Tususie Huu Mchakato wa Sensa, sababu na uwezo wa kufanya hivyo tunavyo...lets do it!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tususie Huu Mchakato wa Sensa, sababu na uwezo wa kufanya hivyo tunavyo...lets do it!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vato, Jun 15, 2012.

 1. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Watanzania tunapenda sana kulalamika na kulaani bila kuchukua hatua.Hatuna courage na audacity ya kwenda step moja mbele na ku act badala ya kulalamika tu miaka nenda miaka nenda rudi. Ukimya na Uoga wetu huu ndio sababu kubwa zinazoifanya serikali ya CCM inakiburi, ina jeuri na dharau kwetu..ni ukosefu wetu wa uthubutu wa kuihoji na kuikaripia serikali ndio maana tuliambiwa mtakula hata nyasi ikibidi, lakini ndege ya rais itanunuliwa, ndio maana tuliambiwa pigeni hata mbizi mwende kigamboni kama ongezeko la nauli ya kivuko mnaona ni kubwa...viongozi wanatoa wapi huu ujasiri wa kutukashifu kama asante ya sisi kuwapa ridhaa ya kutuongoza???!!! ni kwasababu tunaogopa, hata nmaandamano yakiitishwa hatuendi, utamkuta mtu mzima kabisa anasema "nani anataka kupigwa mabomu ya machozi", anaogopa ku risk maisha yake ili atetee maslahi mapana ya kizazi hiki na zaidi kizazi kijacho.

  Jana serikali kwa makusudi kabisa imewasilisha bungeni bajeti ambayo itamzidishia maskini ugumu wa maisha mara dufu...gawio la fedha kwenye sekta inayoajiri zaidi ya asilimia 50 ya watanzania wote, Kilimo, limepungua kwa kiasi kikubwa. Serikali badala ya kubuni vyanzo vipya vya mapato kila mwaka inapandisha kodi katika bidhaa na huduma zile zile, kila mwaka wa fedha utasikia sigara, bia, soda, vinywaji vikali bei juu, kila mwaka lazima bidhaa hizi zichajiwe kodi...na mwaka huu na vocha nazo zinapigwa kodi kwanzia Jully...tunaelekea wapi sasa?? makato yote haya ya kodi mwisho wa siku yanageuka kuwa mzigo mzito mabegani mwa watanzania maskini..ndio maana yake!!! kwanini serikali haibuni vyanzo vipya endelevu vya mapato???? kama hakuna wataalamu wanaoweza kufanya hiyo kazi si wawaajiri washauri elekezi/ consultants kutoka kwenye makampuni ya kimataifa ya ushauri wa mambo ya uchumi na fedha wawasaidie kubuni vyanzo vipya vya mapato??? hapa Tanzania kodi nyingi wanalipa Maskini na Middle class, makampuni makubwa kwenye sekta kama madini na huduma/ tertiary sector, na matajiri wanalipa kodi kidogo mno serikalini!!!! they do not pay their fair share of tax to tax authorities. Hivi katika kudhihirisha kuwa tumechoshwa na hii serikali mbovu isiyotujali watu wake kwanini tusisusie huu mchakato wa Sensa kama walivyofanya ndugu zetu waislamu kupitia BAKWATA??? tuususie huu mchakato wa sensa kuishinikiza serikali isikilize vilio vyetu tunavyovitoa kupitia NGOs na vyama vya siasa kama CHADEMA nk..kwanzia kwenye ile sheria ya marekebisho ya katiba, huduma mbovu za kijamii hasa afya na elimu, ufisadi uliokithiri serikalini, kupanda kwa gharama za umeme, nk..tususie huu mchakato kama taifa kila mmoja kwa wakati wake...tutumie mitandao ya kijamii kuhamasishana kuususia huu mchakato...ni wajibu wetu kama kizazi kuitaka serikali iwajibike, kuitaka serikali ifanye mabaddiliko ya kiutendaji ili iweze kuwatumikia wananchi vizuri, huu wajibu tusipoutekeleza leo vizazi vijavyo vitatudharau...alisema Frantz Fanon kuwa, EACH GENERATION MUST OUT OF RELATIVE OBSCURITY DISCOVER ITS MISSION, FULLFILL IT OR BETRAY IT..kinachotokea hapa Tanzania ni kwamba tupo katika juhudi za makusudi kabisa za kujitahidid kama taifa kutokutekeleza wajibu wetu wa kufanya mabadiliko, wajibu wa kuiwajibisha serikali ingawa hali halisi inatupa sababu ya kufanya hivyo...
   
