Tutafute mkakati mwingine wa kupambana na Rushwa!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutafute mkakati mwingine wa kupambana na Rushwa!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Dec 12, 2009.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Dec 12, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Rushwa ni fadhila zitolewazao au kupokelewa ili kutokee upendeleo fulani. Zamani sana ningali shule ya msingi nilikuwa nimeakaririshwa ahadi, imani na madhumuni ya TANU; mojawapo ilikuwa inasema hivi:

  "Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa."

  Katika sheria za Tanzania, kuna sheria zinazoharamisha rushwa, na ndiyo maana kuna kitengo maalum cha serikali kinachopambana na rushwa. Mwanzoni mwa utawala wa Mkapa, kulikuwa na tume ya kuchunguza tatizo la rushwa nchini. Yote hayo ni kuonyesha kuwa Taifa letu linatambua wazi ubaya wa rushwa.

  Hhata hivyo, inaonekana kuwa bado hatujajua namna ya kupambana na rushwa sawasawa, ndiyo maana beneficiaries wengi wa rushwa hawajawahi kutiwa hatiani kwa makosa hayo. Katika kosa la rushwa, mtoaji na mpokeaji kwa pamoja wanavunja sheria. Hata hivyo, kisheria inabidi washikwe na mtu wa pembeni na athibitishe kuwa watu hao walikuwa wakipeana rushwa ili kuwe na upendeleo wa aina fulani, vinginevyo hakuna njia rahisi ya kuwashika watumia rushwa hasa kama wote wamekubaliana. Mara kwa mara wapokea rushwa wamekuwa wakishikwa pale tu ambapo mtu aliyeombwa rushwa anaona kuwa hana haja ya yeye kutoa rushwa hiyo ili apate haki yake; na watoa rushwa wamekuwa wakishikwa pale wanapotoa rushwa ndogo sana kiasi kuwa mpewa rushwa anaona kuwa hatapata faida yoyote kwa kupokea rushwa hiyo. Njia rahisi ya kushika watumia rushwa waliokubaliana ni kutoa msamaha na kumtisha mmoja hasa yule aliyeshawishiwa kujihusisha na rushwa hiyo ili atoe ushahidi dhidi ya yule aliyeshawishi rushwa kumtia hatiani na yeye shahidi aachiwe huru. Kwa vyovyote sheria zetu dhidi ya rushwa bado ni dhaifu sana.


  Kuanzia miaka ya themanini wakati wa "Mikingamo" wapokea na watoa rushwa walianzisha njia nyingine ya kufanya hivyo kwa kupitia "wakaa kati." Yaani ama mtoa rushwa au mpokea rushwa au wote wawili wanatumia watu wengine kuomba, kutoa au kupokea rushwa hiyo ili upendeleo ufanyike baina ya wahusika. Kwa vile sheria zetu bado zinataka ithibitike kuwa anayeshitakiwa ndiye aliyehusika na rushwa ile moja kwa moja, ni wazi kuwa haziwezi kufanya lolote kuhusiana na rushwa zinazohusisha wakaa kati.

  Kwa wanaojua sheria, je tufanye nini katika sheria zetu ili kukabiliana na rushwa zinazotumia wakaa kati? Yaania kumtia hatiani yeyote aliyehusika kama mkaa kati wa rushwa na wale beneficiaries wa rushwa inaytumia wakaa kati.
   
 2. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kichuguu

  Safi sana, nitairudia baadaye na some comments.
   
 3. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kichuguu

  Ulofa na ujinga wa kuiga mambo bila kuyatathmini. Nchi hata zilizoendelea kama vile UK wana agency ambayo inajulikana kama SOCA ambayo kazi yake kubwa ni kuchunguza na kuwaadhibu wanaopokea rushwa na kuwafilisi bila kuwapeleka mahakamani. Kunyang'anya mali pamoja na magari ya kifahari nyumba n.k. endapo utashindwa kutoa ushahidi kwa maandishi umewezaje kupata utajiri huo na umeweza kulipa kodi halali. Bongo tunawaona tena wana dharau sana wakati hizo ni mali za wizi na jasho la walipa kodi.

  Tanzania lazima sheria zibadilishwe ili wakupuaji wote na pesa zao za ufisadi washughulikiwe. Kitu kingine cha kustaajabisha hata Bank wameruhusu kuchukua forex kwenye ATMs na capital flight inaondoka bure bure tu, sijui lini tutaamka.

  Mataifa yaliyoendelea hayakubali watu waondoke na pesa zao bila ku-prove kwamba wamezipata kihalali.

  "Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa."

  Hii ilikuwa moja ya ahadi za wana TANU kama sikosei, Je JK akiulizwa bado ana uhakika na hiyo statement? Anaweza kuishuhudia under oath?
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hivi mnajua hata hii tunayoita misaada kutoka mataifa tajiri ni RUSHWA nyengine?? hivyo kama Taifa linapokea rushwa ujue inaleta ugumu kupambana na rushwa ya kambale au sangara mmojammoja.

  Mbinu ni kukataa misaada na kukata au kupunguza matumizi na kudhibiti mfumuko bila kusahau kuwapa meno wanausalama kubaini vyanzo vya mapato ya viongozi na watawala kuanzia ngazi ya mtaa...... need me to say more?
   
 5. W

  Wasegesege Senior Member

  #5
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaaaaaaaaaaaammmmmmmmmmmmmmaaaaaaaaaaaaaaaaannnnnnnnnnnniiiiiiiiii eeeeeeeeeee nataka mnisaidie kufahamu hivi ni nchi gani ambayo haina rushwa? Maana nasikia juzi kumbe yule jamaa aliyezamia ikulu kule marekani kwa mkenya (obama) wakati wa dhifa alitoa kitu kidogo kwa walinzi na wapiga picha za television ili aweze kuingia na kuuza sura yake. Na kweli jamaa alifanikiwa maana hivi sasa anauza picha zake kama karanga.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  So, what is your point?
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Jan 9, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tanzania tunalea rushwa kwa sababu kadhaa:

  (a) Tu waoga wa kuwakabili viongozi wetu tuliowapa dhamana ya rushwa.

  (b) Tuna tabia ya kuangalia kwa upeo mfupi tu; watu hawajali kukemea rushwa kwa vile wanona kuwa haiwaingilii katika maisha yo ya kila siku. Hawaangalii upeo mrefu wa maisha yao.

  (c) Tuna tamaa ya mambo mengi yaliyo nje ya uwezo wetu. Ndiyo maana utaona kuna watu hao wanajenga majumba hapa na kuyapa thamani ya majumba yaliyoko New York bila kuangalia tofauti za kiuchumi baina ya miji hii miwili.

  (d) Wengi wetu tunatamani tupewe nafasi hizo zenye mianya ya rushwa kusdi nasi tuendeleze libene hiyo hiyo ya rushwa

  (e) Tunadhani kuwa kumkemea mla rushwa ni kumwonea wivu

  (f)......  Ninashauri tu kuwa wabunge wetu watuwekee sheria inayoharamisha kitendo chochote cha rushwa direct or inderct kwa kiwangoi sawa na murder. Adhabu itolewe kwa wote direct beneficiaries na agents wao.
   
Loading...