Tutafakari: Uzuiaji wa mikutano ya kisiasa na sheria ya habari je zimetusaidia chochote ?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,603
8,743
Je kwa mawazo yako hizi sheria za habari ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na kusababisha waandishi wa habari na wanasiasa wengi kufunguliwa kesi zimesaidia nchi yetu kwa miaka minne sasa?. Vilevile uzuiaji wa mikutano kwa wapinzani Je imeleta amani yeyote na imesaidia chochote?. Tuliambiwa kufanya hivi itasaidia maendeleo na hatutakuwa na siasa kwa miaka mitano!!

Kwa mawazo yangu binafsi yote hapo juu hayajasaidia badala yake yamegawanya nchi zaidi. Wapinzania wamepata njia za kuongea tena hizi za mitandao kwa miaka ijayo inawezekana zikazidi nguvu ya mikutano ya nje. Lakini vilevile tumeona hizi sheria zimeanza kuharibu uhusiano wetu na nchi nyingine. Hivyo sijaona faida ya hizi sheria zaidi ya majanga. Sheria nyingi za hivi hazitugwi kwa masilahi ya nchi bali ya watu wachache na chama zaidi.

Lawama hapa sio serikali pekee bali bunge letu
 
Hii nchi jiwe anazidi kuikandika matope imefika point vyombo vywtu vya usalama vimeamua kumlinda mtu mmoja na kuisaliti nchi na wananchi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imesaidia sana - kwanza kabisa, vyama vya upinzani vimeshindwa kuhamasisha migomo ya mara kwa mara. Na kwa hivyo usalama wa raia umekuwepo tena kwa gharama ndogo.
Pili, wapinzani wamepata muda wa kujitafakari kwamba matendo yao hasa kwa awamu ya nne yalikuwa ya hovyo.
Tatu, wananchi wameelewa kauli mbiu ya kufanya kazi na kuona kelele za wapinzani siyo tija
..... Nk.
 
Migomo gani ilikuwa inafanywa na vyama vya upinzani?. Wapinzani wamepata muda wa kujitafakari kwa lipi mbona mawazo yaleyale?. Walisema hatutaki siasa mbona bado siasa zipo kila mahali? Tena siasa zimezidi hata zamani
 
Back
Top Bottom