Tutafika Miaka80 ya Uhuru tukiwa hapahapa Sababu:-

M2flan

JF-Expert Member
Jun 27, 2013
414
250
Huu ni mwaka wa 52 tangu kupata uhuru nchii hii toka kwa Mwingereza,Lakini ni hatua flani chache za maendeleo tulizozifikia tangu kupata kwetu uhuru1961.Maendeleo mengi tuliyonayo hadi hivi sasa ni kwa mchango wa Mwl.JK Nyerere, ambapo tangu kufariki kwake naweza sema hamna cha maana sana tulichofanya kama Mzee wetu huyu.Sababu zifuatazo ndizo zilizotufanya tudumae katika maendeleo ya Taifa hili nazo ni:-
1)Siasa za mdomoni zisizolenga utekelezaji.
2)Kulewa madaraka kwa viongozi wetu
3)Uvunjifu na kutofuata Maadili ya Uongozi
4)Kushindwa kwa Serikali kudhibiti mapato yake ikiwa pamoja na kutowawajibisha viongozi wabadhilifu
5)Uanzishaji wa Sera zinazolenga kuleta maendeleo pasipo na mikakati madhubuti.
6 )Kuwa na sheria dhaifu katika udhibiti wa Rasilimali.
Hizo ni baadhi ya sababu tu ambazo zitafanya tufike Miaka80 ya Uhuru tukiwa hatuna maendeleo ya kulinganisha na umri wa Uhuru husika.Muhimu Serikali itambue hili
 

aduwilly

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
1,178
1,195
usijali mkuu, Makamba alisema watatawala miaka mia which means tutaendelea kuwa hivi hivi kwa muda wa miaka 48 more from now
 

BALAKI

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
371
0
Riport ya lembeli inaonyesha jins viongoz na watendaji wetu wanaweza kusimamia uhujumu na ufirauni juu ya wananchi wao wenyewe huku wakisimamia hali mbaya ya wananchi. kumbe tunaweza simamia ouvu kwa gharama yeyote lkn hatuwez simamia maendeleo kwa nusu gharama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom