Tusiwabeze Wazee wetu vikongwe wanapoamua kuoa binti mdogo uzeeni; Uzee siyo lelemama

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Wengi huwa hatujisumbui hata kuwaza wazee wetu wanajisikiaje katika umri wao Wa kiutu uzima!

Wengi huwa tunazani anaepaswa kuwekwa karibu ni mzee (mama). Na mzee baba tunamtelekeza!

Ukweli ni kwamba mtu anapoanza kufikia umri wa uzee ndipo huduma ya kupendwa inahitajika zaidi kwake!

Ifahamike kwamba wakati huo mke na mme wanakuwa wamezeeka kiasi cha wote wawili kuhitaji msaada wa kusogezewa vitu vidogo vidogo!

Kibaya zaidi sisi watoto wa mjini mda mwingine huwa tunakosea zaidi kwa kumchukua mzazi mama na kuishi nae mjini! Huku mzazi baba akibaki kijijini akihangaika! (Huwa hatuwazi kabisa kuwa tumechukua mke Wa mtu)

Kwahiyo uzee huongeza machungu zaidi pale mzazi anapoaangalia watoto Wa kuzaa anao lakini wamemtelekeza!

Hapo ndipo mzee baba huamua kutumia Mali zake kutafta mwanamke mwenyewe nguvu ( binti mdogo) Wa kumstili kwa kufunga nae ndoa kabisa!!

Watoto ukisikia mzazi wako anaoa au kuolewa kama hujatimiza wajibu wako kwake, Toa ushirikiano ili harusi yake ifane !!!
 
Nadhani umehusisha pia yule mzee kule chuga, Ushauri mzuri kiongozi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom