Tutaendelea kuishi chin ya dola mpaka lini??

schulstrasse

Senior Member
May 31, 2010
108
0
Habarini wandugu, najua hili swali si geni saana kwetu wote tukizingatia Tanzania ni miongoni mwa nchi TAJIRI sana kwa mali asili na ni moja kati ya nchi MASKINI saana KIUCHUMI, wengi wa wananchi wake tunaishi chini ya dola moja kwa siku, hili nimelishuhudia mwenyewe kwa macho yangu, ndugu zetu vijijini bado wanaishi KIUJIMA na ni kama vile wamesahaulika na serikali yao pamoja na jumuia iliyobahatika kuishi juu ya dola moja kwa siku. Elimu, afya, chakula bora, miundo mbinu na Media ni tatizo sana kwa watanzania halisi waishio vijijini. Wengi wetu humu JF angalau kaelimu tumepata hivyo uwezo wa kuchanganua mambo yanayohusu nchi yetu tunao tofauti na wenzetu wa kijijini ambao wengi wao maskini hata shule hawana na hawajui dunia inaendaje manake vyombo vya habari haviwafikii hivyo taarifa muhimu na mstakabali wa nchi hawaujui. Swali langu ni kwamba asilimia kubwa ya watanzania tutaendelea kuishi chini ya dola moja kwa siku mpaka lini ukizingatia rasilimali tunazo na hatujawahi kuwa na machafuko ya amani nnchi ukilinganisha na nchi za jirani, nini Tatizo? sababu zake? na nini kifanyike manake :doh:!
 
yeah tatizo linaweza kuwa mfumo wa Siasa hasa chama tawala na sera zake, lakini mbona hata kabla ya JK kuwa raisi hali ilikuwa mbaya kiuchumi??unahisi Slaa ataleta mabadiliko au??
 
Back
Top Bottom