Tutachati baadae MPENZI wangu, niko na hili kubwa jinga...

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,181
409
Upo na mkeo kwenye eneo la matanuzi, hapo mmeagizia pombe na mnasubiri msosi wanguvu mle muondoke nyumbani
Mazungumzo yenu hapo ni ya amani na vicheko kwa sana. Mara mgongeshane mikono, mara mpigane mabusu ya uhakika.
Wateja wengine wanawaangalia huku wakisema"Wale lazima watakuwa mahawara tu, mke na mume huwa hawana kawaida yakucheka na kupigana mabusu mbele ya watu"

Wewe unawasikia na unamwambia mkeo awasikilize kisha mnacheka sana maana kwenu kuoneshana upendo hadharani ni jambo la kawaida.
Mara inaingia meseji kwenye simu ya mkeo, lakini yeye badala ya kuisoma anaendelea kupiga domo na wewe, mwisho unamwambia "Dear, ungeisoma hiyo meseji pengine alietuma ana imejensi"
mkeo anasema hakuna wakumtumia imejensi yeyote, watu wasumbufu sana " Tena kama sio Mwajuma huyu atakua Nuru, maana hao ndio wanapenda sana kuchati, mi wananikera sana", mke anakwambia.

Mkeo anachukua simu yake na kuisoma meseji, ukimwangalia usoni kama anakasirika, lakini pia kama anataka kuachia tabasamu,
Mara anachanganya vidole kuandika meseji nyingine. Wewe unajua anajibu iliyoingia. Ile anaweka simu mezani tu anashika kichwa na kusema;
"Mama weee."
Kabla hujamuuliza nini kimempata, simu yako inaingia meseji, unaishika kuifungua unaona jina la mkeo, maana umemsevu 'MY WIFE.'
MY WIFE:"Tutachati baadae mpenzi wangu, niko na hili kubwa jinga. Lakini elewa nakupenda sana mwaaaaaa."

Je, kama wewe ungechukua uamuzi gani???...
 
Ningeliweka wazi kwake ili ajue najua nini kibaya annifanyia kwenye mahusiano yetu

Uamuzi wa kwanza ni kumwambia Twende ANGAZA tukaaenze kujihahkiki afya zetu

Na baada ya hapo ningeanza kuona / kuchunguza kama anamadiliko ktk hili

Maamuzi yoyote yatategemea na ni jinsi Gani na mimi ni MSAFI ktk Ndoa/Mahusiano tuliyonayo

UKIWA MCHAFU kwa nini umuhukumu mwenzako kwa hilo???
 
Kweli utakuwa umetumia busara mkuu, yanini kumhukumu mwenzio kama nawewe sio msafi...
 
ningeendelea kukaa hapo km dkk 10 huku nikicheka naye kama mwanzo then namwambia twende home tunaondoka hk nimeweka mkono wangu kiunoni mwake, nampeleka home then NAMPA KIPIGO CHA MBWA MWIZI AFUNGASHE MIZIGO YK ASEPE kesi itaongelewa badae
 
Humpi hata nafasi ya kujirekebisha?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom