Tusiwabembeleze wabunge wa CCM, Wachague wenyewe kupitisha au kutopitisha marekebisho ya Muswada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiwabembeleze wabunge wa CCM, Wachague wenyewe kupitisha au kutopitisha marekebisho ya Muswada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Feb 6, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM ni watu wa ajabu sana. Wameshasahau kwamba suala la Rais kuonana na CHADEMA lilijadiliwa na NEC ya CCM. CCM ndiyo waliomshauri Kikwete asiishie kuonana na CHADEMA bali aonane na vyama vyote vya upinzani.

  Sasa, JK kaonana na wapinzani na taasisi kadhaa anazojua yeye, zingine waziwaz zingine kisiri.


  Matokeo yake kaona kwamba ukweli wa mapendekezo yao haukwepeki na kaamua kuyaingiza kwenye marekebisho ya Muswada ule.

  Kwa maana hiyo NEC itakapokaa tena JK atatakiwa arudishe feedback ya kile CCM ilichomtuma yaani kukutana na vyama vyote vya upinzani.

  Kikwete anaweza kuwaambia "Ndugu zangu NEC, nyinyi wenyewe ni mashahidi, nimesikilza ushauri wenu na nimewaita wapinzani na wanaharakati Ikulu. Wamekuja na hoja zao mmeziona na matokeo mmeyaona".

  Sasa, hawa wabunge ni akina nani kuchukia matokeo ya mkakati unaosimamiwa na Chama chao CCM. Mle bungeni kuna wajumbe tele wa NEC kuanzia Makinda, Makamba, Chenge, Sitta na wengine tele.

  Kama Kikwete kakosea kuwasikiliza wapinzani basi hapa wabunge wanatuambia kuwa hata CCM chama chao kimekosea na hivyo hawakubaliani na mkakati huo.

  Hali hii mimi naifananisha na ile sakata ya G55 kuhusu hoja ya Tanganyika mwaka 1993. Majority walitaka utanganyika na wakapitisha Azimio hilo bungeni tofauti na mkakati au msimamo wa CCM.

  NEC ikaitwa Dodoma na Nyerere akawauliza "nyinyi sera ya Utanganyika mmetumwa na Chama gani?"

  Hivyo, hawa wabunge akina Beatrice Shelukindo na Kilango Malecela na kundi lao wanatakiwa kuulizwa vilevile. Kwamba kama CCM imemuagiza Rais awasikilize CHADEMA na wapinzani wote, wao mle bungeni wanapochukia kisha waukwamishe mmuswada wanatimiza mikakati ya chama gani?

  Ni wazi wabunge hawa hawatimizi matakwa ya CCM wala CHADEMA au chama chochote hasa vile vilivyokutana na Rais Ikulu.
  Chama pekee ambacho hakikukutana na Rais ni hiki CCK kilichovuma wiki jana. Nasema hivyo ni kwa sababu hata vingine vya siku nyingi siwezi kusema havikukutana na Rais kwa sababu tu sikuviona magazetini kwani inawezekana kakutana navyo kisiri.

  Hivyo, wabunge hawa kama hawataki mikakati unaokubaliwa na CCM, CHADEMA, CUF, NCCR na vingine, basi ni wazi kuwa wanakokaribishwa ni CCK tu.

  Ifikie mahali sasa tusionekane kama tunawabembeleza sana hawa wabunge wa CCM kwa sababu ya majority yao mle bungeni. Kwa sababu hoja iliyopelekwa ni ya msingi basi tuwaache waamue wanavyotaka. Kwa lugha nyingine wapime wenyewe.


  Tuendelee na shughuli zetu kama kawaida bila kujali watakalolifanya. Wakiyapitisha marekebisho basi tuseme ni jambo la kawaida. Wakikataa kuyapitisha basi CCK inawasubiri na wasijihangaishe na chama chochote ambacho kimeona mazungumzo ya Ikulu ni ya msingi katka hili.
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu imetulia sana hii hoja yako, kwa hakika, wabunge wa CCM wapime wenyewe....thats great!
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wanaasira na posho, si umesikia wana madeni mengi ndio maana wanataka ongezeko la posho
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  great!!!!!
   
 5. S

  SOBIBOR Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtoto akililia wembe mpe ......................
   
 6. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  magamba wanajua dhahiri kwamba kwa mwamko wa watanzania kwa sasa, mswada wa katiba ijayo hautawapa nafasi ya kufanya unyang'anyi wao kama walivyozoea. Imekula kwao magamba fisadi hao. Cdm hoyeeeee
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  No wonder Rais aliwaambia watumie busara!!! Alishawastukia kuwa wabunge wake hawatumii busara nini??
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Wakikataa wakipita Dar wazomewe tu.
   
 9. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ccm wote na rais wao walivamia hoja ambayo hawaiwezi wala hawana akili ya kuongoza mchakato wa katiba. Hao ni vilaza tusitegemee kupata kitu chochote kizuri kutoka kwao. Kati yao hakuna mwenye goodwill juu ya jambo hili. Anayetegemea ccm iwezeshe kupatikana kwa katiba inayolifaa taifa hili anajidanganya.
   
 10. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nawaunga Mkono Wabunge wa CCM! Kama uzalendo wa Nchi mbona Chadema walitoka Bungeni ilipowasilishwa? Je safari hii CDM hawatoki bungeni? Kama hawatatoka hapo Wabunge wa CCM mjue kuna jambo!
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja yako. Wasipoteze muda wetu kwasababu ya ushabiki wao wa kijinga waliofanya kupitisha muswada bomu. Malipo ni hapa duniani. Hiyo ni aibu yao.
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  wakamugomee huyo aliye waita ktk vikao vyao vya siri wkt huo akawashawishi waupitishe. wenye akili pamoja na rais tumewastukia wasitubabaishe hawa vilaza.
   
Loading...