Tususie Matokeo Ya Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tususie Matokeo Ya Uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Muke Ya Muzungu, Nov 2, 2010.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania, kama mnavyofahamu, NEC ilipoona mwelekeo wa matokeo ya Urais, mara moja walibadilisha kibao na kuanza kutangaza wenyewe toka makao makuu na siyo jimboni tena. Hii inamaanisha yakwamba wanalo lao jambo

  Sisi wapiga kura tena walipa kodi kwa miaka zaidi ya 40 sauti zetu zimekuwa hazina maana, na hata kodi zetu kutumiwa vibaya na wakina Kikwete na familia zao. Kura zetu haziwezi kuchezewa tena. Kura lazima zitangazwe kwenye kila jimbo au kituo cha kupigia kura na hata NEC wakiyatangaza, yawe ni yale yale vinginevyo hatutavumilia na tutasusia hadi uchaguzi mwingine wa Rais ufanyike

  Tumechoka kuburuzwa na kundi la kikwete, tumechoka naye na uvumilivu wetu umefika mwisho. Tupo tayari kujitoa mhanga ili watoto wetu wawe na maisha ya baadae. Waniue lakini msimamo wangu hautabadilika. Shida niliyonayo, ni heri nife kuliko kuona uhuru wangu na haki yangu ya msingi inachezewa na wakina Ridhiwani wakiendesha magari ya kifahari
   
 2. The Good

  The Good Senior Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Shida yako ni Demokrasia au kuona Ridhwani akipanda dala dala. Kwa hali ilivyo popote ambapo matokeo yatatangazwa JK ataibuka kidedea. Mpaka sasa maximum number of seats kwenda Chadema ni 20. Wabunge wa upinzani hawatazidi 35 kwenye bunge lenye wabunge over 250. So where is your hope?
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Endelea kuota
   
 4. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wee the Good

  Unasemaje 35, wakati CUF peke yao wanao 22?

  Kama 5 wa CHADEMA walifanya vizuri, 35 je?
   
 5. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mimi nilikwisha sema si tu kwa ajili ya kutotoa matokeo ya tume lakini hata la kuzuia wapiga kura vituoni kwa ubabaishaji!!!!!!!!
   
 6. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  sawa kabisa.Mpaka sasa sijaiona mantiki ya kupoteza fedha nyingi kwenye uchaguzi ikiwa maamuzi ya wananchi hayaheshimiwi.Hivi kwani wao ni nani hata watuburuze kiasi hiki?kwa nini watanzania tunakosa ujasiri wa kupambana na hawa mafirauni?Watz wenzangu,muda wa kuwaachia watuburuze umekwisha sasa,tuondoe woga tupambane nao,SHIME WATz tupiganie haki yetu!
   
 7. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  MGsalon nakubaliana nawewe 101%. Ushindi wetu hautaletwa na mafisadi bali sisi wenyewe kwa kujitoa muhanga. Twende mbele na kudai haki yetu. Tusikubali kuibiwa kura kirahisi
   
 8. K

  Konaball JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
   
 9. M

  Mnyankole Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WRONG BROTHER!! what about the 18 CUF seats in Zanzibar and already TLP and NCCR-MAGEUZI each has one seat? It's coming to 40 and we count on some more!!!!!

  Mind you, if the 5 MPs from CHADEMA caused that much HAVOC in the parliament, what about 50 more? SASA BUNGE LITANYOKA!!!!
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Tatizo hapa ni utekelezaji wake.......

  Jk na CCM yake wakishakutangazwa wao wanaendelea na kuchapa kazi kama waonavyo yafaa...........sasa utasusa vipi?
  Labda uende mahakamani kupinga matokeo vinginevyo ni kujipanga upya kudai demokrasia tu................
   
Loading...