Tutaendelea kutayarisha Bajeti Mbadala, Ndio Upinzani Makini

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Kumekuwa na mada mbalimbali kuhusu mapungufu ya kihariri kwenye Bajeti Kivuli ambayo Kambi ya Upinzani iliandaa na kuwasilisha Bungeni.

Kwa niaba ya wenzangu tulikiri mapungufu haya na kuoomba radhi kwa usumbufu uliotokea. Kwa niaba ya wenzangu wote ninawajibika kwa jambo hili kwani mimi ndio mwenye mamlaka ya mwisho ya kuwasilisha Hotuba yetu kwenye Baraza la Mawaziri Kivuli na hatimaye Bungeni. Ninawajibika mapungufu yote yaliyotokea. Ninaahidi kwamba tutaboresha zaidi miaka inayokuja.

Kulikuwa na makusudi kwenye mapungufu?

Hapana. Utaona kwamba nambari ambazo hazikuwekwa kwenye Jedwali zilikuwepo kwenye hotuba. Kosa ilikuwa ni kusahau kuhamisha nambari za vyanzo vya mapato ambazo viliweza kufikia tshs 11tr tulizoweka kama mapato ya ndani. Sio kweli kwamba tuliweka Mapato Sifuri. Mapato yote ya ndani ya Serikali tuliweka jumla yake na kusahau kuweka vyanzo kama Mapato ya kikodi, mapato yasiyo ya kikodi na mapato ya halmashauri. Tulipoona mapungugu hayo tulikrekebisha mara moja. Hapakuwa na makusudi yeyote isipokuwa tunfanya kazi kwenye mazingira magumu sana. Waziri Kivuli wa Fedha anasaidiwa na kundi dogo la 'interns' na wataalamu wengine walio nje ya Bunge. Hivyo kosa kama hili la kiuhariri linaweza kutokea. Tumezingatia hasira za wanachama na wapenzi wetu na hivyo tunaahidi kwamba tutaangalia kwa kina zaidi hotuba zetu zinazofuata.

Hakuna haja ya kuwa na Bajeti Mbadala?
Upinzani wowote makini lazima uwe na uwezo wa kutoa mawazo tofauti, hatuwezi kuwa watu wa kulalamika tu bila kuonyesha sisi tungefanya nini. Tumekuwa tunatoa Bajeti Mbadala kila mwaka tangu mwaka 2007 na mafanikio yamekuwa makubwa sana.

Tumeboresha hotuba zetu mwaka hadi mwaka na hoja zetu zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kuboresha Mapato. Changamoto kubwa sana tuliyonayo ni namna bora ya kusimamia uwajibikaji katika matumizi ya Serikali ambayo yanakua siku hadi siku.

Mwaka jana katika Bajeti mbadala, tulishauri kuhusu tozo ya SDL itumike kugharamia elimu ya Juu. Serikali ilichukua wazo hili. Mwaka huu tumependekeza kwamba tozo hii pia itolewe na Mashirika ya Umma, Serikali imekubali. Mabadiliko haya yataingiza zaidi ya Tshs 320bn na kuweza kulipia mikopo wanafunzi takribani 120,000 ikiwemo fedha kwa ajili ya VETA.

Mwaka jana katika Bajeti mbadala tulipendekeza kutunga sheria kuzuia makampuni makubwa ya nje yanayouziana 'assets' zilizopo Tanzania bila kulipa kodi. Mwaka huu Serikali imetekeleza wazo hili. Kuanzia sasa mauzo ya rasilimali zetu yaliyokuwa yanafanywa holela sasa yamezuiwa kisheria. Changamoto ni utekekezaji kutokana na ufisadi uliokithiri katika mfumo wa Serikali na wakusanya mapato.

Kuna jumla ya mapendekezo 10 katika Bajeti Mbadala ya mwaka huu yamekubaliwa na Serikali. Tunatendelea kutoa mawazo zaidi ili kuboresha nchi yetu na kuwaonyesha Watanzania kuwa tukikabidhiwa dola tunaweza kuendesha nchi bila mashaka yeyote.
 
tatizo ni kwamba hata mkiweka budget mbadala haitasaidia kitu, ccm wapo wengi bungeni so they will always approve budget za serikali bila kuangalia kwa undani kama zinaleta faida gani kwa wananchi wake
 
Safi sana hon zitto kwa ufafanuzi na hii inaonesha kuwa chama chetu kipo kwa ajili ya watu na kinasikiliza watu na hapa ndio tunatimiza falsafa yetu ya nguvu ya umma.

