Tusiwape nafasi vibaraka na makuadi wa mabeberu

Masters dissertation ya international cooperation.
Screenshot_2019-04-19-22-14-41-986_com.android.chrome.jpeg
 
Labda kama utakuwa hujui maana ya ufisadi ndio utaandika haya matapishi awamu unayodai inapambana na ufisadi ndio hii inayovunja sheria ya manunuzi ya umma,haitangazi tenda/zabuni,inatumia pesa zisizopitishwa na bunge na haipendi jyjmmkukaguliwa? Naona una akili timam japo bado humjui adui yako
 
Maswali mazuri ila kwa mada isiyohusika. Kuhusu Lissu na Ben Saanane ni uhalifu ambao vyombo vya dola vinayashughulikia kwa ustadi mkubwa. Kama una taarifa zinazoweza kurahisisha majukumu yao tafadhali toa ushirikiano. Ila pia nimejaribu kukupa taarifa kuwa Juni, 2016 Mbunge wa upinzani wa chama cha labour nchini Uingereza naye alipigwa risasi na kufa akiwa eneo la bunge mpaka leo M16 na Scotland yard bado wanapambana kuwabaini
Hebu acha upuuzi !! Angalau baada ya kelele huyu mtu amepunguza upotezaji, mauaji ya watu wa itikadi tofauti, jeuri na majivuno.
Tz hawakuwahi kuwa na mambo haya ya visasi. Tulikuwa na upinzani wa vyama vingi bila uadui. Lakini this is different.

Maendeleo yanayokuja na maumivu haya si endelevu bali fahari ya muda mfupi.
 
Unaipenda nchi yako unashabikia haiko salama wakati ulipo unachat na kinywaji baridi pembeni yako huna hofu ndio uzalendo huo. Tujifunze kuisema nchi yetu vizuri hata kama tupo wapi!
Hakuna mTz asiyeipenda nchi hii bali uongozi uliopo. Na kuuchukia uongozi kwa madhaifu yake si dhambi.
 
Wapinzani wengi sana wameuliwa na kupotezwa uchunguzi ukoje ?! Alianzwa Mawazo tena green guard, wakaja vijana wa Trm, wa kilosa, diwani kule kilombero, Hananasifu, Saa 8, nk . Uchunguzi wao uko Je ?!.
Upelelezi unaendelea haimaanishi hakuna waliokamatwa utakapokamilika ndipo taarifa kamili mtaipata
 
Mnaacha kujibu hoja za CAG mnaanza kusingizia mabeberu mnajifanya mmesahau kuwa ccm ndo mlopwaleta hao mabeberu na kuwapa rasilimali wavune watakavyo bro nyie mmechoka kuongoza taifa hili kwakuwa mmegoma kuondoka kwa box la Kula time will tell ccm haijawah kumtetea mtanzania bali utetea maslah ya wakubwa ndo maana kila kukicha sera zenu zinabadilika na kuzidi kuwatia umasikin watu
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za baadhi ya watanzania wasio na uzalendo na nchi yao kuamua kuichafua Nchi yao kwa makusudi kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa mabeberu.

Uhaini wa kichuki unafanywa na baadhi ya watanzania wanaotumiwa na mataifa ya kigeni yanayozitolea udenda rasilimali zetu ambazo awali walikuwa wakizichota watakavyo bila kuzuiliwa huku wakitupamba na kila neno tamu lengo likiwa ni kutuzubaisha au kutuhadaa ili waendelee kupora mali zetu na kutunyonya.

Historia inatukumbusha kuwa tangu wakati wa ukoloni wapo waafrika waliokubali kutumika na wakoloni ili waafrika waendelee kutawaliwa au kuhujumu jitihada za ukombozi dhidi ya ukoloni. Vile vile wakoloni walitumia mbinu ya kuwagawa waafrika ili kupunguza nguvu harakati zao za kujipatia uhuru.

