Tusiwe wanafiki, ni kweli standard operating procedures za majanga kama tetemeko hazikufuatwa

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Mwaka huu tetemeko limetikisa, Kitengo cha maafa kinatakiwa kiitikie mara moja na kwa haraka, lakini tunaenda masaa 96 hakuna "Rapid Response" yoyote kutoka "Kitengo cha Maafa" toka Ofisi ya Waziri Mkuu. Hiki kitengo kilipitishiwa bajeti lakini mpaka sasa hakijapeleka si maturubai, mahema, chakula wala hata maji safi kwa wahanga. Sasa kweli kuna maaana ya hiki kitengo kupewa pesa na Bunge?

Kuna Standard Operating Procedures for Disaster Mgt (SOP),na hasa hizi "Natural Hazards" kama tetemeko na mafuriko. Kuanzia "zero hour","Past zero hour","Day One","Day Two" nakuendelea na siku zinazofuata kulingana na ukubwa wa tatizo. Hizi SOPs zinatakiwa kuwa implemented na Kitengo cha Maaafa toka ofisi ya Waziri Mkuu. Kila hatua ina namna yake ya uwokozi. Lakini mpaka leo siku ya tano bado serikali inafanya "procedures" za "Zero hour" wakati ilitakiwa kuwa kwenye "Day Two and Nth"

Ndani ya masaa 24 tulitakiwa tuwe tunapata taarifa ya mwenendo wa majanga toka kituo maalumu cha habari kilichopo Bukoba, kituo kinachoratibiwa na ofisi ya PM. Kuwe na team maalumu wa wataalamu wa afya, team ya Wanasaikolojia na washauri ili kuwafariji na kuwajenga wale waliopatwa na mshtuko ktk maeneo ya majanga.

Zero Hour huwa ni dakika 45 baada ya tukio,kamati za Maafa za Mkoa na Wilaya chini ya kamati ya Ulinzi na Usalama hukutanika. Hapa huwa ni hatua ya kwanza kuhakikisha wadau wa maafa wamekusanywa kwa ngazi ya Mkoa/Wilaya na kuanza kazi haraka. Wadau kwa nchi kama yetu ni JWTZ,JKT, Scouts, Red Cross, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Volunteers. Hawa wanatakiwa kupata muongozo na kuanza kazi haraka. Kwa hali ya Bukoba, hiki kitu hakikufanyika matokeo yake wahanga wote walisaidiwa na ndugu na jamaa ambao wangeweza kuongeza majanga kwa kukosa elimu ya uokoaji wakati wa maafa.

Past Zero Hour. Lazima kuwepo na "Media Control Centre" ili kuhakikisha habari zinazotoka eneo la maafa ni sahihi na za kweli. Hii hutoa taarifa kwa wanahabari na Taifa,mara nyingi TV/Radio ya Umma huwa ndio mratibu kwa vyombo vingine kupata habari. Japo vyombo vingine havizuiwi kutoa habari ili mradi ziwe za hakika na kuthibitishwa na mamalaka husika kwa kuhojiwa.Bukoba haikutokea, wakati maafa yanaendelea, TBC wako na mambo yao. Matokeo yake Mbunge wa Jimbo akawa na wanahabari wake binafsi anaozunguka nao na TBC wanaigilizia habari toka kwa wengine.

Past Zero Hour SOPs inahitaji kuwepo na "Basic Sustainability Kit" ndani ya masaa 24 baada ya tukio, vitu kama Maji safi ya kunywa, sleeping bags, dry food, chandarua, madawa, kurunzi kwa nyumba ambazo umeme umekatika, nguo, mablanketi nk. Haya yote hayakutokea, ndio maana mpaka masaa 72 kuna watu wanalala nje,watu walilala giza kutokana na umeme kukatwa, yote ni jukumu la "KITENGO CHA MAAFA OFISI YA WAZIRI MKUU" , lakini mpaka sasa tunaenda masaa 96 na hakuna "Kikosi Kazi" kilichopiga kambi katika eneo la tukio. Na Bunge lilipitisha bajeti ya Kitengo hiki.

"Day One" na "Day Two and Nth" ilipaswa kuwa na medical teams, wataalamu wa umeme, mratibu wa misaada toka kwa wahisani na media Assessment ili kuepuka "tetesi" zinazoweza kuleta taharuki ktk eneo la madhara.