Peoples... Power.........
 
Ni jambo jema mkigundua kuwa umakini ni muhimu katika kazi zenu.
Pia inapendeza kuonyesha njia na kusaidia watanzania kwa kuboresha bajeti ya nchi maana wanaoumia ni watanzania na si Magwanda.
 
tatizo ni kwamba hata mkiweka budget mbadala haitasaidia kitu, ccm wapo wengine bungeni so they will always approve budget za serikali bila kuangalia kwa undani kama zinaleta faida gani kwa wananchi wake
Mbona ameeleza kuwa mapendekezo 10 ya bajeti ya upinzani yamekubaliwa na serikalli. Tatizo CCM wanaona aibu na walidhani watauaminisha umma kuwa CDM hawawezi kwa kosa dogo la kiuhariri.
 
I wish CCM wangejifunza kwenu angalau hili la kukiri mapungufu hadharani!! Huku ndiyo kukomaa tunakotaka na wala siyo kufanya ushabiki kwa kila kitu!!!!!
 
Zitto;

Umefanya vema kujitokeza na kuweka bayana jambo hili, kwani tayari maadui zetu sisi watanzania ambao ni CCM wamekuwa wakieneza porojo sana katika hili.

Pia naomba niwakumbushe CCM kwamba CHADEMA ina watu makini sana, hivyo msipate shida kwamba kwenye CDM kuna wasomi wachache sana. Nataka niwafahamishe tu kwamba wasomi walio wengi TZ kwasasa wako CHADEMA. Rejea uchaguzi uliopita.
 
Last edited by a moderator:
Zitto,
First, have my accolades for ending the matter with a victory on your side. This is how gentlemen settle critique arising from mistakes they had made. I deserve the authority to claim being among the founders of this issue. I raised a very loud voice through an hypothesis posted here. But so far with an apology statement issued, you've my pardon and gradually you can regain my trust.
 
Zitto.

Kwa nini mnawatenga wapinzani wenzenu kwenye maswala muhimu kama haya ya kuunda bajeti hamuoni kama bajeti yenu mnayoiita ya upinzani inakosa nguvu inaoneka ni ya Chadema aina picha ya upinzani...watu kama Prof Lipumba, Dr Sengodo Mvungi ni washauri wazuri upande wa upinzani lakini mnashindwa kuwatumia mnaonekana wabinafsi watu wanashindwa kuwatofautisha na CCM.
 
Last edited by a moderator:
Kauli kama hizi hazijengi jaribu kuwa binadaam japo kidogo,
kinachofanywa na upinzani ni kwa faida ya wa Tanzania wote ukiwemo na wewe, usipende kujiangalia wewe kwa kuwa umeshiba kuna mamilion wana njaa,wakiwemo wa ukoo wako.

Chadema wana ubinadamu gani mkuu zaidi ya kuendekeza ubaguzi?? (kwa vitendo)
 
Kumekuwa na mada mbalimbali kuhusu mapungufu ya kihariri kwenye Bajeti Kivuli ambayo Kambi ya Upinzani iliandaa na kuwasilisha Bungeni. Kwa niaba ya wenzangu tulikiri mapungufu haya na kuoomba radhi kwa usumbufu uliotokea. Kwa niaba ya wenzangu wote ninawajibika kwa jambo hili kwani mimi ndio mwenye mamlaka ya mwisho ya kuwasilisha Hotuba yetu kwenye Baraza la Mawaziri Kivuli na hatimaye Bungeni. Ninawajibika mapungufu yote yaliyotokea. Ninaahidi kwamba tutaboresha zaidi miaka inayokuja.

Kulikuwa na makusudi kwenye mapungufu?

Hapana. Utaona kwamba nambari ambazo hazikuwekwa kwenye Jedwali zilikuwepo kwenye hotuba. Kosa ilikuwa ni kusahau kuhamisha nambari za vyanzo vya mapato ambazo viliweza kufikia tshs 11tr tulizoweka kama mapato ya ndani. Sio kweli kwamba tuliweka Mapato Sifuri. Mapato yote ya ndani ya Serikali tuliweka jumla yake na kusahau kuweka vyanzo kama Mapato ya kikodi, mapato yasiyo ya kikodi na mapato ya halmashauri. Tulipoona mapungugu hayo tulikrekebisha mara moja. Hapakuwa na makusudi yeyote isipokuwa tunfanya kazi kwenye mazingira magumu sana. Waziri Kivuli wa Fedha anasaidiwa na kundi dogo la 'interns' na wataalamu wengine walio nje ya Bunge. Hivyo kosa kama hili la kiuhariri linaweza kutokea. Tumezingatia hasira za wanachama na wapenzi wetu na hivyo tunaahidi kwamba tutaangalia kwa kina zaidi hotuba zetu zinazofuata.

