Tusiuogope wingi (majority) wa wabunge wa CCM


K

Kisanduku

Member
Joined
Jul 9, 2009
Messages
90
Likes
21
Points
15
K

Kisanduku

Member
Joined Jul 9, 2009
90 21 15
Kwanza niwieni radhi kwani thread hii nimeiandika harakaharaka lakini naamini mtaiona ni ya msingi.

Mimi sina shaka na kina Tundu Lissu kufikisha hoja yoyote . Wala siiogopi majority ya CCM mle bungeni ambayo ni 78%. Hivi ingekuwa majority ya CCM bungeni ndiyo kikwazo je Dr. Slaa angethubutu kupeleka hoja ya EPA bungeni tena wakati huo CHADEMAhawazidi watano?

Ukweli alijua majority ni kubwa lakini aliamini amaijenga hoja yake vizuri kisomi kiasi kwamba ukiipinga unajiumbua tu mbele ya jamii. Kilichokwamisha hoja ile ni Spika Sitta mnayemsema alipambana na ufisadi wakati yeye ndiye aliyeizuia kwa kusema hawezi kupokea hoja yenye ushahidi wa internet.

Vinginevyo Dr. Slaa hoja yake ingeunguruma na ingetikisa si bunge tu bali nchi nzima. Inaelekea wengine hawaukumbuki mwaka 1992 ambapo hoja ya Njelu Kasaka ya Utanganyika ilipovurumisha nchi. Njelu Kasaka alijua majority ya wabunge wangeikataa hoja ile lakini yeye alikuwa na wafuasi 55 tu wakijiita G55 wakiwemo Philim Marmo, Generali Ulimwengu na wenzao.

Hoja ile ilishindwa kuzuiwa bungeni hadi Julius Nyerere akaingilia na kuwatungia kitabu Malecela na Kolimba kushindwa kuipinga hoja ya wabunge 55.

Hoja ya Chrisant Mzindakaya ya minofu ya samaki ilimuondoa Proffessa Mbilinyi sikumbuki wizara gani ilikuwa. Hoja nyingine ya Mzindakaya ya vibali vya sukari ilimuondoa Idd Simba kwenye wizara ya Viwanda.
Hivyo tatizo si majority ya wabunge. Tatizo ni uzito na ukweli wa hoja. Uzito na ukweli unaoweza kujengwa kisomi lakini kila mwananchi akauelewa.

Hoja ya tume huru ikipangwa vizuri na ushahidi ukaletwa lazima nchi itetemeke. Kwa mfano CHADEMA ikipeleka bungeni ushahidi mzito unaoonyesha kura za uraisi zilivyochakachuliwa hata kwa jimbo moja tu. Ushahidi wa FOMU za mawakala ambazo na CCM walipata kopi.

Hakuna mwana-CCM mle bungeni anayeweza kuipinga bila kuleta na yeye fomu za mawakala. Kwa sababu wataumbuka. Hivyo mjadala hautafika hata kwenye kupiga kura. Sanasana ili kufuta aibu bunge lote litaamua ipite mara moja.

TUnasahau kuwa hata hoja ya kuwa na vyama vingi ilikuja kwa shinikizo la dunia kubadilika na kwa wana-ujamaa kukosa support Urusi iliposambaratika. Ingekuwa ni suala la majority basi majority yaani 80% walisema hawataki vyama vingi kupitia tume ya Nyalali.
Nyerere alijua wazi hao 80% hawana hoja au hawajui ni kinaendelea duniani ndipo aliposisitiz kwamba vyama vingi lazima vije tu.

Turudi kwenye mifano ya juzi. Ni wana-CCM wangapi mle bungeni tuliwabatiza jina "makamanda wa ufisadi". Hakika hawazidi hata kumi. Lakini wameungurumisha karibu miaka miwili yote ya mwisho ya bunge lililopita. Mbona hapo wingi wa wabunge wa CCM haukusaidia makamanda hao wanyamaze hadi wakaishia kuitana kwenye vikao vyao vya chama na kutaka kuvuana uanachama!?
Hoja ya Halima Mdee na ufisadi wa Kinondoni mbona aliibeba kivyake bila utegemezi tena akitishiwa na Makamba kuchukuliwa hatua. Mbona Makamba mwenyewe aliinua mikono akachomoa mwishoni na hoja ya Halima Mdee ikapita.

Hivyo tusijidanganye na minority yani uchache wa wenye hoja. Hakuna minority ndogo zaidi ya mtu mmoja. Ndiyo maana kuna hoja ya vikundi au hata hoja binafsi ya mtu mmoja. Hoja ikijaa ukweli huna haja ya kupiga debe ikubaliwe. Hoja zinapojadiliwa mle bungeni usidhani wote wanachangia au kupinga. Hata hoja iwe na upinzani vipi sanasana wachangiaji wanaweza wasizidi 20 wakati bunge lina wabunge zaidi ya 200.

Kufikia kupiga kura ni lazima uzito wa hoja uwe umelinganalingana. Mkiipinga kwa minajiri ya kuipiga basi yanaweza kuwatokea puani kama Mudhihiri alivyoleta hoja ya kumuadhibu Zitto Kabwe. Majority ya wabunge ikakubali na Zitto akaadhibiwa. Nini kilifuata. Zito alipokelewa kama shujaa na tangu hapo akawa maarufu. Kwa serikali je, nini kilitokea. Wananchi walipiga kelele kila kona hadi Naibu Spika Anne makinda akalaumu kwamba wananchi wanatakiwa kufundishwa kanuni za bunge. Serikali haikuadhibika hivyo tu. Wiki zilizofuata ikawatuma mawaziri wake kwenda mikoani kumpinga Zitto lakini wakaishia kuzomewa kila kona. Kumbuka wakati huo Dr. Slaa ameshachomoa hoja yake ya EPA lakini siku za Mwembeyanga hazijafika.

Hoja ya RICHMOND ilitimia kwa kuletwa ripoti ya Mwakyembe. Mwakyembe na kamati yake walikuwa hawazidi kumi. Iliposomwa ripoti hawakuchangia zaidi ya watu kumi. Je, ni kina nani walikuja na mchango hoja nzito mle bungeni na ikaleta ubishi ili kuipiga ripoti ya Mwakyembe. Unbishi ambao kama tungefikia deadlock basi ingebidi ipigwe kura. Hakuna. Kama ulisimama ukaipiga ripoti ile basi ulikuwa unajitafutia balaa ambalo ungepona kwa kuhama nchi hii. Balaa la kuzomewa tu na kuitwa fisadi.

Hivyo kama kweli tunataka kusaidia basi humuhumu JF na nchi nzima tujadili jinsi ya kujenga hoja nzito zitakazofikishwa bungeni ili tupate walau Tume huru.

Makala ya Celina Kombani nimeisoma yote. Nilivyomelewa ninaona kama serikali wanajua wananchi wameamka sasa ni lazima ifikapo 2015 Tume huru itakuwa imeshakuja kwa njia zozote.

Mimi naona kama ni maandalizi ya kuonekana kuwa hata wao pia walishiriki kuileta hiyo tume huru kama wanavyojisifu kuleta vyama vingi.

Naishia hapa mengine ongezeeni.

 
M

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
445
Likes
1
Points
35
M

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2010
445 1 35
Mwana JF Kisanduku umenifurahisha kweli kweli !!!!!!! kwa thread yenye kuondoa wasiwasi na kuingiza ujasiri , jinsi hoja hizi nzito za Tume Huru ya Kuchunguza matokeo ya uchaguzi; Katiba Mpya (kama ile ya Kibaki/Raila!!!!); Tume Huru ya Uchaguzi!!!!!; Kupunguza madaraka ya rais; viporo vya EPA,na Richmond; zinavyokwenda kupita bila kupingwa mjengoni!!!!!!!!!Tamu kweli kweli!!!!!!! JF tuelimishe hata wabunge wa sisiemu walio mbumbumbu kwamba wakitaka kuchaguliwa 2015, waangalie Tundu Lissu anatetea hoja ipi waiunge hiyo hiyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hapo full support!!!!!!!!!!!!
Unajua hata mkwere akiwa mjanja anaweza akaitosa sisiemu kwa kukimbiza hoja hizi kwenye line ya Dr wa PhD na kusapraise watanzania kiasi kwamba at the end of his term (2015) sisiemu ikapinduliwa na CDM lakini yeye mkwere akipata legacy ya kuandika Katiba Mpya; Tume Huru ya Uchaguzi Mpya (akawatelekeza makame na kiravu-maana nani atamshika shati tena???????); na Kupunguza Madaraka ya rais Dr wa PhD-si ndivyo anavyotaka Dr wa PhD??????????? Safi sana mwana JF Kisanduku kwa kuleta thread hii!!!!Congrats!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
S

SubiriJibu

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2009
Messages
1,441
Likes
1,129
Points
280
S

SubiriJibu

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2009
1,441 1,129 280
Ukweli ni kwamba hoja bungeni hupita kutokna na uthabiti wake na si kutegemea wingi wa wabunge au wanaoipenda.

Kumbuka Seneti ya USA ilikuwa imepania kumnyima George Bush hela za kwenda kuipiga Iraq. Ilibidi Bush mwenyewe abebe mikoba yake toka White House na ninakumbuka alitumia masaa mawili akitoa speech ni kwa nini anahitaji kwenda Iraq.

Seneti wote walimsikiliza huku wakitumbua macho toka mwanzo wa speech hadi mwisho. Baada ya hotuba hakuna yeyote aliyeinuka kupinga vita, si Democrat au Republic. Wote waluinga mkono hoja na Marekani ikaingia vitani.

Hivyo watanzania tujenge hoja nzito inoyokublika tuone kama kuna mbunge anatakeinuka kuipinga, achilia mbali kuipigia kura.

Hoja ya TUme Huru ni rahisi sana kuijenga hata kama kusingekuwa na vipanga kama Wilbroa Slaa au Tundu Lissu. Ni kwamba tu hakukua na wa kuishikia bango.

Lakini sasa wakati ndiyo huu.
 
Cassava

Cassava

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
282
Likes
7
Points
35
Cassava

Cassava

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2010
282 7 35
SWALI. Je? mnafahamu ili hoja ijadiliwe bungeni inahitaji kupita kwa na nani kwanza?

Kila mbunge anaibua makabrasha yake ya hoja na kuanza kuisoma Bungeni? Tafakarini kwanza.
 
Mpelijr

Mpelijr

Member
Joined
May 17, 2010
Messages
89
Likes
12
Points
15
Mpelijr

Mpelijr

Member
Joined May 17, 2010
89 12 15
Kweli na tusishindwe kupaza sauti na kuongea mambo ya muhimu bungeni kwa hofu hiyo pia!!!
 
Questt

Questt

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2009
Messages
3,013
Likes
30
Points
135
Questt

Questt

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2009
3,013 30 135
Kisanduku u have reveled the reality in TRUTH.....U r 99% right the 1% remains kwa watoa hoja na waunga Hoja....I think its time up not to rush kutumia nguvu ya Uma wakati wana nafasi ya kuupeleka Ukweli mezani.....kama wataukataa ukweli na wananchi tukajua hapo upo ukweli na umekataliwa kwa kulinda maslahi ya CCM then nina uhakika hata watoto wa shule ya Msingi wataingia Barabarani kama wazee wa EAC.
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,219
Likes
878
Points
280
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,219 878 280
sina hofu na idadi ya wabunge wa ccm coz kazi yao kubwa ni kulala tu bungeni wakisubiria siku iingie wavute posho.
 
K

Kisanduku

Member
Joined
Jul 9, 2009
Messages
90
Likes
21
Points
15
K

Kisanduku

Member
Joined Jul 9, 2009
90 21 15
SWALI. Je? mnafahamu ili hoja ijadiliwe bungeni inahitaji kupita kwa na nani kwanza?
Kila mbunge anaibua makabrasha yake ya hoja na kuanza kuisoma Bungeni? Tafakarini kwanza.
Mkuu Cassanova,

Nashukuru kuwa kwa maelezo yako unakubaliana na hoja zangu isipokuwa tatizo kwako ni utaratibu wa kuzifikisha hoja hizo bungeni. Sidani kama hilo ni tatizo ndiyo maana kuna kanuni za bunge ambazo kila mleta hoja azipitie iwe ni serikali, mbunge au kamati. Na kama umenisoma nieeleza mifano mingi ya hoja zilizopelekwa na zikafaulu kutikisa bunge.

