Tusiwe na vyama vya siasa, tubuni namna yetu ya peke yake ya kupata viongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiwe na vyama vya siasa, tubuni namna yetu ya peke yake ya kupata viongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ayubuchacha12, Jun 7, 2012.

 1. ayubuchacha12

  ayubuchacha12 Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :clap2:
  Rais na viongozi wengine wa taifa hili wachaguliwe kwa kupitia mitihani, wapewe mitihani wafanye na atakayeonekana ana IQ kubwa kuliko woote Tanzania ndiye awe rais, wa pili awe makamu wa rais na kuendelea.

  Richa ya IQ pia uadilifu uwe kigezo, kama mtu alishawahi kuiba au kukosa uadilifu wa namna yeyote ile kwa taifa hili asipewe urais hata kama ana IQ kubwa kuliko woote.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Its a good idea, na tunaweza kuliboresha hili wazo kwa kuongeza vigezo vingine viingi. Mfano: tunaweza kuangalia mchango wake katika taifa tokea akiwa mdogo hadi, shule za msingi, secondary na vyuo vikuu alikosoma bila kusahau sifa zingine za kiongozi bora.
  Swali! Unadhani wanasiasa watakubali hilo wazo? Na uhakika siyo karne hii, watakuwa tayari kupiga kelele hadi uonekane muongo na mambo chungu nzima ilimradi wazo hili halipiti kwenye katiba mpya.
  Anyway: Its a challenge to our systems na kama kuna nchi ilishawahi kufanyika ikafanikiwa itakuwa rahisi kujenga hoja, lakini kama hakuna basi tegemea kuambiwa hiyo kitu haijawahi kufanyika wala haipo duniani. Sababu ni zile zile, uzito wa kufanya au kujaribu vitu kwa manufaa ya taifa.
   
 3. B

  Benaire JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tanzania kuna mawazo mengi....sijui kama katiba mpya itatosha.....kila anaemka asubuhi anakuwa na wazo lake.....most of them are idealistic!
   
 4. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Dah! Mtoa mada nashukuru sana! Yaani imegusa at the deepest part of my brain and not heart!
  Naamini mtu mweusi amejaliwa akili nyingi na nguvu pia katika kufanya UBUNIFU chanya wa chochote kile! Nilishasema mara nyingi na sitoacha kusema kwama "DEMOKRASIA SIO NJIA SAHIHI KWA MAENDELEO YA NCHI ZA KIAFRIKA" Tuna mataifa zaidi ya arobaini, lakini hakuna hata moja lililojikwamua kutoka katika hali ya unyonge, chanzo ni nini? Kwangu ni siasa chafu, siasa zisizo na tija kwa mazingira na nyakati zetu, siasa tulizopandikiziwa makusudi kuendeleza ukoloni, siasa ambazo zinajulikana si zaidi ya asilimia 10% ya watz. KWANINI TUZING'ANG'ANIE? TUMEROGWA NA NANI? Embu fikiria mfano huu... Wanasema yeyote mwenye kufikisha miaka 18 ana haki ya kupiga kura, ila tu awe na akili timamu. Tunawaona mabibi na mababu zetu kwenye vyumba vya kupigia kura, wanataka waoneshwe Nyerere ili wampigie kura, iyo ni mwaka 2010, mbadala yake eti tunafanya assumption ni ccm...PUMBAVU! Wazee hao ni wajinga wa demokrasia, wajinga wa mfumo, lakini wana akili timamu hivyo ni haki kwao kupiga kura. Je, sio watujaziao magalasa kama Jk na serikali yake nchini?
  Ili Demokrasia iwe applicable kwa taifa lolote lile, ni lazima walau Political Consciousness ya raia wake walau ianzie 80%. Nchi nyingi za kiafrika hazijafikisha hata 20% Tunategemea nini? PUMBAVU!
  Hao vijana, ambao ndio chachu ya maendeleo kokote pale nao zaidi ya 80% ni mbumbumbu wa demokrasia, ni ushabiki na misifa tu, kama ilivyokuwa kuvaa Kata K, wakaona ni usasa, ndio huku kushabikia vyam vya siasa ni usasa kwao, muulizi maana ya neno demokrasia "patupu", maana ya neno "sera" sifuri, ataje sera za chama chake atajaribu, muulize ujazo wa sera hizo yaani kwanini anazikubali tofauti na za chama kingine "atakwambia we fulani umuoni bungeni, unadhani atatoa sera mbovu", HANA UWEZO WA KUHOJI NA KUPIMA UFANISI WA SERA, anafuata mkumbo!
  Sisi ngozi nyeusi tuna akili zaidi ya wazungu, sasa TUKAE CHINI NA TUFANYE UBUNIFU WA MIFUMO MAHUSUSI KWA MAZINGIRA NA NYAKATI ZETU, IKIWEMO YA SIASA, ILI KUTUONGOZA,....TUNAWEZA ILA TU "NGUVU YETU NI UMOJA NA KUTHUBUTU"
  Hakuna tofauti ya viongozi wa chadema na ccm serikalini, wote ni zao la mfumo mbovu nao wenyewe ni wabovu vile vile!
  Habari njema ni hii...MUNGU wetu yu tayari kutushindia vitani, anaita sasa!
   
