Tusiwape nafasi vibaraka na makuadi wa mabeberu

nchi iko salama kwa CCM, hivyo hatutegemei naibu katibu mkuu wa UVCCM / usalama wa CCM aseme tofauti.
after all hamna uzalendo wowote zaidi ya kuwa ma opportunist
 
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za baadhi ya watanzania wasio na uzalendo na nchi yao kuamua kuichafua Nchi yao kwa makusudi kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa mabeberu.

Uhaini wa kichuki unafanywa na baadhi ya watanzania wanaotumiwa na mataifa ya kigeni yanayozitolea udenda rasilimali zetu ambazo awali walikuwa wakizichota watakavyo bila kuzuiliwa huku wakitupamba na kila neno tamu lengo likiwa ni kutuzubaisha au kutuhadaa ili waendelee kupora mali zetu na kutunyonya.

Historia inatukumbusha kuwa tangu wakati wa ukoloni wapo waafrika waliokubali kutumika na wakoloni ili waafrika waendelee kutawaliwa au kuhujumu jitihada za ukombozi dhidi ya ukoloni. Vile vile wakoloni walitumia mbinu ya kuwagawa waafrika ili kupunguza nguvu harakati zao za kujipatia uhuru.

Hii inatufundisha kuwa hata leo tunapokabiliana na ukoloni maomboleo ili kujipatia uhuru wa kiuchumi kwa maendeleo yetu ukibaraka utajitokeza na mbinu za kutugawa zitaibuka lakini yatupasa kusimama imara zaidi ili kushinda hila hizi.

Hivi karibuni kumeibuka watanzania wenzetu wanaojiita wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu au watetezi uhuru wa habari kuisema serikali yetu nje ya nchi kuwa imeshindwa kuwajibika katika nyanja kuu mbili:-

1. Imeshindwa kusimamia usalama wa raia wake.

2. Inaminya uhuru wa habari

Naomba nieleze kwa hoja haya madai yao.

1. Serikali ya Tanzania imeshindwa kusimamia usalama wa raia wake, hii si kweli na ni hoja mfu.

Nchi yetu iko salama na ina utulivu wa kutosha, hivyo inatosha kusema Tanzania ina AMANI. Kielelezo chake ni nini?

Wananchi wa Tanzania wapo huru kufanya majukumu yao ya kila siku bila hofu yoyote.

Mfano: Hapa Dar es Salaam, saa kumi alfajiri unakutana na kina mama wachakarikaji wapo na chupa za chai au uji na vitumbua au chapati wakiwahisha huduma kwa wateja wao kwenye masoko au stendi za mabasi kuuza, wanamaliza na wanarejea majumbani bila hofu yoyote na ndio maisha yao ya kila siku kwanini kwa sababu usalama upo na amani imetawala.

Acha hiyo, alfajiri na mapema nakutana na vijana waendesha guta hapa Dar es Salaam masoko ya mahakama ya ndizi au Manzese au Buguruni wanapakia mizigo kuwapelekea wateja wao bila hofu yoyote, siku hizi matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yamekuwa adimu sababu usalama ni mkubwa na amani imetawala. Tuvipongeze vyombo vyetu vya dola sababu vipo imara.

Wikiendi nenda Beach za Kawe au Jangwani au Coco au Kigamboni utakuta idadi kubwa ya wanawake na watoto tena wengi wao hawajaenda na walezi au wazazi wao wapo wanaogelea kwa furaha na uhuru bila hofu yoyote kwanini kwa sababu usalama ni wa kutosha na amani imetawala.

Waumini wa dini mbalimbali wapo huru kwenda kwenye nyumba zao za ibada muda wowote na kufanya ibada zao bila hofu yoyote kwa sababu tu usalama ni mkubwa na amani imetawala.

