Tutafakari hivi inakuaje hadi mh mbunge kuachia kiti chake?

stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,227
5,132
Msaada wakuu:-Najiuliza saaana lkn sijapata bado jibu lake, hivi inakuaje mbunge wa chama fulani wa jimbo flani ameng’atuka rasmi ubunge na kukihama chama chake na kujiunga na chama fulani,

Yaani mtu anaweza kufanya maamuzi kama hayo na kuutema mshahara wa ubunge, posho za bungeni, mkopo wa gari(kilimo kwanza)posho za ziara jimbo kwake na marupurupu kibao.

KILA NIKITAFAKARI SILIPATI JIBU
Kwamwenye mtazamo zaidi naomba na mimi anifahamishe vizuri wanajamvi wenzangu
 
Jibu ni hii!Nakupa Mfano ni sawa na kutaka kumsajili Ronaldo au messi....wao Lazima watahama kwa Dau wakataopewa....
So kwa mb akiacha ubunge ni sawa na kauza j---mbo kwe mwingine ...
Nafikiri utakuwa umenielewa

Ova
 
ela inaongea,wanalipwa kila kitu ndio wanaachia ubunge.uwezi acha kazi wakati una madeni kibao na bado una mshahra wa kutosha kirahisi rahisi tu,
 
Vipi mme/mke kuachana na mwenza!, hilo unalo majibu yake? Otherwise usituchoshe mkuu..
 
Anakuwa amechoka kazi. Asipewe tena

Anakuwa mamluki. Amemaliza kazi yake

Kaona fursa nyingine ya kuneemeka mahali kwingine.

Katishwa.

Basi tu
 
Wanafika bei, hivi huko hakuna wanaume wa kuwakamata na kuwachapa bakora? Maana wanafanya mambo ya kitoto na ulafi
 
Wanahama ili waendekuunga mkono juhudi na kasi ya awamu ya tano chini ya jemedari rahc John pombe magufuri,kwani yale waliyokuwa wakiyapgania kwa mda mrefu wanaona yanatekelezwa na JPM.
 
Back
Top Bottom