Tutafika 2015 tukiwa na chadema yenye afya njema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutafika 2015 tukiwa na chadema yenye afya njema?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by twijuke, Oct 24, 2012.

 1. t

  twijuke JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimekuwa nikifuatilia siasa zetu hapa Tz. Kitambo watanzania wengi walihitaji sana mabadiliko na ushahidi tosha ni kura alizo pata Augustine Mrema mwaka 1995 kwa zati kabisa wenzetu wale walihitji mabasiliko.

  Kilichokuja kutokea baada ya NCCR maeuzi kubomoka watu wakahamia TLP, hapa tunaona ni jinsi gani Mzimu wa mabadiliko ungali hai. Baada ya TLP, mwendo ukawa uleule tumeshuhudia jinsi TLP livyo fumuka na hatimaye kubaki ikiwa haina afya.

  Ikaja CUF tukasema sasa tukasema sasa wanachukua nchi, pamoja na kwamba CUF haikuwa imejidhatiti Tz bara lakini walifika mahali pa kutia moyo. Lakini baada ya minyukano ya baina ya viongozi ndani chama watu wakakosa imani na hatimaye hali hii kupelekea watanzania wengi kuamini kuwa mfumo wa vyama vingi ni danganya toto. Kwamba ni janja ya Chama tawara na hawa waanzilishi wa vyama ni mapandikizi kutoka CCM.

  Na sasa hatimaye CHADEMA, kitambo sasa baada ya chama kuonesha ukomavu na kuwa na wabunge wenye kujenga hoja zenye mashiko tumeona watanzania wengi jinsi walivyo na imani na Chapman hiki, tuligikia hatua ya watanzania kutokupiga kura kwamba hata mtu akipiga kura nisawa na bule hivyo bora kutokupiga kabisa. Lakini tumeshuhudia mwaka 2010 baada ya Dr. S kugombea tuliona mwamko wa watu vijana walipiga kura kiasi cha kushangaza.
  Hofu yangu je tutafika 2015 tukiwa na chadema yenye afya njema?
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Usiwe na shaka mkuu. CHADEMA ni chama chenye mizizi imara isiyotetereka. Pia ni chama cha umma na Mungu. Tuombe uzima tufike 2015 ili tuushuhudie ukombozi wa taifa letu.
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  tutafika mkuu...CHADEMA NI CHAMA MAKINI sana na hii inatokana na kuwa na "thinking tanks" wengi ambao hawako publicly known...hili hata ccm inalijua na ndio maana kila kukicha hawapati usingizi.......
   
Loading...