Sasa, wanapotokea watu kuyatumia matukio machache ya uhalifu ambayo hata hivyo vyombo vyetu vya dola vimesimama imara kuvikomesha ni dalili kuwa si watu wema kwa nchi yetu kwani ipo idadi kubwa sana ya matukio ya kikatili yanatokea katika nchi hizo wanakokwenda kusimulia kuliko hapa kwetu Mfano:Mbunge wa upinzani nchini Uingereza wa chama cha Labour Mhe Hellen Joanne Cox alipigwa risasi na kufa akiwa eneo la bunge mnamo Juni 2016, mwaka 2018 zaidi ya wanafunzi 113 waliuwawa kwa kupigwa risasi wakiwa shuleni nchini Marekani, Hivi karibuni tu rapa Nipsey Hussle alipigwa risasi na kufa nchini Marekani.

Lakini vyombo vyao vya habari hawatangazi kuwa nchi zao raia hawako salama sisi vinatangaza na kuwatumia vibaraka wao kuiaminisha dunia kuwa hatuko salama kwa lengo la kutuchafua na kutaka tuwaruhusu waendelee kutunyonya kama ilivyokuwa awali tusiwape nafasi.

Ifahamike idadi kubwa ya wawekezaji au watalii tunayoipata kichocheo kimojawapo ni hali nzuri ya usalama, amani na utulivu tulionayo ambayo kwa nchi nyingi ni changamoto.

Tunajua yapo mataifa yenye agenda zao kwa baadhi ya mataifa ya Afrika yenye utajiri mkubwa wa rasilimali kama Tanzania ambayo yamebaini namna rahisi ya kuzivuna rasilimali hizo ni kuwapiganisha au kuyavuruga mataifa hayo kwa chokochoko za kisiasa kwa kuwatumia baadhi ya raia wake, viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali au dini wasio wazalendo kwa kuwalipa ili kueneza chuki, hofu au uzandiki kufanikisha mipango yao.

Hapa Tanzania zaidi ya asilimia 92 ya watu wakilala usiku kinachowaamsha ni mkojo tu au haja kubwa hivyo huwalazimu kwenda kujisaidia, bila ya hivyo wanaweza kuuchapa usingizi mpaka jua linachomoza, ajabu watu hawa tena nao unawakuta wakipayuka Tanzania hakuna usalama ndio maana nasema tusiwashangae wapo kazini na wanatafuta kupata Tonge. Tanzania ni salama sana, tuzidi kuwa wamoja na tuvipe ushirikiano vyombo vyetu vya dola.

Rai yetu kwa watanzania wote ni kuwa lazima dunia ijue kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli tumeamua kuijenga nchi yetu upya hivyo waporaji, wezi, watoroshaji na wanyonyaji wa rasilimali zetu hawapo salama na hawatakuwa, Mafisadi, wakwepa kodi, wauza dawa za kulevya, watakatishaji fedha, wala rushwa na wahujumu uchumi hawapo salama na hawatakuwa huru tena.

Uhuru na usalama wao ni kujisalimisha kwa kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kujenga uchumi usio tegemezi.

2. Serikali ya Tanzania inaminya uhuru wa habari. hoja hii ni kichekesho. Uandishi wa habari duniani kote unaongozwa na miiko na weledi ambapo wakati wote maslahi ya taifa lazima yazingatiwe kinyume na hapo ni kuruhusu matumizi ya kalamu kubomoa nchi au jamii jambo ambalo hatuwezi kulipa nafasi aslani.

Anayeandika na kusema hakuna uhuru wa habari, huyu amepata nafasi ya kuandaa habari yake hadi kuitoa bila bugudha yoyote au gazeti lake kusambaa na kuzika bila bugudha yoyote, ameitisha press conference na kufanya mahojiano na watu wa media akiwa ndani ya Tanzania bila kubugudhiwa wala kuzuiliwa wala kutishwa, yote haya hutokea Tanzania, Kama nchi isingekuwa na uhuru wa habari au Amani na usalama haya wasingefanya.

Ifike pahala watu hawa tuwaogope kama ukoma kwani tukiwaendekeza watatupeleka kubaya. Ikumbukwe wengi wao wametumia keki ya taifa hili kupata elimu nzuri na kuwa walivyo leo ila wamesahau kuwa wanadeni kubwa kwa nchi yao na wanapaswa kuitumikia na kuipenda kwa uaminifu badala ya kukengeuka na kuidhihaki. Ni WASALITI.

