Kina mama wawili wanakuja nyumbani kwangu na kuniomba kadi ya CCM,wanaiangalia na kuandika namba zake wananirudishia hapo hapo wanaomba kitambulisho cha mpiga kura nacho wananakili baadhi ya mambo na kisha wananirudishia na kunishukuru.
Kabla hawajaondoka ninawauliza kwa nini wanafanya hivyo?Kwa sauti ya upole wananiambia kuwa wanataka wajue watu ambao ni mtaji wa CCM yaani wenye kadi na hati ya kupigia kura.
Kwa haraka silioni kosa lakini natamani nijue angalau yafuatayo,

- Kwa nini wafuate watu majumbani badala ya kuwaita kwenye ofisi za chama?
- Jambo hili linavunja taratibu zozote?
- Je katika siasa za ki mafia halitatuletea matatizo kwa familia ambazo sio wanachama?