Bahati mbaya haya yote hayakufanyika, matokeo yake baada ya tetemeko la mchana, kesho yake kulitokea "mtetemo" mdogo ambao uliwatia watu hofu. Watu hawakuwa na taarifa na hivyo wengine kujua limerudi tena na katika kujiokoa wakaumia zaidi. Baadae ndio serikali inatoka na "wataalamu" wake kusema huwa kuna kitu kinaitwa "Earthquake aftershocks", hivyo ni jambo la kawaida. Sasa kwanini hiki kitengo cha maafa kwa kutumia wataalamu hao haikutoa taarifa mapema?

Siku ya nne baada ya maafa ndio inaundwa kamati ya kuratibu misaada,wakati hatua hii ilipaswa kuwa ndani ya masaa 24 au "Past Zero Hr". Yaani jambo lilitakiwa kufanywa jana, linafanywa mtondogoo. Jamani hivi ni lini kama Taifa tutarudi ktk mstari na kuwajibika kwa watu wetu? Mpaka leo bado "kamati imeundwa" kufanya uokozi na kutathimini. Hivi hicho kitengo cha maafa hakina ABC ya "Emergency Disaster Drill" ili kujua yanapotokea majanga kuna "Standard Operating Procedures (SOP)" zinapaswa kufuatwa?

Kitengo cha maafa kilitakiwa kujua majanga hayana hodi wala miadi. Wanachopaswa kujiandaa ni kutumia hiyo bajeti wanayopata kila mwaka kufanya "Emergency Drill" ili kujiweka sawa. Na hizi drills ziwe katika maeneo yanayokumbwa mara kwa mara na majanga kama mafuriko Kilombero Morogoro na Pandambili Dodoma, Maporomoko ya mawe na udongo Same, Tsunami kando mwa Bahari ya Hindi, matetemeko eneo la bonde la ufa, milipuko ya gesi kwa wakazi wa jirani na Songas Ubungo n.k.

Miaka kadhaa iliyopita Serikali iliamua kuanzisha Degree ya maafa Chuo Kikuu Dodoma ikifahamika kama "Bachelor of Arts in Disaster Management". Ni wakati sasa wa kutumia wataalamu kutengeneza sera ya kukabiliana na majanga, kuliko kuishi kwa mazoea.

Ukiangalia sehemu ya Hotuba ya Waziri Mkuu bungeni mwaka huu juu ya majanga alisema hivi:

"Serikali imeimarisha Mfumo wa Upatikanaji wa Taarifa za Tahadhari za majanga kwa haraka kwa kujenga vituo 16 vya upimaji wa hali ya hewa na kuweka vifaa vya kupima wingi na kasi ya maji katika vituo 10 vilivyopo katika mabonde ya mto Pangani na mto Ruvuma. Aidha, Serikali imetoa mafunzo kwa Kamati za Maafa katika wilaya 14 za mikoa mitano nchini. Katika mwaka 2016/2017, Serikali itaendelea kuimarisha uratibu na menejimenti ya maafa nchini kwa kuanzisha Wakala wa Usimamizi wa Maafa, kuzijengea uwezo Kamati za Maafa za Mikoa na Wilaya na kuendelea kuimarisha Mfumo wa Taarifa za Tahadhari ya Awali".

Ni matumaini yetu sasa,serikali itaamka na kuona maafa ni jambo la kujiandaa wakati wowote. Kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya PM kinachoongozwa na Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kitakuja na mikakati mipya juu ya maafa kuliko kuishi kwa "mazoea".

Hili la Bukoba limetuumbua.Tujifunze tusirudie makosa.
 
Wenye nchi yao wakija utatukanwa mpaka ukione cha moto.Pili hata yale matubai waliyopewa na Mbunge wao na Upinzani yamechukuliwa eti wasubiri msaada wa serikali.
Hili la kukomba mablanketi na maturibai...Siyo sahihi kabisaaa
 
Ndugu yangu Barafu kwa Tanzania hiyo emergency management plan ni issue, unaongelea SOP ambayo ni subset ya plan nzima; plan yenyewe km ipo haiwezi kuwa implemented due to one or more of the triple constraints.
 
Mkuu tatizo Lao hawakubali makosa ndio laana wakawapokonya maturubahi na mahema
 
Ndugu yangu barafu kwa Tanzania hiyo emergency management plan ni issue, unaongelea SOP ambayo ni subset ya plan nzima wakati plan yenyewe na km ipo haiwezi kuwa implemented due to one or more of the triple constraints.
Sasa mkuu Freema Agyeman hiki Kitengo cha Maafa kitakuwa na maana gani?Kama kinapata bajeti na matukio kama haya kinaweweseka kuyakabili?
 
Mtoa mada umenena ukweli. Jambo la kushangaza nchi hii ni kutowatumia ipasavyo wataalamu walionao na kubaki kuloloma tu. Kuna wataalamu wa counselling wengi tu waliohitimu chuo kikuu cha Tumaini Iringa ambao walitakiwa wawe wameajiriwa wilaya zote za nchi hii chini ya ofisi ya waziri mkuu lakini hadi leo wapo tu mitaani kwenye vijiNGOs visivyo na mbele wala nyuma.

Laiti wangewaajiri hawa wangesaidia sana kuwaondolea wahanga tatizo la kisaikolojia ambalo ndio kubwa linalowakabili wahanga hadi sasa.
Nimshauri mwajiri mkuu wa umma awaajiri wanasaikolojia hawa na kuwapa ofisi angalau kila wilaya kama ilivyo kwa nchi jirani ya Kenya.

Niliwahi kutembelea ofisi ya waziri mkuu wa Kenya miaka ya 2011 na nilikuta ana counsellors 22 ofisini kwake. Nimuulize waziri mkuu ofisi yake ina counsellers wangapi? Isijekuwa tunasubiri wataalamu hawa kutoka china au marekani?

Wataalamu wa majanga na unasihi tupo lakini hatutumiki kabisa.
Kwa taarifa yao tu ni kuwa waathirika wa aina yoyote wanahitaji la mingi moja tu nalo ni counseling. Hayo mengine ni subsidiary.
Iundwe idara ya unasihi haraka iwezekanavyo na iwe kila wilaya tuache siasa.
 
Mwaka huu tetemeko limetikisa, Kitengo cha maafa kinatakiwa kiitikie mara moja na kwa haraka, lakini tunaenda masaa 96 hakuna "Rapid Response" yoyote kutoka "Kitengo cha Maafa" toka Ofisi ya Waziri Mkuu. Hiki kitengo kilipitishiwa bajeti lakini mpaka sasa hakijapeleka si maturubai, mahema, chakula wala hata maji safi kwa wahanga. Sasa kweli kuna maaana ya hiki kitengo kupewa pesa na Bunge?

Kuna Standard Operating Procedures for Disaster Mgt (SOP),na hasa hizi "Natural Hazards" kama tetemeko na mafuriko. Kuanzia "zero hour","Past zero hour","Day One","Day Two" nakuendelea na siku zinazofuata kulingana na ukubwa wa tatizo. Hizi SOPs zinatakiwa kuwa implemented na Kitengo cha Maaafa toka ofisi ya Waziri Mkuu. Kila hatua ina namna yake ya uwokozi. Lakini mpaka leo siku ya tano bado serikali inafanya "procedures" za "Zero hour" wakati ilitakiwa kuwa kwenye "Day Two and Nth"

Ndani ya masaa 24 tulitakiwa tuwe tunapata taarifa ya mwenendo wa majanga toka kituo maalumu cha habari kilichopo Bukoba, kituo kinachoratibiwa na ofisi ya PM. Kuwe na team maalumu wa wataalamu wa afya, team ya Wanasaikolojia na washauri ili kuwafariji na kuwajenga wale waliopatwa na mshtuko ktk maeneo ya majanga.

Zero Hour huwa ni dakika 45 baada ya tukio,kamati za Maafa za Mkoa na Wilaya chini ya kamati ya Ulinzi na Usalama hukutanika. Hapa huwa ni hatua ya kwanza kuhakikisha wadau wa maafa wamekusanywa kwa ngazi ya Mkoa/Wilaya na kuanza kazi haraka. Wadau kwa nchi kama yetu ni JWTZ,JKT, Scouts, Red Cross, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Volunteers. Hawa wanatakiwa kupata muongozo na kuanza kazi haraka. Kwa hali ya Bukoba, hiki kitu hakikufanyika matokeo yake wahanga wote walisaidiwa na ndugu na jamaa ambao wangeweza kuongeza majanga kwa kukosa elimu ya uokoaji wakati wa maafa.

Past Zero Hour. Lazima kuwepo na "Media Control Centre" ili kuhakikisha habari zinazotoka eneo la maafa ni sahihi na za kweli. Hii hutoa taarifa kwa wanahabari na Taifa,mara nyingi TV/Radio ya Umma huwa ndio mratibu kwa vyombo vingine kupata habari. Japo vyombo vingine havizuiwi kutoa habari ili mradi ziwe za hakika na kuthibitishwa na mamalaka husika kwa kuhojiwa.Bukoba haikutokea, wakati maafa yanaendelea, TBC wako na mambo yao. Matokeo yake Mbunge wa Jimbo akawa na wanahabari wake binafsi anaozunguka nao na TBC wanaigilizia habari toka kwa wengine.

Past Zero Hour SOPs inahitaji kuwepo na "Basic Sustainability Kit" ndani ya masaa 24 baada ya tukio, vitu kama Maji safi ya kunywa, sleeping bags, dry food, chandarua, madawa, kurunzi kwa nyumba ambazo umeme umekatika, nguo, mablanketi nk. Haya yote hayakutokea, ndio maana mpaka masaa 72 kuna watu wanalala nje,watu walilala giza kutokana na umeme kukatwa, yote ni jukumu la "KITENGO CHA MAAFA OFISI YA WAZIRI MKUU" , lakini mpaka sasa tunaenda masaa 96 na hakuna "Kikosi Kazi" kilichopiga kambi katika eneo la tukio. Na Bunge lilipitisha bajeti ya Kitengo hiki.

"Day One" na "Day Two and Nth" ilipaswa kuwa na medical teams, wataalamu wa umeme, mratibu wa misaada toka kwa wahisani na media Assessment ili kuepuka "tetesi" zinazoweza kuleta taharuki ktk eneo la madhara.

Bahati mbaya haya yote hayakufanyika, matokeo yake baada ya tetemeko la mchana, kesho yake kulitokea "mtetemo" mdogo ambao uliwatia watu hofu. Watu hawakuwa na taarifa na hivyo wengine kujua limerudi tena na katika kujiokoa wakaumia zaidi. Baadae ndio serikali inatoka na "wataalamu" wake kusema huwa kuna kitu kinaitwa "Earthquake aftershocks", hivyo ni jambo la kawaida. Sasa kwanini hiki kitengo cha maafa kwa kutumia wataalamu hao haikutoa taarifa mapema?

Siku ya nne baada ya maafa ndio inaundwa kamati ya kuratibu misaada,wakati hatua hii ilipaswa kuwa ndani ya masaa 24 au "Past Zero Hr". Yaani jambo lilitakiwa kufanywa jana, linafanywa mtondogoo. Jamani hivi ni lini kama Taifa tutarudi ktk mstari na kuwajibika kwa watu wetu? Mpaka leo bado "kamati imeundwa" kufanya uokozi na kutathimini. Hivi hicho kitengo cha maafa hakina ABC ya "Emergency Disaster Drill" ili kujua yanapotokea majanga kuna "Standard Operating Procedures (SOP)" zinapaswa kufuatwa?

Kitengo cha maafa kilitakiwa kujua majanga hayana hodi wala miadi. Wanachopaswa kujiandaa ni kutumia hiyo bajeti wanayopata kila mwaka kufanya "Emergency Drill" ili kujiweka sawa. Na hizi drills ziwe katika maeneo yanayokumbwa mara kwa mara na majanga kama mafuriko Kilombero Morogoro na Pandambili Dodoma, Maporomoko ya mawe na udongo Same, Tsunami kando mwa Bahari ya Hindi, matetemeko eneo la bonde la ufa, milipuko ya gesi kwa wakazi wa jirani na Songas Ubungo n.k.

Miaka kadhaa iliyopita Serikali iliamua kuanzisha Degree ya maafa Chuo Kikuu Dodoma ikifahamika kama "Bachelor of Arts in Disaster Management". Ni wakati sasa wa kutumia wataalamu kutengeneza sera ya kukabiliana na majanga, kuliko kuishi kwa mazoea.

