Tutaacha lini kukosa ubunifu? "Visit Tanzania" kwanini isiwe "Karibu Tanzania"?

Mimi sina takwimu yeyote na ndio maana sikuegemea katika msimamo wowote. Ukitoa msimamo unaohusisha data basi ni lazima uthibitishe msimamo wako kwa kutoa takwimu. Idadi kubwa ya wafuatiliaji wa Simba ni watu wasio watanzania ukilinganisha na watanzania. Hivyo ili isionekane ni hisia atupe takwimu inayoonesha hayo aliyoyasema
Basi ngoma draw. Kila mmoja yupo sahihi. Na hii hujaambiwa ni kwenye page ya simba. Haya mashindano yanaoneshwa hadi ulaya na marekani. Sasa huoni ni njia ya kutangaza? Au hilo hulifahamu? Ulidhani wanapost tu kwnwye page za simba insta na facebook?😁
 
Visit sio 'Karibu' kwa kiswahili... 'Tembelea'.

Anza kwa kujifunza hiyo unayodai ni lugha yako kwanza.
 
Klabu cha Simba kimeweza kuisaidia Tanzania kujitangaza kwa bila malipo huku ukivaa fulana zao kifuani zikiwa na neno VISIT TANZANIA tukiiga kutoka kwa VISIT RWANDA.

Ni jambo jema sana Simba wanafanya kama ni kweli hakuna malipo. Lakini Rais wetu anapigia debe sana Kiswahili kuwa kijulikane na tumepata bahati hii ya kubebwa na Simba SC.

Kwanini tusitumie neno KARIBU TANZANIA?
Nje ya mada kwanini umejiita rufiji dam na sio mwalimu nyerere dam Kama ilivyopewa jina jipya?
 
Tusijadili sasa hivi ngoja tuone implementation yake kwanza kwa sasa ndiyo tutaifanyia mabadiliko
 
Mkuu nenda usome upya hiyo project ya Visit Tanzania,simba haikuiga kwa Rwanda,Tanzania ishawahi kufanya hilo kupitia club ya sunderland miaka ya nyuma.
 
Kununua T shirt lako halafu andika karibu Tanzania,simple like that.usiwapangie maana hujawachangia chochote
 
Inbound Tourism ndio inayolengwa hapa kwenye Market ni lazima mtu natumia nguvu ndogo katika kuelewa kitu kinacholengwa

Mfano ukiandika Karibu Tanzania Mmarekani haelewi Visit Tanzania watu wanaelewa

India wana Incredible India wameweka makusudi ili kila mtu aweze kuelewa wangeweza kuandika अतुल्य भारत lakini wakaamua kuandika incredible India

Malaysia wangeweza andika malaysia benar-benar Asia ila wameamua kuandika Malaysia Truly Asia sio Wajinga na hata Sisi sio Wajinga
Klabu cha Simba kimeweza kuisaidia Tanzania kujitangaza kwa bila malipo huku ukivaa fulana zao kifuani zikiwa na neno VISIT TANZANIA tukiiga kutoka kwa VISIT RWANDA.

Ni jambo jema sana Simba wanafanya kama ni kweli hakuna malipo. Lakini Rais wetu anapigia debe sana Kiswahili kuwa kijulikane na tumepata bahati hii ya kubebwa na Simba SC.

Kwanini tusitumie neno KARIBU TANZANIA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom