Tusiyoyajua kikao kati ya madiwani waasi wa chadema na kamati ya marando.....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
....Leo kwa mara ya kwanza nimesikia kituko kilichotokea kwenye kikao cha kamati ya Marando iliyoundwa kusimamia suala ya madiwani waasi wa CDM-ARUSHA ambacho sidhani kama kiliwai sikika.

...Inasemekana baada ya wale madiwani kuitwa kwenye kikao kile,kiongozi wao alikwenda duka la vitabu vya Mungu yaani BIBLIA(Jina la duka limeifadhiwa) na kununua BIBLIA moja yenye cover lenye zipu.Baada ya kununua aliipeleka kwa mtumishi mmoja wa Mungu aka Mchungaji(Jina limeifadhiwa) ili aiombee,na baada ya kufanya hivyo akaelekea kwenye kikao cha ile kamati.Baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza huyu jamaa akafungua BIBLIA yake na kuanza kuzungumza maneno haya wakati anaichana baadhi ya kurasa za ile BIBLIA na hapa namnukuu;

"MUNGU kama nilipokea shilingi mia kwa ajili ya muafaka huu,basi ile hela itakuwa imechangamana na damu zetu,tunaomba uikaushe,na MUNGU kama kuna mmoja wetu alipokea hata shilingi mia na kuichanganya na zake,basi kausha hela zote na usimpatie nafasi ya kupata tena,vinginevyo kama kuna mtu hanatumia jukwaa hili kutuchafua,basi umnyime sauti na jukwaa la kutuchafua sisi"


Wakati akiongea maneno hayo alikuwa akichana baadhi ya kurasa za BIBLIA.Na baada ya kumaliza aliifunga BIBLIA yake na kuikabidhi kwa kamati ya Marando na kumwambia naomba akifikishe kwa Dr Slaa.

Mytake:
Huyu diwani alikuwa na ujasiri gani wa kufikia kiwango cha kuchana BIBLIA na kutoa viapo kama hivyo? Na je anadhani Mungu uwa anashughulika na watu wasiotaka kufuata utaratibu? Kutofuata utaratibu wa chama ni dhambi pia kwa Mungu,maana huo ndio utaratibu mliokubaliana kama chama na unapaswa kuheshimiwa na kila mmoja.Lakini pia sidhani kama ishu ni rushwa ya hela tu,hata ukikubali kurubuniwa kwa maneno ili upate cheo fulani pia ni rushwa.Dua la kuku alimpati mwewe!!!

source : Radio Five-Arusha
 
Yatamrudi mwenyewe!
Huyu atakuwa ni John Bayo, aliyekuwa Diwani wa kata ya Elerai.
 
Majibu halisi ni hapo uchaguzi mdogo utakapoitishwa, hivi wametimkia wapi hao jamaa?
Waje kutetea viti vyao!
 
Duh! hakuwa na haja kuapa na kuapiza, bali KWELI yake imaanisheni KWELI..
 
Afu mleta mada anatumiwa na hao wazandiki

Soma vizuri thread wewe,usikimbilie kuchangia kupitia maoni ya wachangiaji wengine,JF ni jukwaa huru,tuko hapa kutoa maoni binafsi yasiyofungwa na mtu mwingine.Tatazo lako umekimbilia kuchangia bila kusoma vizuri na kupata muda wa kutafakari.Huu ndio mfano halisi wa kufikiria kwa kutumia masaburi.
 
Radio Five - Au - Only83

Mkuu mimi nilete habari kama hizi toka wapi? Na kwa taarifa yako waulize watu walisikiliza hii habari,jamaa anaitwa aliyekuwa anatangaza anaitwa David na ameirudia hii habari mara kibao,nikahisi ana lake jambo,na watu walimuuliza kupitia sms kuna nini kimetokea mpaka unaleta hii habari akasema hakuna ila nawapa ndio nimeipata leo.
 
huyo jamaa ndo aliyepewa pesa kwa ajili ya muafaka maana aingii akilini kama una mwamini Mungu kwa maneno yake uchane biblia huu ni usanii mtupu
 
JE, alisalimika? au alikwenda na maji pamoja na mbwembe zote hizo za kudhihaki vitabu vya Mungu?
 
Back
Top Bottom