Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,494
- 1,874
Kwanza, katiba ya nchi inatoa haki na uhuru wa kutoa maoni yoyote kwa jambo au mtu yeyote ilimradi yasivunje sheria zilizopo. Polepole, Bulembo, Nape, nk.; wote wana haki hiyo.
Pili, si jambo la ajabu na wala si geni kwa wana CCM kutofautiana na kulumbana. CCM ni taasisi kubwa yenye watu wengi ambao si rahisi wote wawe na mtazamo na msimamo mmoja. Wanapishana makanisani na misikitini kwa watu wenye Imani moja, na pengine Bwana mmoja na Ubatizo mmoja, sembuse wanasiasa kwenye vyama vyao?!
Tatu, tusiache kujadili hoja muhimu za kubadili na/au kuboresha mifumo yetu yenye maslahi mapana kwa taifa, kama vile madai ya katiba mpya na maudhui yake, na kuanza kuwajadili watu binafsi kama akina Polepole. Tunapotea na kupoteza muda!