Muandishi wa makala hii ni Ndugu Galila Wabanh'u Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
View attachment 1075583
Maelezo yako ndio uhalisia big up ,like hupati,unatakiwa uwe na kifua kipana ,matusi yanakuja ,vibaraka hawakuachi salama
 
Sautiyamnyonge..huyu bwana alikamatwa na ameshahukumiwa. Usiwafananishe Mabeberu na sisi kabisaa. Ila kama ukatili haulalalishwi na ukatili wa jirani. Tuulinde nchibyetu dhidi ya ukatili. Soma hapo
Murder of Jo Cox

On 16 June 2016, Jo Cox, the British Labour Party Member of Parliament for Batley and Spen, died after being shot and stabbed multiple times in Birstall, West Yorkshire. In September, a 52-year-old local man named Thomas Alexander Mair was found guilty of her murder and other offences connected to the killing, and was sentenced to life imprisonment with a whole life order.
Hata hapa kwetu wamekamatwa na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani. Nilitaka kukuonesha uhalifu wa aina hiyo unatokea hata huko mnakoenda kuwapigia stori kuwa Tanzania hakuna usalama
 
Kwa waliompiga risasi Tundu Lisu hakuna aliyekamatwa hata mmoja kwa taarifa za Polisi. Tafadhali Kama hufahamu kitu usiingize Serikali yetu na CCM yetu kwenye kashfa ya mitandao. Hadi Lisu na Dereva warudi ndio upelelezi uanze. Please keep quite unatutesa watetezi wa JPM.
 
Maelezo yako ndio uhalisia big up ,like hupati,unatakiwa uwe na kifua kipana ,matusi yanakuja ,vibaraka hawakuachi salama
Mwambie atutajie majina ya wahaini wa kiuchumi akieleza aina ya uhaini na kiwango cha hasara tulicho kipata kutokana na huo uhaini. Sote tunaipenda nchi yetu tusemezane kwa uzalendo tujenge taifa letu
 
Una husda tu una hoja... Hao wanaodai Tanzania hakuna usalama na wakimaliza kueleza wanarudi tena kuishi na kula bata katika nchi ambayo haina usalama kwa raia wake wanasema hivyo kwa faida ya nani au ili iweje au wapate nini?
nchi iko salama kwa CCM, hivyo hatutegemei naibu katibu mkuu wa UVCCM / usalama wa CCM aseme tofauti.
after all hamna uzalendo wowote zaidi ya kuwa ma opportunist
 
Mwambie atutajie majina ya wahaini wa kiuchumi akieleza aina ya uhaini na kiwango cha hasara tulicho kipata kutokana na huo uhaini. Sote tunaipenda nchi yetu tusemezane kwa uzalendo tujenge taifa letu
Kakataa kukujibu?
 
Unaipenda nchi yako unashabikia haiko salama wakati ulipo unachat na kinywaji baridi pembeni yako huna hofu ndio uzalendo huo. Tujifunze kuisema nchi yetu vizuri hata kama tupo wapi!
 
Una husda tu una hoja... Hao wanaodai Tanzania hakuna usalama na wakimaliza kueleza wanarudi tena kuishi na kula bata katika nchi ambayo haina usalama kwa raia wake wanasema hivyo kwa faida ya nani au ili iweje au wapate nini?
scale ya usama wa nchi sio 'bibary state', kwamba ni either upo au haupo bali ni 'continuos range' kwa maana kwamba kiwango cha usalama kimepungua ukilinganisha na awamu ya 4, swala la watu kuishi hata Yemen kuna watu wanaishi lakini haimaanishi kuwa ni sehemu salama!
 
Upelelezi unaendelea haimaanishi hakuna waliokamatwa utakapokamilika ndipo taarifa kamili mtaipata
Kwa waliompiga risasi Tundu Lisu hakuna aliyekamatwa hata mmoja kwa taarifa za Polisi. Tafadhali Kama hufahamu kitu usiingize Serikali yetu na CCM yetu kwenye kashfa ya mitandao. Hadi Lisu na Dereva warudi ndio upelelezi uanze. Please keep quite unatutesa watetezi wa JPM.
 
Upelelezi unaendelea haimaanishi hakuna waliokamatwa utakapokamilika ndipo taarifa kamili mtaipata
Kaka sijui hufahamu ninachoongea. Jinai haishii kabisaa..ila haimaanishi wahusika au washukiwa wameshakamatwa hata mmoja. Taarifa za Polisi zinasema hakuna aliyekamatwa Wala kushilikiliwa na Polisi kuhusiana na kupigwa risasi Lissu. Naomba tufunge mjadala. Huna unalojua bhana mdogo. Tusiwanufaishe wapinzani wetu. Ila kama unaamua kubisha basi endelea tuu ila vijana wetu hatujawafundisha hivyo.
 
Kipi kinakufanya useme usalama umepungua?
scale ya usama wa nchi sio 'bibary state', kwamba ni either upo au haupo bali ni 'continuos range' kwa maana kwamba kiwango cha usalama kimepungua ukilinganisha na awamu ya 4, swala la watu kuishi hata Yemen kuna watu wanaishi lakini haimaanishi kuwa ni sehemu salama!
 
Una nyodo
Kaka sijui hufahamu ninachoongea. Jinai haishii kabisaa..ila haimaanishi wahusika au washukiwa wameshakamatwa hata mmoja. Taarifa za Polisi zinasema hakuna aliyekamatwa Wala kushilikiliwa na Polisi kuhusiana na kupigwa risasi Lissu. Naomba tufunge mjadala. Huna unalojua bhana mdogo. Tusiwanufaishe wapinzani wetu. Ila kama unaamua kubisha basi endelea tuu ila vijana wetu hatujawafundisha hivyo.
 
Muandishi wa huu uzi anamaanisha kwamba
1.Hata Marekani na Uingereza wapo watu wasiojulikana wanaoua na kupoteza watu bila kujulikana
2.Vyombo vya habari nchini vina uhuru kama walio nao CNN,NBS,Sky News n.k huko Marekani na Uingereza
 
Awamu hii vita dhidi ufisadi na ubadhirifu ni ya kudumu na sote ni mashahidi. Wewe mnazi wa kisiasa ndio unajipa upofu na uziwi ili usione au kusikia mazuri yanayofanywa
Naona umeishia kuniita mnazi wa kisiasa. Sasa wewe na mimi nani kaonyesha unazi? Hati sio wazalendo/wasaliti wanalipwa na mabeberu-mkiambiwa mtoe mifano mnakosa majibu. Kufanya mazuri hakukupi tiketi ya kuita wengine wasaliti au wakosa uzalendo. Wewe sifia tu kwa mapambo kile ukipendacho sina tatizo kama ni kweli shida yenu ni kuita watanzania wenzenu wasaliti kisa wana maono tofauti.
 
Kwa Africa mabeberu ni watu weusi. Fikiria serikali ya Mobutu. Nguema, Albashir, Mengistu, Taylor, Mugabe nk. Hawa walisingizia Mabeberu wa nje wakapata uhalali wa kufanya walioyafanya. Unless unafaidika na status Quo
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za baadhi ya watanzania wasio na uzalendo na nchi yao kuamua kuichafua Nchi yao kwa makusudi kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa mabeberu.

Uhaini wa kichuki unafanywa na baadhi ya watanzania wanaotumiwa na mataifa ya kigeni yanayozitolea udenda rasilimali zetu ambazo awali walikuwa wakizichota watakavyo bila kuzuiliwa huku wakitupamba na kila neno tamu lengo likiwa ni kutuzubaisha au kutuhadaa ili waendelee kupora mali zetu na kutunyonya.

