Tutafakari Wazo Hili

TANURU

Senior Member
Jan 13, 2010
162
6
Kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikiwaza sana ni kwa jinsi gani tunaweza kuliunganisha bara letu la Afrika kwa gharama nafuu kabisa ukilinganisha na faida na kuweza kuwa na fursa ya kuweza kuona na kujua kila siku nini kinafanyika katika nchi zetu.

Tunaweza kweli kuungana kisiasa lakini bila ya kuwa na Televisheni Yetu Maalum ya Afrika ambayo itaonekana katika kila kijiji hapa Afrika, basi tutaendelea kuota ndoto za mchana kila siku. Na ili tuweze kujua angalau kidogo kuhusu bara letu tutaendelea kuizitengemea televisheni za BBC, VOA, CNN n.k.

Televisheni hii ya Afrika itatusaidia sana katika kukuza demokrasia na kujifunza mambo mbali mbali toka katika nchi zetu na itakuwa pia rahisi kuwa na mafunzo maalum kwa njia ya Televisheni yakilenga zaidi katika kutuongezea ujuzi na maarifa katika nyanja mbalimbali lengo kuu likiwa ni kufuta umasikini katika uso wa bara letu ndani muda usiozidi miaka 30 toka sasa.

Ni muhimu sana Televisheni hii iwe na Channels zaidi ya 10 ili kuhakikisha kuwa matangazo yake na mafunzo kupitia Televisheni hii yanapatikana kwa lugha zote kuu zinazotumika katika bara letu.

Kupitia Televisheni hii mahususi kwa Afrika (PAN AFRICAN TELEVISION---PATV) itakuwa pia rahisi kuwaunganisha wataalam wetu mahili walioko ndani na nje ya bara letu la Afrika.
 
Unawaza kuunganisha Afrika wakati EA inatukimbiza mbio? Sio hiyo tu Muungano wetu na Zanzibar unatukimbiza mbio pia ndo sembuse na Afrika bana?
 
Wazo zuri sana mkuu.

Yaani inaboa sana kuangalia BBC, CNN n.k na kuona wanavoitangaza Africa kwa mabaya yake tu. Njaa, magonjwa, maisha duni, vita n.k. Kana kwamba hawaoni the positive side of things. It sucks, really!

Tutakapokua na PATV itatusaidia kuwaonesha kua tunayo pia mambo mazuri kwetu.

Ni hayo tu.
 
The following user M-BONGOTZ says thank you TANURU for this useful post.
 
Wazo zuri sana mkuu.

Yaani inaboa sana kuangalia BBC, CNN n.k na kuona wanavoitangaza Africa kwa mabaya yake tu. Njaa, magonjwa, maisha duni, vita n.k. Kana kwamba hawaoni the positive side of things. It sucks, really!

Tutakapokua na PATV itatusaidia kuwaonesha kua tunayo pia mambo mazuri kwetu.

Ni hayo tu.

Bahati mbaya sana viongozi wetu hawalioni hilo. Tutaendelea kuwa nyuma kila wakati. Kama televisheni zinadaiwa kuwaharibu vijana wetu katika bara letu la Afrika, ni muhimu basi tukazitumia televisheni hizo kuwajenga vijana wetu kimaadili na kielimu. Hivi ni lini mimi na waafrika wenzangu tutajifunza kuhusu ufugaji bora wa ng'ombe Zimbabwe bila msaada wa televisheni. Kwangu mimi televisheni ni Muhimili Mkuu wa maendeleo iwapo itatumika ipasavyo.
 
Back
Top Bottom