 5. B

  Benaire JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nani atapewa mamlaka ya kusimamia huo mtihani wa IQ.....Nani atatunga mtihani....Je usiri wake utakuwaje usileak....Unapozungumzia IQ unamaanisha nini? Watu wengi wenye IQ kubwa Afrika ni zao la mfumo huo wenye elements za demokrasia.
  Kwa pendekezo lako,turudishe utamaduni wetu wa asili,turudishe elimu yetu (informal),turudishe dini zetu za asili,turudishe tawala zetu za ntemiship....haya ndio yana match na mazingira yetu.....apart from that tunacheza ngoma ile ile kwa jina tofauti....tutakuwa tunawaza kidemokrasia ya magharibi kuongoza TANZANIA....IQ kubwa, haya bana.
   
 6. m

  mabhuimerafulu Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Kwa masharti hayo nchi haitapata Rais. Pili nani atasahihisha mtihani huo? Nadhani kama hatauawa kabla ya kutoa matokeo basi rushwa atakayopata ni balaa
   
 7. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Binafsi siungi mkono njia ya mtihani kupima IQ ya watu kupata viongozi, ila nachoamini ni "DEMOCRACY HAS PROVEN FAILURE IN AFRICA" IT SHOULD NO LONGER EXIST ANY MORE, FOR THE SAKE OF OUR MAZINGIRA & NYAKATI, that's over!
  Ni kweli sio kazi rahisi kubuni mbadala wake, lakini pia HATUSHINDWI-TUNAWEZA, ni lazima tuumize vichwa, si lele mama!
  Tumezoe kusema kuwa chochote chetu ni "idealistic" lakini huwa ni utumwa "mental slavery" unaotusumbua, kasumba ya uduni "inferiority complex".
  Ndio maana babu yako unayeamini aliishi katika hekima kubwa akifa atakuwa mzimu, ila babu kama huyo, wa kizungu akifa utamwita mtakatifu, ni "upunguani". Hata mzungu akituambia uwepo wetu ni "idealistic" na wao ni "realistic" tutaamini tu, kwa kuwa wao wamesema. Ni upunguani! TUZINDUKE WANAAFRIKA WENZANGU. Haimaanishi kurudisha kabisa ukale wetu, ila ni kurudisha uafrika wetu uendane na mazingira yetu!
  Mungu wetu anaita!
   
 8. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60

  ​Hapo pekundu, wewe una IQ ya ngapi (Kiasi gani)..?
   
 9. ayubuchacha12

  ayubuchacha12 Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :clap2:
  Mtihani utasimamiwa na baraza la mitihani chini ya uangalizi mkali,,,na sheria iwekwe kwamba kukitokea udanganyifu wowote adhabu kali kuliko zooote duniani itolewe. Kuna namna ya kupima IQ ya mtu na waalimu hufundishwa kupima IQ ya wanafunzi na watu wote kwa ujumla, kwa hiyo kama kuna mwalimu hapa atusaidie namna ya kupima IQ ya mtu.
  Kuhusu IQ yangu ni ya wastani ndo maana hata huo urais siufikirii kama tukianzisha mfumo huu wa kuchagua viongozi kwa kuangalia IQ. Unajua mojawapo ya kazi ya kiongozi ni kutoa maamuzi na yawe sahihi,,,na mtu mwenye IQ kubwa ni dhahiri atatoa maamuzi sahihi na kwa haraka.
  UNAJUA SUALA LA KUCHAGUA KIONGOZI KWA KUANGALIA ANAVYOONGEA NA KUCHANGIA KIFEDHA SIO ZURI KWA SABABU UONGOZI SIO FEDHA WALA MANENO...UONGOZI NI KUTOA MAAMUZI SAHIHI...HII YA KUCHAGUA WATU WANAOJUA KUONGEA KUMEWANYIMA HAKI YA KUWA RAIS MA-BUBU WENYE IQ KUBWA!!!
  Please hata mabubu nao wana haki ya kuwa ma-rais japo hawajui kuongea maneno bali wana akili ya kufanya maamuzi sahihi.
   