Hii inatufundisha kuwa hata leo tunapokabiliana na ukoloni maomboleo ili kujipatia uhuru wa kiuchumi kwa maendeleo yetu ukibaraka utajitokeza na mbinu za kutugawa zitaibuka lakini yatupasa kusimama imara zaidi ili kushinda hila hizi.

Hivi karibuni kumeibuka watanzania wenzetu wanaojiita wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu au watetezi uhuru wa habari kuisema serikali yetu nje ya nchi kuwa imeshindwa kuwajibika katika nyanja kuu mbili:-

1. Imeshindwa kusimamia usalama wa raia wake.

2. Inaminya uhuru wa habari

Naomba nieleze kwa hoja haya madai yao.

1. Serikali ya Tanzania imeshindwa kusimamia usalama wa raia wake, hii si kweli na ni hoja mfu.

Nchi yetu iko salama na ina utulivu wa kutosha, hivyo inatosha kusema Tanzania ina AMANI. Kielelezo chake ni nini?

Wananchi wa Tanzania wapo huru kufanya majukumu yao ya kila siku bila hofu yoyote.

Mfano: Hapa Dar es Salaam, saa kumi alfajiri unakutana na kina mama wachakarikaji wapo na chupa za chai au uji na vitumbua au chapati wakiwahisha huduma kwa wateja wao kwenye masoko au stendi za mabasi kuuza, wanamaliza na wanarejea majumbani bila hofu yoyote na ndio maisha yao ya kila siku kwanini kwa sababu usalama upo na amani imetawala.

Acha hiyo, alfajiri na mapema nakutana na vijana waendesha guta hapa Dar es Salaam masoko ya mahakama ya ndizi au Manzese au Buguruni wanapakia mizigo kuwapelekea wateja wao bila hofu yoyote, siku hizi matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yamekuwa adimu sababu usalama ni mkubwa na amani imetawala. Tuvipongeze vyombo vyetu vya dola sababu vipo imara.

Wikiendi nenda Beach za Kawe au Jangwani au Coco au Kigamboni utakuta idadi kubwa ya wanawake na watoto tena wengi wao hawajaenda na walezi au wazazi wao wapo wanaogelea kwa furaha na uhuru bila hofu yoyote kwanini kwa sababu usalama ni wa kutosha na amani imetawala.

Waumini wa dini mbalimbali wapo huru kwenda kwenye nyumba zao za ibada muda wowote na kufanya ibada zao bila hofu yoyote kwa sababu tu usalama ni mkubwa na amani imetawala.

Sasa, wanapotokea watu kuyatumia matukio machache ya uhalifu ambayo hata hivyo vyombo vyetu vya dola vimesimama imara kuvikomesha ni dalili kuwa si watu wema kwa nchi yetu kwani ipo idadi kubwa sana ya matukio ya kikatili yanatokea katika nchi hizo wanakokwenda kusimulia kuliko hapa kwetu Mfano:Mbunge wa upinzani nchini Uingereza wa chama cha Labour Mhe Hellen Joanne Cox alipigwa risasi na kufa akiwa eneo la bunge mnamo Juni 2016, mwaka 2018 zaidi ya wanafunzi 113 waliuwawa kwa kupigwa risasi wakiwa shuleni nchini Marekani, Hivi karibuni tu rapa Nipsey Hussle alipigwa risasi na kufa nchini Marekani.

Lakini vyombo vyao vya habari hawatangazi kuwa nchi zao raia hawako salama sisi vinatangaza na kuwatumia vibaraka wao kuiaminisha dunia kuwa hatuko salama kwa lengo la kutuchafua na kutaka tuwaruhusu waendelee kutunyonya kama ilivyokuwa awali tusiwape nafasi.

Ifahamike idadi kubwa ya wawekezaji au watalii tunayoipata kichocheo kimojawapo ni hali nzuri ya usalama, amani na utulivu tulionayo ambayo kwa nchi nyingi ni changamoto.

