Tusiwatazame mafisadi kidini wala kikabila hawa ni maadui wa taifa letu

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Waungwana,

Tunapowajadili wale wote ambao wanatengeneza njia za kuiba fedha za umma, tusiwatazame kwa misingi ya dini wala kabila.

Wale wote wanaowadhulumu masikini wa nchi hii kwa kutengeneza njia za wizi wa fedha nyingi, ni watu ambao hawafai kutetewa kwa kutumia itikadi za dini wala makabila yao.

Wote wenye kuhusika na mikataba mibovu, wote ambao wapo tayari kujenga majumba ya kifahari kwa kutumia fedha wasizostahili kuzitumia, ni watu wasiofaa kutetewa kwa sababu wanaswali kwenye msikiti fulani au kanisa fulani, hawa ni maadui wa ustawi wa nchi.

Mabilioni yanayotumika bila ya uwepo wa sababu zenye kuweza kuhalalisha matumizi makubwa, yangeweza kujenga zahanati nyingi tu, kujenga barabara za lami, kujenga visima vingi tu, yangeweza kusaidia katika kujenga mazingira yatakayowawezesha walemavu kupunguziwa adha za kimaisha.

Hawa wanaodumaza ukuaji wa kiuchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla, wasitazamwe kama vile wanachokifanya ni sifa kwa wanajamii. Wanaweza kuwa na msaada kwenye maisha ya wachache lakini hao ni wale wenye ukaribu na hawa wenye vyeo, huko vijijini kuna shida nyingi ambazo uwepo wake unaendelea kuchangiwa na huu ufisadi uliopo.

Hivyo rai yangu ni kwamba, yule anayechangia katika uwepo wa umasikini wa watu wengi atazamwe kama kikwazo cha maendeleo asitazamwe kwa zile huruma za kidini na kikabila.
 
Mda mwingine natamani tungetumia Sheria kama China.

Sasa hivi mafisadi kibao wangekuwa kuzimu
 
swala la din au ukabila linatokea pale double standard zinapotokea yaani unakuta mtu mtu wa dini flani akikosea watu wenye id flan wanamtetea lakin kosa hilo hilo likitendwa na mtu wa dini / kabila la upande flani wanamshambulia
mfano wakurugenzi wa haya mashirika PPF /NSSF haya mashirika yanaaongoza matumizi mabaya ya mifuko lakin kuna wakati wachangiaji wanaacha kuangalia uhalisia badala yake wanaangalia udini wao /ukabila wao
Mimi naunga mkono hoja tusiangalie udini /ukabila wa mtu kwenye kujadili uadilifu wa mtu MWIZI ni mwizi tu
 
Ni kweli kabisa mwizi ni mwizi tu, roho ya wizi ipo kila sehemu, na ni tabia ambayo inaanzia utotoni. Nakumbuka shuleni kulikuwa na wanafunzi wawili kazi yao kuiba vichongeo, wakati wa mapumziko wao wawili hawaendi kula mihogo, mmoja anasimama mlangoni kutazama nani anakuja na mwingine anapitia makompasi yote ya darasani, moja baada ya jingine. Watu hao wawili waliojifunza wizi tangu darasa la tatu, wanapokuja kupewa madaraka serikalini ni lazima wataiba.
 
Waungwana,

Tunapowajadili wale wote ambao wanatengeneza njia za kuiba fedha za umma, tusiwatazame kwa misingi ya dini wala kabila.

Wale wote wanaowadhulumu masikini wa nchi hii kwa kutengeneza njia za wizi wa fedha nyingi, ni watu ambao hawafai kutetewa kwa kutumia itikadi za dini wala makabila yao.

Wote wenye kuhusika na mikataba mibovu, wote ambao wapo tayari kujenga majumba ya kifahari kwa kutumia fedha wasizostahili kuzitumia, ni watu wasiofaa kutetewa kwa sababu wanaswali kwenye msikiti fulani au kanisa fulani, hawa ni maadui wa ustawi wa nchi.

Mabilioni yanayotumika bila ya uwepo wa sababu zenye kuweza kuhalalisha matumizi makubwa, yangeweza kujenga zahanati nyingi tu, kujenga barabara za lami, kujenga visima vingi tu, yangeweza kusaidia katika kujenga mazingira yatakayowawezesha walemavu kupunguziwa adha za kimaisha.

Hawa wanaodumaza ukuaji wa kiuchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla, wasitazamwe kama vile wanachokifanya ni sifa kwa wanajamii. Wanaweza kuwa na msaada kwenye maisha ya wachache lakini hao ni wale wenye ukaribu na hawa wenye vyeo, huko vijijini kuna shida nyingi ambazo uwepo wake unaendelea kuchangiwa na huu ufisadi uliopo.

Hivyo rai yangu ni kwamba, yule anayechangia katika uwepo wa umasikini wa watu wengi atazamwe kama kikwazo cha maendeleo asitazamwe kwa zile huruma za kidini na kikabila.
Hoja kuntu.
 
Back
Top Bottom