Tutafakari maamuzi ya serikali kipindi hiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutafakari maamuzi ya serikali kipindi hiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KGARE, Jul 31, 2012.

 1. K

  KGARE Senior Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wana JF!!
  Mnalionaje hili swala la serikali kuwa n trend ya kutoa makaripio kwa kila kikundi kinachokuwa kikilalamikia hali na mwenendo wa mambo katika sekta mbalimbali? Je wananchi hawana haki ya kusema hapana katika kile kinachoendelea katika serikali yao kutokana na maamuzi ya serkali yao?
  Kwa nini serikali hailiangalii swala hili kama ni dalili ya kutoridhika kwa wananchi inayowatumikia na kuamua kwa dhati kuyatatua kwa nia njema hata kama ni ngumu...lakini ishirikishe wananchi njia za kuyamaliza?
  Mfano kwa sasa ni WALIMU na MADAKTARI.

  WANAHABARI wanaojaribu kutafuta chanzo cha mambo yanayotokea, vinanyamazishwa kwa kuambiwa ni wachochezi.
  Tutaruhusiwa kusema nini na kwa nini tusimseme yoyote katika sehemu yoyote kama ina mahusiano na kuvunja sheria maana hakuna aliye juu ya sheria hata kama ni Rais mwenyewe?

  Katika hayo yote, wawakilishi wa wananchi (viongozi wa vyama vya kazi, wabunge na wanahabari) wanazuiliwa wasiyazungumzie.


  WANANCHI TUFANYEJE JAMANI maana naogopa tunaweza kufika mahali tukakosa amani kwa mambo yanavyoenenda.TUTAYAMALIZAJE MATATIZO TUNAYOYAONA SERIKALINI KWA MTINDO HUU?
   
 2. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  muda wa kutafakari na kufikiria ulishaisha muda mrefu maana sasa kila mtu anajua ukweli wa hili, cha msingi kilichobakia ni VITENDO (In English ACTION/DEEDS) mbali na hapo ni bora kukaa kimya mkuu
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wao wanavyofanya,wanadhani wanatatua tatatizo,kumbe kiuhalisia wanalikuza na itafika kipindi itaghalimu hata maisha ya watu!serikali hii ilishazoe ukandamizaji sababu ya kusistiza amani ambayo ki ukweli haipo.siku zaja bomu litalipuka!!!
   
Loading...