Tunajua yapo mataifa yenye agenda zao kwa baadhi ya mataifa ya Afrika yenye utajiri mkubwa wa rasilimali kama Tanzania ambayo yamebaini namna rahisi ya kuzivuna rasilimali hizo ni kuwapiganisha au kuyavuruga mataifa hayo kwa chokochoko za kisiasa kwa kuwatumia baadhi ya raia wake, viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali au dini wasio wazalendo kwa kuwalipa ili kueneza chuki, hofu au uzandiki kufanikisha mipango yao.

Hapa Tanzania zaidi ya asilimia 92 ya watu wakilala usiku kinachowaamsha ni mkojo tu au haja kubwa hivyo huwalazimu kwenda kujisaidia, bila ya hivyo wanaweza kuuchapa usingizi mpaka jua linachomoza, ajabu watu hawa tena nao unawakuta wakipayuka Tanzania hakuna usalama ndio maana nasema tusiwashangae wapo kazini na wanatafuta kupata Tonge. Tanzania ni salama sana, tuzidi kuwa wamoja na tuvipe ushirikiano vyombo vyetu vya dola.

Rai yetu kwa watanzania wote ni kuwa lazima dunia ijue kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli tumeamua kuijenga nchi yetu upya hivyo waporaji, wezi, watoroshaji na wanyonyaji wa rasilimali zetu hawapo salama na hawatakuwa, Mafisadi, wakwepa kodi, wauza dawa za kulevya, watakatishaji fedha, wala rushwa na wahujumu uchumi hawapo salama na hawatakuwa huru tena.

Uhuru na usalama wao ni kujisalimisha kwa kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kujenga uchumi usio tegemezi.

2. Serikali ya Tanzania inaminya uhuru wa habari. hoja hii ni kichekesho. Uandishi wa habari duniani kote unaongozwa na miiko na weledi ambapo wakati wote maslahi ya taifa lazima yazingatiwe kinyume na hapo ni kuruhusu matumizi ya kalamu kubomoa nchi au jamii jambo ambalo hatuwezi kulipa nafasi aslani.

Anayeandika na kusema hakuna uhuru wa habari, huyu amepata nafasi ya kuandaa habari yake hadi kuitoa bila bugudha yoyote au gazeti lake kusambaa na kuzika bila bugudha yoyote, ameitisha press conference na kufanya mahojiano na watu wa media akiwa ndani ya Tanzania bila kubugudhiwa wala kuzuiliwa wala kutishwa, yote haya hutokea Tanzania, Kama nchi isingekuwa na uhuru wa habari au Amani na usalama haya wasingefanya.

Ifike pahala watu hawa tuwaogope kama ukoma kwani tukiwaendekeza watatupeleka kubaya. Ikumbukwe wengi wao wametumia keki ya taifa hili kupata elimu nzuri na kuwa walivyo leo ila wamesahau kuwa wanadeni kubwa kwa nchi yao na wanapaswa kuitumikia na kuipenda kwa uaminifu badala ya kukengeuka na kuidhihaki. Ni WASALITI.

Muandishi wa makala hii ni Ndugu Galila Wabanh'u Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
View attachment 1075583
 
Hawezi kujibu huyo ni malaya wa kisiasa anayetoa majibu mepesi kwenye maswali magumu mzee ccm imekufa imebaki kulindwa na tanpol ila soon watapata habari yao
Nadhan ungetusaidia yafuatayo:
1. Ni nani aliye ingia mikataba mibovu ya kuuza rasilimali zetu kwa bei ya kutupwa?
2. Walichukuliwa hatia gani?
3. Ni akina nani walio anza kupigia kelele na kutahadhalisha madhala ya hii mikataba? Walisikilizwa?
4. Ni nani aliye uza gesi yetu? Amechukuliwa hatua gani?
5. Ben saa nane yuko wapi? Nani alimpiga Tundu lisu risasi?
Tusaidie kwa hayo machache.

Ziko nchi nyingi sana Afrika zina amani na wanaheshimu utawala Bora na katiba mfano Ghana na Botswana. Kwa nini tusiige hii mifano mizuri?
 
Back
Top Bottom