Hakuna haja ya kuwa na Bajeti Mbadala?
Upinzani wowote makini lazima uwe na uwezo wa kutoa mawazo tofauti, hatuwezi kuwa watu wa kulalamika tu bila kuonyesha sisi tungefanya nini. Tumekuwa tunatoa Bajeti Mbadala kila mwaka tangu mwaka 2007 na mafanikio yamekuwa makubwa sana. Tumeboresha hotuba zetu mwaka hadi mwaka na hoja zetu zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kuboresha Mapato. Changamoto kubwa sana tuliyonayo ni namna bora ya kusimamia uwajibikaji katika matumizi ya Serikali ambayo yanakua siku hadi siku.

Mwaka jana katika Bajeti mbadala, tulishauri kuhusu tozo ya SDL itumike kugharamia elimu ya Juu. Serikali ilichukua wazo hili. Mwaka huu tumependekeza kwamba tozo hii pia itolewe na Mashirika ya Umma, Serikali imekubali. Mabadiliko haya yataingiza zaidi ya Tshs 320bn na kuweza kulipia mikopo wanafunzi takribani 120,000 ikiwemo fedha kwa ajili ya VETA.
Mwaka jana katika Bajeti mbadala tulipendekeza kutunga sheria kuzuia makampuni makubwa ya nje yanayouziana 'assets' zilizopo Tanzania bila kulipa kodi. Mwaka huu Serikali imetekeleza wazo hili. Kuanzia sasa mauzo ya rasilimali zetu yaliyokuwa yanafanywa holela sasa yamezuiwa kisheria. Changamoto ni utekekezaji kutokana na ufisadi uliokithiri katika mfumo wa Serikali na wakusanya mapato.
Kuna jumla ya mapendekezo 10 katika Bajeti Mbadala ya mwaka huu yamekubaliwa na Serikali. Tunatendelea kutoa mawazo zaidi ili kuboresha nchi yetu na kuwaonyesha Watanzania kuwa tukikabidhiwa dola tunaweza kuendesha nchi bila mashaka yeyote.
Mkuu Zito, umefanya vyema kuja kutupatia ufafanuzi. Ushauri wangu kwenu, next time, you must have more than two eyes kwenye final product!, nimenote haya ni baadhi ya makosa madogo madogo Chadema mnafanya!. Nakubaliana na wewe kabisa kuwa no one is parfect, lakini katika hali ilivyo sasa, kwa vile CCM has not only failed us, but has also fu..d us so many times for so many years!, hivyo watu wame despair na wana too much great expectations on Chadema!, hivyo vikosa vidogo vidogo kama hivi, vinaihang credibility yenu on at stake.

Wish you all the best!.
 
Zitto.

Kwa nini mnawatenga wapinzani wenzenu kwenye maswala muhimu kama haya ya kuunda bajeti hamuoni kama bajeti yenu mnayoiita ya upinzani inakosa nguvu inaoneka ni ya Chadema aina picha ya upinzani...watu kama Prof Lipumba, Dr Sengodo Mvungi ni washauri wazuri upande wa upinzani lakini mnashindwa kuwatumia mnaonekana wabinafsi watu wanashindwa kuwatofautisha na CCM.

Mkuu nchi hii chama cha upinzani ni CDM tu,vingine vyote ni mawakala wa CCM
 
Last edited by a moderator:
Zitto.

Kwa nini mnawatenga wapinzani wenzenu kwenye maswala muhimu kama haya ya kuunda bajeti hamuoni kama bajeti yenu mnayoiita ya upinzani inakosa nguvu inaoneka ni ya Chadema aina picha ya upinzani...watu kama Prof Lipumba, Dr Sengodo Mvungi ni washauri wazuri upande wa upinzani lakini mnashindwa kuwatumia mnaonekana wabinafsi watu wanashindwa kuwatofautisha na CCM.

Kama Lipumba mwenyewe alikuja na kauli ya kuiponda CDM kwenye vyombo vya habari,
Unategemea CUF itakuwa upande gani?
CUF ni wife wa Magamba si mpinzani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom