Tutachati baadae MPENZI wangu, niko na hili kubwa jinga...

tungeendelea kukenua ili watu wa pembeni wasijue kuna soo maana tumeshawapagawisha kwa mapenzi yetu halafu nisingemuliza chochote. silence kill faster
 
Hapo ni kumwambia tu mrudi nyumbani, halafu unajipa muda wa kumchukulia hatua.
Usiwe na haraka kabisa coz ni mke wako wa ndoa.
just take your time, wala usimuulize chochote maana ushahidi unao tayari.
 
hahaahaaaa,eti kubwa jinga,ndio hivyo tena maigizo yamezidi sana kwenye taasisi yetu hii
 
kwa trend hii itafika wakati watu watakuwa hawaoi au kuolewa... mnabaki kuwa friends with benefits tu or even f**k buddies, no strings attached...
 
ningepotezea wala simuulizi,,, nitaendelea kufurahi nae kama kawaida,, hata tukienda nyumbani wala simuulizi tena hiyo siku nitaongeza mapenzi kwake,,, UNAJUA KWA NINI?? adhabu ya mzinzi ni kutokumuuliza pindi unapogundua uzinzi wake na yeye akajua kuwa umejua YANI IYO NI ADHABU TOSHA,, na lazima ataachana na huyo awala yake,, na usije ukashangaa anaondoka mwenyewe kwenda kujishtaki kwa wazazi maana hajui unamfikiria nini kwa ukaaji wako kimya pasipo kumuuliza
 
sitaki yanikute.................. du, mimi ndo ningetoka mwenyewe ningetangulia nyumbani, ukirudi utanionea huruma mwenyewe maana jinsi nitakavyokuwa.................
 
kwaaa kwaaa kwaaa....teeeheee teeeheeee.ni ngumu lakini mnakausha ,mnakula mnashiba,tibwiri la Asha Ngedere hooomeeee!!!!!!
 
duu! ila ndo ndoa za kisasa zinavyoendeshwa inauma lakin no way out, huwezi mtambua mtu ka kumwangalia tu. Unamsamehe madam alishajua uchafu wake umejulikana kama ana akili timamu atajirekebisha.
 
hata ukimuadhibu haisadii kwa sababu hivyo ndivyo anavyokuona (i.e kubwa jinga) .... ni ngumu sana kubadilisha perception ya mtu once ikishakuwa created

Hayo makofi lengo lake si kubadili perception yake bali kui- reinforce hiyo perception yake kuwa yes indeed me ni kubwa jinga. Na atakula makofi ya kutosha aiseeee!
 
Hapo uamuzi wa haraka ni kuendelea na matanuzi!
Halafu uchunguzi baadaye japo itauma sana,lakini tambua kuwa huyo ni mke wako wa ndoa!
 
mi na act normal,sionyeshi changes zozote!!nampa psychological torture,ataomba mwenyewe talaka
 
ningenyanyuka niende zangu home, napitia kwa mangi naagiza pombe ya kutosha ya kunizima mpaka asubuhi, pakikucha ntakua na mawazo mapya, ofcoz sitaki kumtoa meno af asingizie nlikua nimelewa!!!
 
sitaki yanikute.................. du, mimi ndo ningetoka mwenyewe ningetangulia nyumbani, ukirudi utanionea huruma mwenyewe maana jinsi nitakavyokuwa.................

Utakuwaje FP? Utajulikana tu unaigiza.
 
Yani huyo ni kumfurahia na kuzidisha upendo mpaka atajishtukia mwenyewe...........
 
ningepotezea wala simuulizi,,, nitaendelea kufurahi nae kama kawaida,, hata tukienda nyumbani wala simuulizi tena hiyo siku nitaongeza mapenzi kwake,,, UNAJUA KWA NINI?? adhabu ya mzinzi ni kutokumuuliza pindi unapogundua uzinzi wake na yeye akajua kuwa umejua YANI IYO NI ADHABU TOSHA,, na lazima ataachana na huyo awala yake,, na usije ukashangaa anaondoka mwenyewe kwenda kujishtaki kwa wazazi maana hajui unamfikiria nini kwa ukaaji wako kimya pasipo kumuuliza
Ningefuata hatua zako, lakini kwa marekebisho madogo tu - tukifika nyumbani ninamtumia ujumbe kumwambia "ni kweli mpenzi, mimi mjinga mkubwa lakini kosa lako ni kunierevusha". Bila ya shaka atataka kujieleza na kujitetea na mimi nitakuwa tayari kumsikiliza mpaka mwisho lakini bila ya kusema wala kuongeza lolote. Nitamwacha ajitese mwenyewe kisaikolojia. Siku nikihisi anafikiri yameisha, ndio ninamtwanga njano mbili na nyekundu moja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom