Tutaacha lini kukosa ubunifu? "Visit Tanzania" kwanini isiwe "Karibu Tanzania"?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,801
8,786
Klabu cha Simba kimeweza kuisaidia Tanzania kujitangaza kwa bila malipo huku ukivaa fulana zao kifuani zikiwa na neno VISIT TANZANIA tukiiga kutoka kwa VISIT RWANDA.

Ni jambo jema sana Simba wanafanya kama ni kweli hakuna malipo. Lakini Rais wetu anapigia debe sana Kiswahili kuwa kijulikane na tumepata bahati hii ya kubebwa na Simba SC.

Kwanini tusitumie neno KARIBU TANZANIA?
 
Statistics zinaonyesha Simba ni Klabu ya mpira wa miguu iliyoongoza kufuatiliwa katika mitandao ya kijamii mwaka 2020, Mitandao mingi inatumia Kiingereza na watumiaji wake wengi wanatumia na wanaelewa Kiingereza. Maneno “Visit Tanzania “ yaliyotumika yamefikisha ujumbe kwa haraka zaidi kuliko wangetumia “Karibu Tanzania “

Wangetumia kiswahili ingechukua muda mrefu kidogo kwa sababu Wanaotangaziwa wengi wao hawajui kiswahili. May be next time watakuja na lingine kwa kiswahili

The same question waulize Rwanda, kwa nini wasiandike Kinyarwanda kweny jezi ya Arsenal 😬😬😬 binafsi mimi sijui kinyarwanda ila nilivoona visit rwanda chap nikaelewa mchezo mzima😃 na nikipata hela nitawatembelea one day
 
Klabu cha Simba kimeweza kuisaidia Tanzania kujitangaza kwa bila malipo huku ukivaa fulana zao kifuani zikiwa na neno VISIT TANZANIA tukiiga kutoka kwa VISIT RWANDA. Ni jambo jema sana Simba wanafanya kama ni kweli hakuna malipo. Lakini Rais wetu anapigia debe sana Kiswahili kuwa kijulikane na tumepata bahati hii ya kubebwa na Simba SC, kwanini tusitumie neno KARIBU TANZANIA?
wanaalikwa wazungu kuja tanzania, unatumiaje kiswahili sasa
 
Ni hoja nzuri ila hapo tatizo linatokea katika ufanisi wa kauli husika ukisema Karibu Tanzania itabidi utoe maana ya neno Karibu kwa hao unaowataka waje kutembelea Tanzania. La sivyo utapoteza itakua kazi bure neno karibu tutalitumia muda tukiwapokea Airport ila tukiwafuata kwa Visit Tanzania ni bora zaidi.
 
Statistics zinaonyesha Simba ni Klabu ya mpira wa miguu iliyoongoza kufuatiliwa katika mitandao ya kijamii mwaka 2020, Mitandao mingi inatumia Kiingereza na watumiaji wake wengi wanatumia na wanaelewa Kiingereza. Maneno “Visit Tanzania “ yaliyotumika yamefikisha ujumbe kwa haraka zaidi kuliko wangetumia “Karibu Tanzania “

Wangetumia kiswahili ingechukua muda mrefu kidogo kwa sababu Wanaotangaziwa wengi wao hawajui kiswahili. May be next time watakuja na lingine kwa kiswahili

The same question waulize Rwanda, kwa nini wasiandike Kinyarwanda kweny jezi ya Arsenal binafsi mimi sijui kinyarwanda ila nilivoona visit rwanda chap nikaelewa mchezo mzima na nikipata hela nitawatembelea one day
Hizo takwimu zinaonesha hiyo population ni ya wapi?
 
Hizo takwimu zinaonesha hiyo population ni ya wapi ?
Usitake kujua location ya population, ila kuongoza kufatiliwa mtandaoni ya umezizidi barcelona, madrid, United ni mafanikio makubwa sana.

Sitaki kuamini watanzania pekee ndo walikua wanafuatilia simba, na haikua champions league lkn bado iliongoza

What if angekua champions league?
 
Umeongea kihisia sana kuliko kutoa uhalisia. Inawezekana Simba ikawa inaongoza kwa kufatiliwa zaidi lakini hao wafuatiliaji wakawa asilimia kubwa ni watanzania. Embu tuambie katika hao followers wa Simba ni wangapi sio Watanzania? Na wangapi ni Watanzania. Tupe takwimu
 
Hajielew huyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom