Kwanza niwieni radhi kwani thread hii nimeiandika harakaharaka lakini naamini mtaiona ni ya msingi.
Mimi sina shaka na kina Tundu Lissu kufikisha hoja yoyote . Wala siiogopi majority ya CCM mle bungeni ambayo ni 78%. Hivi ingekuwa majority ya CCM bungeni ndiyo kikwazo je Dr. Slaa angethubutu kupeleka hoja ya EPA bungeni tena wakati huo CHADEMAhawazidi watano?
Ukweli alijua majority ni kubwa lakini aliamini amaijenga hoja yake vizuri kisomi kiasi kwamba ukiipinga unajiumbua tu mbele ya jamii. Kilichokwamisha hoja ile ni Spika Sitta mnayemsema alipambana na ufisadi wakati yeye ndiye aliyeizuia kwa kusema hawezi kupokea hoja yenye ushahidi wa internet.
Vinginevyo Dr. Slaa hoja yake ingeunguruma na ingetikisa si bunge tu bali nchi nzima. Inaelekea wengine hawaukumbuki mwaka 1992 ambapo hoja ya Njelu Kasaka ya Utanganyika ilipovurumisha nchi. Njelu Kasaka alijua majority ya wabunge wangeikataa hoja ile lakini yeye alikuwa na wafuasi 55 tu wakijiita G55 wakiwemo Philim Marmo, Generali Ulimwengu na wenzao.
Hoja ile ilishindwa kuzuiwa bungeni hadi Julius Nyerere akaingilia na kuwatungia kitabu Malecela na Kolimba kushindwa kuipinga hoja ya wabunge 55.
Hoja ya Chrisant Mzindakaya ya minofu ya samaki ilimuondoa Proffessa Mbilinyi sikumbuki wizara gani ilikuwa. Hoja nyingine ya Mzindakaya ya vibali vya sukari ilimuondoa Idd Simba kwenye wizara ya Viwanda.
Hivyo tatizo si majority ya wabunge. Tatizo ni uzito na ukweli wa hoja. Uzito na ukweli unaoweza kujengwa kisomi lakini kila mwananchi akauelewa.
Hoja ya tume huru ikipangwa vizuri na ushahidi ukaletwa lazima nchi itetemeke. Kwa mfano CHADEMA ikipeleka bungeni ushahidi mzito unaoonyesha kura za uraisi zilivyochakachuliwa hata kwa jimbo moja tu. Ushahidi wa FOMU za mawakala ambazo na CCM walipata kopi.
Hakuna mwana-CCM mle bungeni anayeweza kuipinga bila kuleta na yeye fomu za mawakala. Kwa sababu wataumbuka. Hivyo mjadala hautafika hata kwenye kupiga kura. Sanasana ili kufuta aibu bunge lote litaamua ipite mara moja.
TUnasahau kuwa hata hoja ya kuwa na vyama vingi ilikuja kwa shinikizo la dunia kubadilika na kwa wana-ujamaa kukosa support Urusi iliposambaratika. Ingekuwa ni suala la majority basi majority yaani 80% walisema hawataki vyama vingi kupitia tume ya Nyalali.
Nyerere alijua wazi hao 80% hawana hoja au hawajui ni kinaendelea duniani ndipo aliposisitiz kwamba vyama vingi lazima vije tu.
Turudi kwenye mifano ya juzi. Ni wana-CCM wangapi mle bungeni tuliwabatiza jina "makamanda wa ufisadi". Hakika hawazidi hata kumi. Lakini wameungurumisha karibu miaka miwili yote ya mwisho ya bunge lililopita. Mbona hapo wingi wa wabunge wa CCM haukusaidia makamanda hao wanyamaze hadi wakaishia kuitana kwenye vikao vyao vya chama na kutaka kuvuana uanachama!?
Hoja ya Halima Mdee na ufisadi wa Kinondoni mbona aliibeba kivyake bila utegemezi tena akitishiwa na Makamba kuchukuliwa hatua. Mbona Makamba mwenyewe aliinua mikono akachomoa mwishoni na hoja ya Halima Mdee ikapita.
Hivyo tusijidanganye na minority yani uchache wa wenye hoja. Hakuna minority ndogo zaidi ya mtu mmoja. Ndiyo maana kuna hoja ya vikundi au hata hoja binafsi ya mtu mmoja. Hoja ikijaa ukweli huna haja ya kupiga debe ikubaliwe. Hoja zinapojadiliwa mle bungeni usidhani wote wanachangia au kupinga. Hata hoja iwe na upinzani vipi sanasana wachangiaji wanaweza wasizidi 20 wakati bunge lina wabunge zaidi ya 200.
Kufikia kupiga kura ni lazima uzito wa hoja uwe umelinganalingana. Mkiipinga kwa minajiri ya kuipiga basi yanaweza kuwatokea puani kama Mudhihiri alivyoleta hoja ya kumuadhibu Zitto Kabwe. Majority ya wabunge ikakubali na Zitto akaadhibiwa. Nini kilifuata. Zito alipokelewa kama shujaa na tangu hapo akawa maarufu. Kwa serikali je, nini kilitokea. Wananchi walipiga kelele kila kona hadi Naibu Spika Anne makinda akalaumu kwamba wananchi wanatakiwa kufundishwa kanuni za bunge. Serikali haikuadhibika hivyo tu. Wiki zilizofuata ikawatuma mawaziri wake kwenda mikoani kumpinga Zitto lakini wakaishia kuzomewa kila kona. Kumbuka wakati huo Dr. Slaa ameshachomoa hoja yake ya EPA lakini siku za Mwembeyanga hazijafika.
Hoja ya RICHMOND ilitimia kwa kuletwa ripoti ya Mwakyembe. Mwakyembe na kamati yake walikuwa hawazidi kumi. Iliposomwa ripoti hawakuchangia zaidi ya watu kumi. Je, ni kina nani walikuja na mchango hoja nzito mle bungeni na ikaleta ubishi ili kuipiga ripoti ya Mwakyembe. Unbishi ambao kama tungefikia deadlock basi ingebidi ipigwe kura. Hakuna. Kama ulisimama ukaipiga ripoti ile basi ulikuwa unajitafutia balaa ambalo ungepona kwa kuhama nchi hii. Balaa la kuzomewa tu na kuitwa fisadi.
Hivyo kama kweli tunataka kusaidia basi humuhumu JF na nchi nzima tujadili jinsi ya kujenga hoja nzito zitakazofikishwa bungeni ili tupate walau Tume huru.
Makala ya Celina Kombani nimeisoma yote. Nilivyomelewa ninaona kama serikali wanajua wananchi wameamka sasa ni lazima ifikapo 2015 Tume huru itakuwa imeshakuja kwa njia zozote.
Mimi naona kama ni maandalizi ya kuonekana kuwa hata wao pia walishiriki kuileta hiyo tume huru kama wanavyojisifu kuleta vyama vingi.
Naishia hapa mengine ongezeeni.