Shangani
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 756
- 1,061
Napenda kutoa wito kwa watanzani wote. Tuisaidie serikali na wabunge wetu kwenda kutengeneza sheria bora za madini, gesi asilia na mafuta kwa kutoa maoni yetu. Tutaweza kutoa maoni yetu vizuri kama tutasoma sheria na sera zetu za sasa za madini na gesi asilia na kuona mapungufu yake.
Kazi hii sio ya wanasheria tu bali ni yetu sote. Nawaomba vyombo vya habari nchini vianzishe vipindi maalum kwa ajili ya wananchi kutoa maoni na kujadili sheria na sera za madini na gesi asilia
Watumiaji wa mitandao ya kijamii Facebook, Instagram Twitter na kwenye WhatsApp tujadili sheria hizi kifungu kwa kifungu.
Natumaini mawazo yetu kwa pamoja tutaisaidia serikali kutengeneza sheria bora na nzuri zaidi.