Tusker Lager: Kutoka TBL kwenda SBL, kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusker Lager: Kutoka TBL kwenda SBL, kulikoni?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Zemu, May 12, 2010.

 1. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wandugu wana JF na wapenzi wa Tusker Lager, kuna kitu kinaniumiza kichwa kuhusu hii bia tamu ya tusker ambayo zamani TBL walikuwa wanazalisha under licence na sasa naona SBL.Je kipi kilitokea mpaka hawa SBL wawe ndio wanaimiliki au kuzalisha?. Kwa upande wangu sina imani sana na uwezo wa SBL kwenye kuzalisha bia. Kuna mwenye tetesi ya kilichotokea? :mad2:
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  SBL wako juu tu. Wamewazidi TBL maarifa kwenye ile vita yao ya biashara . Waache wapambane maana afterall this is waht we want . Tbl wamebakia na bia zao za Safari, Kili ,na Castle.
   
 3. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Unajua Tusker ni Bia ya East African Brewaries, Kulikua na mgogoro kati ya EAB na TBL hasa hasa on the issue of Tusker Promotion. EAB wakaamua kuwithdraw licence ya kutengeneza tusker from TBL. for your information, SBL imenunuliwa na EABL
   
 4. J

  Jafar JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  What I understand - wote ni wa shenzi tu. TBL (makaburu) wanapeleka faida nje na hao EABL (wakenya /Diagio) watapeleka faida nje.
  Mwisho wa siku watanzania tumelewa lakini hela yote wamechukua wajanja.

  Kule nigeria wanasema "Shine your eyes" - means watanzania tufungue akili sasa, tuache kupewa peremende wanaondoka na dhahabu
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Well wote ni washenzi kivipi wakati tuliwapa wenyewe? Ulitegemea faida watugawie Bro?. Hiyo haipo kwenye business. Tulikuwa na viwanda vyetu vya TBL na KIBO. Tukawapa hao. Sasa mshEnzi ni nani? WE ARE FOOLS IF YOU WISH TO JUSTFY THEIR USHENZI.
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hivi mkataba wa Makaburu na TBL unaisha Lini? I want to run TBL as a local Investor. Nitatumia unga wa mahindi kama wanavyotumia wao, nitarudisha yale mashamba ya Basutu, na sukari nitanunua hapo Kilombero au TPC Moshi. Maji ya kumwaga yapo tena ya Arusha ni the best. Wapiga kazi wako kibao, na mashine zetu zile za zamani zipo tu wala hazijachoka maana ndio Makaburu wanazitumia . Sasa nitakuwa nimekosa nini wakati kuna viwanja Kibao? Yaani CRDB wataninyima mkopo wa Kununua sukari hapo TPC. Well wakininyima najua TPC watanikospesha tani kadhaa za kuanzia. Wanywaji ndio usiseme maana wengine huanza kukata kiu saa nne asubuhi. KWa nini Makaburu TUUUU?
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  .
  Zemu hii issue ni ngumu kuielewa kwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe, inahitaji utaalamu japo kidogo kujua nini haswa kinaendelea, na kulikuwa na vita kwenye media, iliyoitwa Vita vya Bia 'Beer War'

  Gemu lilianzia kama ifuatavyo, kwanza Tusker ni bia ya Kenya, ya Tanzania ni Ndovu. Kiwanda cha Kibo kule Moshi kilichokuwa kinamilikiwa na EABL ndio kilikuwa kinatengeneza Tusker, kulifanyika makubaliano fulani au hostile take over kati ya TBL na EABL kuwa kila nchi itengeneze bia ya mwenzake na kuiuza nchini kwake. Hawakuuziana kwa pesa bali waligawana kila kiwanda kimiliki asilimia 20% chenzake, yaani 20% EABL imilikiwe na TBL (SUB) nao wamiliki 20%, TBL watengeneze Tusker, EABL watengeneze Castle. Ndipo Ghafla TBL wakakifunga kiwanda cha Kibo na kuwamwaga wafanyakazi karibu wote wakapigwa chini, menejiment wakahamishiwa TBL. Mpaka hii leo sijui kilitokea nini, lakini Tusker ikazalishwa TBL.

  EABL akahisi TBL inaihujumu brand yake ya Tusker na kupromot zaidi Safari na Kilimanjaro, ndipo wakafanya mazungumzo na SBL kuwapa tenda ya kutengeneza Tusker, TBL wakawakatalia EABL kujitoa ubia wao mpaka wakafikishana mbele ya vyombo vya sheria, tume ya Ushindani FCC hadi mahaka ya usuluhishi London. Wakati huo TBL ikakodi vijana kuyahujumu matangazo yoyote ya Tusker ikiwemo kuya vandalize na kuwalazimisha ma ajenti wao wasipokee Tusker, ilikuwa vita kweli, mastatement na mastatement yakitumwa magazetini.

  Mwishowe EABL na SBL wakatoa statement vita imeisha kwa amani na hakuna vita yoyote baada ya kufikia makubaliano kwa amani. TBL nao wakatoa statement yao, hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa.

  Kwa bahati mbaya mimi sinywi kabisa bia (haina maana sinywi pombe), sikujua kabisa hatima ya Tusker mpaka leo ulipouliza.

  Huo ndio uelewa wangu mdogo.
   
 8. B

  Bunsen Burner Member

  #8
  May 12, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  100% correct!! Kenya Breweries bado ni ya Wakenya!! Nambian Breweries with Windhoek lager etc., is still Namibian! But sisi mbumbumbu tuuu na maneno mengi!!!!! kalaghabao
   
 9. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hilo nalo neno, sasa napata picha kamili.Thanks
   
 10. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda hii sentensi niliyobold hapo juu.Wakati wa ukombozi ni sasa, tumechoka na ushenzi huu wa wawekezaji washenzi.
   
 11. G

  Godwine JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ni vita kati ya serengeti na TBL isitoshe inatokana na kuimarika kwa TBL kupelekea kuona
  kwamba inaweza kusimama bila ya EAB hivyo basi walitaka mkataba ushushe gharama
  wanazotozwa kwa kibali cha kuzalisha bia ya tusker hivyo basi serengeti kusikia hivyo
  nao wakatumia mwanya huo kuomba kibali hicho toka kwa EAB kwa hiyo ndivyo ilivyo
   
Loading...