 2. i

  isotope JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Aisee, umefikiria sana....hongera! ila cjui kama itawezekana. Bongo hakuna wanaharakati wa ukweli.., ukisikia kikundi fulani kinasusia jambo, ujue mgao wa posho umewapita kushoto, wakikumbukwa tu kelele zote kwisha! hata hao waliotangaza kususia SENSA serikali ikiwapa fungu kuhamasisha watu washiriki sensa, hizo kelele hutazisikia!
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ngoja nifikirie nitarudi.
   
 4. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuunga mkono jambo la kipuuzi kama KUSUSIA SENSA. Hivi nani alikwambia kuwa watakaosusia Sensa ni ndugu zetu?

  Mimi binafsi naichukia CCM mara 100 zaidi yako lkn hilo sio jibu. Hoja za kitoto kama hizo za kususia kitu ambacho hata anayekifanya hajali ukamilifu wake ni kupoteza muda. Hawa wanaosusia SENSA we waache wana yao na mwarabu anayewatuma lkn hii sensa ni muhimu kwetu ili kujua idadi yetu na namna tunavyojipanga kui-replace nyinyiemu madarakani.

  Badala ya kuhamasisha watu kususia SENSA, hamasisha watu kupiga kura mwaka 2015 (mwaka wa ukombozi)
   
 5. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu ulipoanza kuelezea niliona upo katika mlolongo mzuri ambao ulikuwa unanivutia kuunga mkono hoja yako ila ukafika mahali ukaongelea BAKWATA ndipo nikajikuta automatically akili yangu inaanza kurudi nyuma katika kuunga mkono hoja yako nzima. Na sasa nasema kwa sauti kuu kwamba SIUNGI MKONO HOJA
   
 6. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Kwani CHADEMA ni nani, huu ni uamuzi wa wananchi sio wa chama cha siasa!!! Maandamano yalioangusha serikali ktk nchi za kiarabua yalikuwa organised na watu wenyewe sio chama. hatima ya hii nchi iko mikononi mwa wananchi sio chama cha siasa.

  Kususia sensa in the sense of kuirudisha serikali katika meza ya mazungumzo ili tujadili maslahi mapana ya jamii yetu. Sensa itafanyika na tutashiriki, lakini sio kwa ratiba waliyooipanga wao, itafanyika baada ya serikali kusikia vilio vyetu na kuvifanyia kazi...desperate time calls for desperate measures, watu wanafanya mpaka hunger strikes kudai haki zao, watu wana fanya rally kwenye squares kwa miezi kutaka mabadiliko, wote tulisikia vijana wa marekani wali anzisha movement iliyoigwa karibia ulimwenguni kote ya kuhoji huu mfumo kandamizi wa soko huria, ilikuwa inaitwa OCCUPY WALL STREET, lakini hapa Tanzania tunakaa tu halafu tunataka mabadiliko yaje automatically tu bila ku sweat...faida za sensa zipo nyingi, lakini zipo kinadharia tu..

  Tunajua sensa inatoa taarifa za takwimu zinazotumika katika mipango ya maendeleo na mgawanyo wa rasilimali, lakini wote tunajua tatizo la Tanzania sio ukosefu wa takwimu ila lipo katika ufisadi uliopo katika matumizi ya takwimu hizo kuleta impact ktk maisha ya mtanzania wa kawaida...umesema hii sio suluhu ya tatizo, itakuwa vizuri ukitaja tatizo na unayodhani ni njia nzuri ya kuli address hilo tatizo....
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kamwe hatutaunga mkono ujinga wa kugomea Sensa.Tuko pamoja na serikali.Kinachokusumbua ni udini tu.
   
Loading...