Historia inatukumbusha kuwa tangu wakati wa ukoloni wapo waafrika waliokubali kutumika na wakoloni ili waafrika waendelee kutawaliwa au kuhujumu jitihada za ukombozi dhidi ya ukoloni. Vile vile wakoloni walitumia mbinu ya kuwagawa waafrika ili kupunguza nguvu harakati zao za kujipatia uhuru.

Hii inatufundisha kuwa hata leo tunapokabiliana na ukoloni maomboleo ili kujipatia uhuru wa kiuchumi kwa maendeleo yetu ukibaraka utajitokeza na mbinu za kutugawa zitaibuka lakini yatupasa kusimama imara zaidi ili kushinda hila hizi.

Hivi karibuni kumeibuka watanzania wenzetu wanaojiita wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu au watetezi uhuru wa habari kuisema serikali yetu nje ya nchi kuwa imeshindwa kuwajibika katika nyanja kuu mbili:-

1. Imeshindwa kusimamia usalama wa raia wake.

2. Inaminya uhuru wa habari

Naomba nieleze kwa hoja haya madai yao.

1. Serikali ya Tanzania imeshindwa kusimamia usalama wa raia wake, hii si kweli na ni hoja mfu.

Nchi yetu iko salama na ina utulivu wa kutosha, hivyo inatosha kusema Tanzania ina AMANI. Kielelezo chake ni nini?

Wananchi wa Tanzania wapo huru kufanya majukumu yao ya kila siku bila hofu yoyote.

Mfano: Hapa Dar es Salaam, saa kumi alfajiri unakutana na kina mama wachakarikaji wapo na chupa za chai au uji na vitumbua au chapati wakiwahisha huduma kwa wateja wao kwenye masoko au stendi za mabasi kuuza, wanamaliza na wanarejea majumbani bila hofu yoyote na ndio maisha yao ya kila siku kwanini kwa sababu usalama upo na amani imetawala.

Acha hiyo, alfajiri na mapema nakutana na vijana waendesha guta hapa Dar es Salaam masoko ya mahakama ya ndizi au Manzese au Buguruni wanapakia mizigo kuwapelekea wateja wao bila hofu yoyote, siku hizi matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yamekuwa adimu sababu usalama ni mkubwa na amani imetawala. Tuvipongeze vyombo vyetu vya dola sababu vipo imara.

Wikiendi nenda Beach za Kawe au Jangwani au Coco au Kigamboni utakuta idadi kubwa ya wanawake na watoto tena wengi wao hawajaenda na walezi au wazazi wao wapo wanaogelea kwa furaha na uhuru bila hofu yoyote kwanini kwa sababu usalama ni wa kutosha na amani imetawala.

Waumini wa dini mbalimbali wapo huru kwenda kwenye nyumba zao za ibada muda wowote na kufanya ibada zao bila hofu yoyote kwa sababu tu usalama ni mkubwa na amani imetawala.

Sasa, wanapotokea watu kuyatumia matukio machache ya uhalifu ambayo hata hivyo vyombo vyetu vya dola vimesimama imara kuvikomesha ni dalili kuwa si watu wema kwa nchi yetu kwani ipo idadi kubwa sana ya matukio ya kikatili yanatokea katika nchi hizo wanakokwenda kusimulia kuliko hapa kwetu Mfano:Mbunge wa upinzani nchini Uingereza wa chama cha Labour Mhe Hellen Joanne Cox alipigwa risasi na kufa akiwa eneo la bunge mnamo Juni 2016, mwaka 2018 zaidi ya wanafunzi 113 waliuwawa kwa kupigwa risasi wakiwa shuleni nchini Marekani, Hivi karibuni tu rapa Nipsey Hussle alipigwa risasi na kufa nchini Marekani.

Lakini vyombo vyao vya habari hawatangazi kuwa nchi zao raia hawako salama sisi vinatangaza na kuwatumia vibaraka wao kuiaminisha dunia kuwa hatuko salama kwa lengo la kutuchafua na kutaka tuwaruhusu waendelee kutunyonya kama ilivyokuwa awali tusiwape nafasi.

Ifahamike idadi kubwa ya wawekezaji au watalii tunayoipata kichocheo kimojawapo ni hali nzuri ya usalama, amani na utulivu tulionayo ambayo kwa nchi nyingi ni changamoto.

Tunajua yapo mataifa yenye agenda zao kwa baadhi ya mataifa ya Afrika yenye utajiri mkubwa wa rasilimali kama Tanzania ambayo yamebaini namna rahisi ya kuzivuna rasilimali hizo ni kuwapiganisha au kuyavuruga mataifa hayo kwa chokochoko za kisiasa kwa kuwatumia baadhi ya raia wake, viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali au dini wasio wazalendo kwa kuwalipa ili kueneza chuki, hofu au uzandiki kufanikisha mipango yao.

Hapa Tanzania zaidi ya asilimia 92 ya watu wakilala usiku kinachowaamsha ni mkojo tu au haja kubwa hivyo huwalazimu kwenda kujisaidia, bila ya hivyo wanaweza kuuchapa usingizi mpaka jua linachomoza, ajabu watu hawa tena nao unawakuta wakipayuka Tanzania hakuna usalama ndio maana nasema tusiwashangae wapo kazini na wanatafuta kupata Tonge. Tanzania ni salama sana, tuzidi kuwa wamoja na tuvipe ushirikiano vyombo vyetu vya dola.

Rai yetu kwa watanzania wote ni kuwa lazima dunia ijue kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli tumeamua kuijenga nchi yetu upya hivyo waporaji, wezi, watoroshaji na wanyonyaji wa rasilimali zetu hawapo salama na hawatakuwa, Mafisadi, wakwepa kodi, wauza dawa za kulevya, watakatishaji fedha, wala rushwa na wahujumu uchumi hawapo salama na hawatakuwa huru tena.

Uhuru na usalama wao ni kujisalimisha kwa kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kujenga uchumi usio tegemezi.

2. Serikali ya Tanzania inaminya uhuru wa habari. hoja hii ni kichekesho. Uandishi wa habari duniani kote unaongozwa na miiko na weledi ambapo wakati wote maslahi ya taifa lazima yazingatiwe kinyume na hapo ni kuruhusu matumizi ya kalamu kubomoa nchi au jamii jambo ambalo hatuwezi kulipa nafasi aslani.

Anayeandika na kusema hakuna uhuru wa habari, huyu amepata nafasi ya kuandaa habari yake hadi kuitoa bila bugudha yoyote au gazeti lake kusambaa na kuzika bila bugudha yoyote, ameitisha press conference na kufanya mahojiano na watu wa media akiwa ndani ya Tanzania bila kubugudhiwa wala kuzuiliwa wala kutishwa, yote haya hutokea Tanzania, Kama nchi isingekuwa na uhuru wa habari au Amani na usalama haya wasingefanya.

Ifike pahala watu hawa tuwaogope kama ukoma kwani tukiwaendekeza watatupeleka kubaya. Ikumbukwe wengi wao wametumia keki ya taifa hili kupata elimu nzuri na kuwa walivyo leo ila wamesahau kuwa wanadeni kubwa kwa nchi yao na wanapaswa kuitumikia na kuipenda kwa uaminifu badala ya kukengeuka na kuidhihaki. Ni WASALITI.

Muandishi wa makala hii ni Ndugu Galila Wabanh'u Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
View attachment 1075583
 
Hata hapa kwetu wamekamatwa na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani. Nilitaka kukuonesha uhalifu wa aina hiyo unatokea hata huko mnakoenda kuwapigia stori kuwa Tanzania hakuna usalama

..waliompiga risasi TL wamekamatwa?

..kwanini hawapelekwi mahakamani?

..kuna watuhumiwa wengi wanapelekwa mahakamani lakini uchunguzi wa tuhuma zao haujakamilika 100%.

..kama madai yako kuwa waliompiga risasi Mh.Lissu wamekamatwa ni ya kweli, basi magaidi hao walipaswa kufikishwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom