Ponda, Khalifa Hamis, Ali Baseleh, Farid na wachungaji mafisi kama Rwakatare, Gamanywa, Kakobe, Lusekelo, Mwakasege, Mwingira na wengine wengi tu. Hawa ndilo tatizo maana wamedandia vitu hata wasivyosomea. Wanasukumwa na njaa na ufisi wa kutaka kuwaibia watu tena wanyonge na wajinga ambao wamewageuza watumwa wanaoweza kuwatumia watakavyo kama kwenye huu upuuzi unaoendelea.
   
Loading...