Tusiwaachie wageni Fursa za biashara jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiwaachie wageni Fursa za biashara jamani

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Malila, Jan 23, 2011.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Nchi yetu ina fursa nyingi za kuwekeza,nyingine ni rahisi na nyingine ngumu kidogo kwa sababu ya kutojua. Kuna biashara hii ya beach plots, kwa sasa inakwenda kimya kimya sana,lakini ni biashara nzuri sana kwa siku za usoni.

  Wakati nataka kujua nini kinaendelea pale Mbamba Bay beach, nimeshitushwa na taarifa kuwa wakuu wa Yerusalem wameshalamba viwanja vyote vya pale Mbamba Bay, nikageuza kibao ili nigeukie Kilwa, nikaambiwa Kilwa yote kwishney, labda nichukue beach yenye coral reefs, lakini bado zipo beach nzuri ambazo hazijaguswa.

  Jamani tusilale na kuwaachia kila kitu kana kwamba sisi hatuna uwezo.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WATANZANIA NI WANGAPI HADI SASA (2005 - 2010) WENYE MAISHA BORA NA HADI HIVI SASA (2010 -2015) WAO WANAJIBIDISHA TU KUTAFUTA KIADA CHAKE NCHINI????

  Watanzania wenzangu tuambizane ukweli hapa na tusifichane hali halisi ndani ya mifuko yetu. Mpaka hivi sasa wengi wetu HATUZUNGUMZII TENAUCHUMI wa maisha yetuTanzania bali hali halisi ni UCHUMA wa maisha yetu nchini. Je, wewe????

  Baya zaidi, ajabu ninayoiona nkule bado CCM na JOPO LA MAFISADI wangependa Watanzania wote tukaseme tu YOTE NI MAISHA na kukimbilia kitanndani, baada kucheka na Masanja TBC, huku CC ya CCM wakibariki Dowans walimpwe.

  Huku waliosbobea katika uchumi nchini wanatutahadharisha KIAMA DOWANS WAKILIPWA na kuongeza kuongeza kwamba tunachoona mpaka sasa kwa gharama ya maisha eti hapo bado ni mwanzo tu wa mapinduzi ya sinema nzima wa ahadi ya Maisha BORA ZAIDI kwa kila Mtanzania; na katika kutimiza hilo Mhe Kikwete na CCM wametuhakikishia dhamira zao za kutufikisha huko kwa Nguvu Zaidi, Ari Zaidi na Kasi Zaidi.

  Sasa Mtu endapo utakuwa hauoni MAISHA BORA ZAIDI basi wala usisubiri kuambiwa na mtu, Wenye kuona UGUMU ZAIDI KWA KILA NAFSI YAKE huyu si Mtanzania tena maana WATANZANIA WOTE waliopata ahadi hizo tangu siku nyingi tu (2005 - 2010) maisha yao ni bora kabisa hivi sasa (2010 - 2015) wanacho kitafu kiukweli ni Uziada wa UBORA HUO WA MAISHA.
  HOJA YANGU:

  Kwa mantki hiyo Mhe Kikwete na CCM, watu wa Takwimu nchini acheni kutu fikicha ukweli, Watanzania ni wastani wa watu wangapi nchini maana hili la watu milioni 46 wala sihitaji tafsiri ya mtaalamu kubani kwamba si kweli.
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hivi Maisha Bora yako wapi
   
 4. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Malila topic imejichanganya hapo juu.(post ya uwezo tuona)
  Swala la kumiliki beach plot ni wazo zuri sana,mwaka 2007 nilienda kilwa nikakuta beach plots zote zimeshachukuliwa na makaburu na vigogo,Mwaka 2009 nikaenda Tanga eneo la Pangani pia plots zimechukuliwa zilizobaki ni kuanzia 40million etc na hapo ni kati ya eka2-7 hivi.leo umeleta habari za Lake Nyasa,sijawahi kufika huko nimeskia kuna beach areas nzuri,
  Nilipokuwa natoka Mtwara around Dec2010 nikawa natafakari kwenda Lindi kucheki beach plots,ila kwa udadisi naskia watu wa karibu na Mama JK wameshahodhi hayo maeneo.
  Wazo la Jamii Farm likishafanikiwa maybe we can attempt Beach Areas.mchango wangu ktk hili tuangalie beach plots karibu na mpaka wa Kenya na Tz kwani hata utalii utaanza kushamiri miaka michache ijayo ukizingatia kenya wamejenga/watajenga Airport nyingine near the Area.
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  kaka lindi na mtwara beach zishuzwa kitambo
  wewe subiri barabara ikikamilika lami uone wamakonde watakavyosogezwa msumbiji na wageni watakaofurika huko
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mimi naamini kuwa beach maarufu zote zimekwisha,lakini beach nzuri nyingi bado zipo mkuu,tatizo hatujachukua uamuzi wa kuzitafuta na kuzimiliki. Taratibu,tunaweza kupata beach nzuri kwa bei poa tu.
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kwa ukanda wa Tanga/Baga/Pangani beach plots ni kizungumkuti,bei ni za kupaa na utapeli kibao. Niliamua kugeukia Nyasa kwa sababu ya future ya Mtwara Corridor, usalama kwa beach hizo huko mbeleni,usafi wake na kumbuka hizo ni za maji baridi, kwa kuogelea ndio zenyewe. Ngoja tuone,dawa ni kufia frontline.
   
 8. Taluma

  Taluma Senior Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa Lilongwe mwishoni mwa mwaka jana, nikafanikiwa kwenda kule Lake Malawi(sisi Nyasa), wenzetu upande wa kule wamejenga mahotel mazuri sana coz hawana bahari wala maziwa mengi kama huku kwetu! Kuna barabara ya lami toka Lilongwe hadi ziwani umbali kama 200 km hivi!
  Ni sehemu muhimu sana kwa utalii malawi.....wakati sasa upande wa tz beach zetu zimetelekezwa, tumelala fofo hakuna tunachokifanya kabisa!
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Yaani beach za nyasa ni nzuri sana mkuu,siku gati la Mbamba bay likipanuka, ndio tutajua kumbe tulilala,watalii watakuja wenyewe bila kelele wala nini.Nitakwenda huko nikajaribu kupambana na wajuba wa serikali yetu, japo nipate eka moja ya kuwaonyesha wanangu kuwa na sisi tuna kasehemu kazuri tunakamiliki kenye maji,hata kama sitaweza kununua speed boat kwa sasa,ila wajukuu watanunua tu na watakuwa na sehemu yao ya kuegesha boat.
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2015
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Beach huko kusini bado zipo nyingi sana. Sikukata tama tangu wakati ule, hatimaye 2015 nimeweza kupata mahali zilipo beach nzuri kwa bei nzuri.
   
 11. renyo

  renyo JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2015
  Joined: May 31, 2013
  Messages: 1,466
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Hio bei nzuri ni ipi????
   
 12. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2016
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mkuu Malila Safari ya mtoni imewadia :)
   
Loading...