Kisanduku u have reveled the reality in TRUTH.....U r 99% right the 1% remains kwa watoa hoja na waunga Hoja....I think its time up not to rush kutumia nguvu ya Uma wakati wana nafasi ya kuupeleka Ukweli mezani.....kama wataukataa ukweli na wananchi tukajua hapo upo ukweli na umekataliwa kwa kulinda maslahi ya CCM then nina uhakika hata watoto wa shule ya Msingi wataingia Barabarani kama wazee wa EAC.
Mkuu Questt,

Nashukuru shukrani zako kunielewa. Labda niongezee kwa kutofautiana na wewe kuhusu kutumu=ia nguvu ya umma. Kama tumekubaliana kuwa tusiogope kupeleka hoja zille bungeni na hatuna wasiwasi na majority ya CCM, basi mimi naamini tutumie kwanza nguvu ya umma kabla ya kuzipeleka hoja zile bungeni.

Tunapotumia ngvu ya umma si kwamba umma utoe maamuzi. La hasha. Umma ueleweshwe kwamba tunachokipeleka bungeni ni hiki na kile. Kwamba bunge lijalo tunapeleka hoja ya kuundwa kwa Tume huru, uwezezekano wa kushiitaki matokeo ya rais kama inavyofanyika kwa wabunge na kadhalika.

Wakati huo tunazunguka nchi nzima kuwaeleimisha tunachoenda kudai bungeni huku tukiwahimiza kufuatilia kwa makini bunge kwenye TV na hansard ili kujua jinsi hoja ilivyofikishwa na ilivyojadiliwa.

Baada ya kuzunguka nchi nzima, maredioni, mitandaoni, midahaloni, basi hoja inatinga bungeni. Ushahidi wa kura zilizochakachuliwa uwe mikononi palepale bungeni.

Sasa tuone ni nani anayeweza kuinua kidole chake na kuleta point za kijinga kupinga hoja ile ya kubadili TUme iwe Tume huru!

Ikifanyika hivi hakuna mbunge anayeweza kuinia uso wake kuipinga akijua kila mwananch anasubiri kwa hamu mjadala wa hoja hizo.

Usishangae wabunge wa CCM wakaomba udhuru kutohudhuria mijadala hiyo wakijua ngoma ni nzito. Kwani akitoke mmoja tu kuipinga siku ya kwanza utanisikilizia kelele kwenye magazet na mitaani kesho ake!

Kama unakumbuka mbinu hii nidyo ilitumika na wanaharakati wa gender mwaka 1997 ilipopitishwa sheria ya kujamiiana. Ukweli sheria ile ilibeba pia mamo ya kijinga. Eti ukimkonyeza mwanamke kwa jicho tu tayari umeshamnyanyasa kijinsia! Unadhani kwa akili ya kawaida mbunge gani angependa aonekane amepitisha sheria yenye utata kama huu.

Ukweli ni kwamba wabunge waliipitisha kwa shinikizo si la wabunge wenzao bali TAMWA na taassisi zote za kijinsia zilitanda nje ya jengo la bunge na mabango wakisubiri hatima ya sheria hiyo. Ama inapitishwa au haipitishwi. Eti mnasema kusubiri matokeo kucha ilifanyika mwaka huu Nyamagana, Arusha mjini, Kawe na kwingineko! Walichkifanya wanaharakati wale pale bungeni ni sawa kabisa na kusubiri matokeo ya upitishwaji wa sheria ile.

Hebu nikumbushe ni mbunge gani aliinuka hata kusema neno. Ilipita bila kubadilishwa hata nukta.

Hivyo hoja hizi za sasa zikieleimishwa ipaswavyo kwa wingi unaostahili, mimi sitarajii kama kuna mbunge anataka kuchafua CV yake kuitamkia neno baya.

Sijui wenzangu mnasemaje.
 

Forum statistics

Threads 1,236,300
Members 475,050
Posts 29,253,371