 10. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hilo la IQ limeniupset! Albert Einstain IQ yake ilikuwa inaaproach Zero unajua hilo? Though he was the genious wa ajabu
   
 11. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mtoa maada katoa la IQ kama mfano, ila siyo lazima iwe IQ pekee yake, tunaweza kuongeza vitu chungu nzima! Wapo watu ambao wana IQ pamoja na karama ya uongozi na bado pia ni wasafi. Point yangu ni kuwa, IQ ya mtu iwe ni moja vigezo lakini siyo ndiyo kigezo pekee!
   
 12. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Ni kweli, tunaweza kubuni vingine vingi tu kama...
  1. UTU, ambao unajenga moyo wa utayari wa kuwatumikia watu, uzalendo, ujasiri, upendo, morali, hekima, usawa, nk.
  2. UBUNIFU, namna alivyoweza kutafuta mbadala mpya katika kutatua matatizo mbalimbali katika jamii, pia awe na alternatives mbalimbali zenye tija kwa mazingira na nyakati zetu endapo atapewa madaraka.
  3. UKARIBU NA JAMII, awe mtu anayeshirikiana na jamii yake katika hali zote. Asiwe na kitu hata kimoja kinachomfanya asikaribiane na watu, mfano wizi, ubinafsi(kujilimbikizia-utajiri), ushirikina, ulevi, kupenda starehe, nk.
  4. TAMADUNI, awe mwenye kuamini na kuishi tamaduni zetu za kiafrika, zenye kuleta tija! Adhihirishe kuchukia umagharibi!
  5. UFAHAMU, awe anamtambua adui yetu mkuu wa unyonge wetu, na aoneshe kuchukua japo hatua chache katika kupambana naye(amechezaje nafasi yake tangu kumjua)
  *Haya yote tutapaswa kuyajengea misingi imara kwa kuyaingiza katika mifumo yetu ya elimu, mifumo yetu ya habari, sanaa zetu, nk. Hapo tutaweza kuandaa viongozi thabiti na raia thabiti vile, nchi itatulia watafanya kazi kwa kujituma wenyewe na maendele yatafikiwa!
  Hayo ni maoni yangu mimi, lakini ninaamini kabisa, tukikaa chini kama jopo, tunaweza kutoka na vigezo makini kabisa!
  Mungu wetu anaita!
   
 13. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Idea zako nazifananisha na za akina Plato na Aristotle'
   
 14. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  WE NEED NO MORE POLITICS, and we have to rise our voices all over the land, crying "NO MORE POLITICS"
  Mifumo huwa inatengenezwa na binadamu, na si vyema kuiamini, ila MANTIKI TU, hii imo katika nafsi ya mtu yeyote duniani. Binadamu hujiundia mifumo makusudi, aidha kulinda MANTIKI iliyomo nafsi mwa kila mtu, ama kupindisha MANTIKI hiyo, kwa sababu zake binafsi hasa "UMIMI/UBINAFSI"
  Demokrasia ni moja ya mifumo iliyobuniwa makusudi na watu wachache, kupindisha MANTIKI iliyomo nafsini mwetu, kwa maslahi ya watu wachache! Tukaaminishwa njia hii, tukaiamini na kupigania kuiishi, matokeo yake ndio haya, ufisadi, wizi, vita, unyonge, uduni, utumwa, unyonyaji, nk. Kamwe hatuwezi kujikwamua humo hadi pale tutakapoacha njia hiyo!
  Mfumo wowote ule katika maisha, ni lazima usadifu MAZINGIRA na NYAKATI za eneo husika! Kama sivyo...ni UPUNGUANI kutarajia maendeleo!
  "NO MORE POLITICS" (nimeipenda sana mada hii, cha ajabu "great thinkers" ....!!!??? Ni jina tu? Naamini kabisa mpo, jitokezeni kuweka mambo sawa panapostahili)
  Mungu wetu anaita sasa!
   
Loading...