Ukiangalia sehemu ya Hotuba ya Waziri Mkuu bungeni mwaka huu juu ya majanga alisema hivi:

"Serikali imeimarisha Mfumo wa Upatikanaji wa Taarifa za Tahadhari za majanga kwa haraka kwa kujenga vituo 16 vya upimaji wa hali ya hewa na kuweka vifaa vya kupima wingi na kasi ya maji katika vituo 10 vilivyopo katika mabonde ya mto Pangani na mto Ruvuma. Aidha, Serikali imetoa mafunzo kwa Kamati za Maafa katika wilaya 14 za mikoa mitano nchini. Katika mwaka 2016/2017, Serikali itaendelea kuimarisha uratibu na menejimenti ya maafa nchini kwa kuanzisha Wakala wa Usimamizi wa Maafa, kuzijengea uwezo Kamati za Maafa za Mikoa na Wilaya na kuendelea kuimarisha Mfumo wa Taarifa za Tahadhari ya Awali".

Ni matumaini yetu sasa,serikali itaamka na kuona maafa ni jambo la kujiandaa wakati wowote. Kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya PM kinachoongozwa na Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kitakuja na mikakati mipya juu ya maafa kuliko kuishi kwa "mazoea".

Hili la Bukoba limetuumbua.Tujifunze tusirudie makosa.
badala yake kenyata ndo akaanza kutupa msaada wa mablanket kyakyakya............. burekabisa
 
Wenye nchi yao wakija utatukanwa mpaka ukione cha moto.Pili hata yale matubai waliyopewa na Mbunge wao na Upinzani yamechukuliwa eti wasubiri msaada wa serikali.
Nani kayachukua?

Kuna majimbo mengine ya ccm hata pole ya kutembelewa na wakuu hawajaipata.
 
hao watabiri wa hali ya hewa; ni heri hata wale wa kule sumbawanga;

Hawana jinsi wanategemea models ambazo ni mahesabu ya kibinadamu. Utabiri utabaki kuwa utabiri, unaweza kuwa ukweli, umakaribiana na ukweli au ukawa sio ukweli (nachelea kuuita uongo haha).
 
Wangeomba msaada wa ushauri kutoka Japan.

Ni kuingia ubalozini na kujieleza na kikaeleweka.

Japan wana uzoefu wa mambo haya, na kule mtoto mdogo wa miaka 5-7 anafahamu emergence exits na hatua za kuchukua endapo tetemeko litatokea mahali palepale alipo.

Mambo mengine ni madogo sana lakini ni mepesi kuyadharau.
 
Ndugu yangu Barafu kwa Tanzania hiyo emergency management plan ni issue, unaongelea SOP ambayo ni subset ya plan nzima; plan yenyewe km ipo haiwezi kuwa implemented due to one or more of the triple constraints.

mkuu barafu na Freema Agyeman mmezungumza kitu nyeti,. niwahakikisie tu kwamba kwa ufahamu wangu hizo Emergency management plan zipo, na SOPs zake zipo. TAtizo kuzitumia, watu kwa idadi fulani wamefundishwa lakini ikifika kwanye maafa utekelezaji wake unakuwa mgumu...mojawapo of course ni kukosekana kwa mazoezi ya utayari (simulation) ambapo kuyafanya yanahitaji fedha nyingi

mnazungumzia bajeti ya kitengo cha maafa lakini kwa kiasi kikubwa ni fedha za wafadhili, kawaulize kama OC wanayopata inatosha kutekeleza majukumu yao ipasavyo?

Kuhusu response, mkuu barafu kwa hali ya kijijini ni sahihi kwamba first responders ni ndugu na majirani katika zero hour, na unahitaji mfumo imara wa mawasiliano kuweza kutekeleza kikamilifu hizo SOP step kwa step. baahti mbaya kwa wilayani wengi wanadhani kamati ya maafa ndiyo kamati ya ulizi na usalama hivyo watu wa muhimu kama wanasihi wanakuwa wanakosekana au wataalamu wa maafa ambao wapo ila hawajaajiriwa bado!

ni hayo kwa sasa
 
Wenye nchi yao wakija utatukanwa mpaka ukione cha moto.Pili hata yale matubai waliyopewa na Mbunge wao na Upinzani yamechukuliwa eti wasubiri msaada wa serikali.
Hivi kwa nini kilamkitumtunaingiza siasa? Kwa kweli ni aibu kwa hicho kitengo cha maafa. Hadi harambee! We need to do better than that. Baada ya kushukuru waliotangulia kutoa musaada wanaikusanya. Makubwa hsya.
 
Kuna mambo mengine ni sisi wenyewe tunajiweka nyuma sana.

Hata hiyo idara ya geology sidhani kama wana tovuti ambayo ipo live na inafanya kazi 24/7, kurekodi seismic events.
 
Back
Top Bottom