Tusitengeneze hamaki: Hizo kura feki zinapigwaje?

Platnam

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
480
500
Kuna taarifa nyingine za kitumbafu Sana kama hii ya kwenu.

Kadanganyaneni pale ufipa.

Bila mtuhumiwa wala ushahidi, hii ni stori ya kutunga. Kwaheri kamanda.
Mtuhumiwa ni Tume ya uchaguzi.
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,869
2,000
Tatizo sio kura feki.
Tatizo NEC WANAKATAA HAKUNA KURA FEKI KWANINI WANAKATAA?
TUANZIE HAPO
Amini kuwa zimetengenezwa ili kuchafua uchaguzi,, we hujiulizi kwann unapata picha za kura tu ila za aliyekamatwa nazo hupati?
 
The Invincible

JF-Expert Member
May 6, 2006
5,939
2,000
Mimi nilipoingia kituoni, msimamizi akanipa karatasi mbili za mgombea Urais. Niliposhtuka, akajifanya amekosea. Sasa hapo maana yake mimi ningepiga kura ya Urais kwenye karatasi mbili. Hii ni namna mojawapo ya kutengeneza kura feki. Huko nje kabla ya kuingia, nilikuwa napiga stori na kiongozi mmoja wa CCM ninayefahamiana naye. Mawakala walikuwa 2 tu. It is so simple, man.
 
yomboo

JF-Expert Member
May 9, 2015
6,235
2,000
Ni muhimu Sana wakati huu kuwa makini na taharuki au hamaki. Madai ya uwepo wa "kura feki" hata Kama yanatolewa na watu makini na wenye akili ni lazima yachukuliwe kwa uzito unaostahili. Hata hivyo yasichukuliwe Kama yanavyotolewa bila kuyahoji.

1: Hizi kura feki zimekutwa au kukamatwa wapi? Chumba cha kura, gari la kula, kwa mtu, mitaani, mtu kazificha kwenye begi au mfukoni?

2: Ni nani kakutwa na kura hizo? Msimamizi wa Uchaguzi, Kiongozi wa chama, wakala, kiongozi wa serikali, mgombea, Polisi? Huyo aliyekuwa nazi anaweza vipi kuziingiza chumba cha siri?

3: Hizi kura feki siyo zile zenye alama za "SPECIMEN"? Au ni makaratasi ya mfano?

4: Kama hizi karatasi ni halali NEC kwanini wanachelewa kutoa maelezo na kuondoa taharuki? Usije kuwa wamekuwa compromised kiasi kwamba hawajui karatasi za kura ziko wapi na isije kusababisha kufutwa kwa uchaguzi mkuu kwa kisingizio cha karatasi za kura kuibwa.

IGP Sirro na wenzako hapa ndio mnatakiwa kuwafanya vijana watulie. Tayari wapi walioanza kuhamaki.

halahala mti na jicho.

Tusitengeneze taharuki na hamaki isiyo ya lazima.
Wewe Ni takakaka sana
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,869
2,000
Mtihani umevuja
NEC watuambie hizo karatasi ni za kwao au sio za kwao?.
Kama za kwao imekuwaje zimekamatwa nje ya vituo vya kura..
Kama sio za kwako zimetoka wapi?
Screenshot_20201028-191013.jpg
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,869
2,000
Upinzani msikubali mpaka NEC.waseme imekuwaje hizo karatasi za kura zimepatikana uraiani.zimeibwa ? Au zimetengenezwa feki.
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,869
2,000
UPINZANI Tanzania muwe na kauli moja.
Uchaguzi urudiwe.
VINGINEVYO MTAKUJA kulia kilio Cha mbwa mwizi.
 
Mao Tanzania

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
208
250
Ni muhimu Sana wakati huu kuwa makini na taharuki au hamaki. Madai ya uwepo wa "kura feki" hata Kama yanatolewa na watu makini na wenye akili ni lazima yachukuliwe kwa uzito unaostahili. Hata hivyo yasichukuliwe Kama yanavyotolewa bila kuyahoji.

1: Hizi kura feki zimekutwa au kukamatwa wapi? Chumba cha kura, gari la kula, kwa mtu, mitaani, mtu kazificha kwenye begi au mfukoni?

2: Ni nani kakutwa na kura hizo? Msimamizi wa Uchaguzi, Kiongozi wa chama, wakala, kiongozi wa serikali, mgombea, Polisi? Huyo aliyekuwa nazi anaweza vipi kuziingiza chumba cha siri?

3: Hizi kura feki siyo zile zenye alama za "SPECIMEN"? Au ni makaratasi ya mfano?

4: Kama hizi karatasi ni halali NEC kwanini wanachelewa kutoa maelezo na kuondoa taharuki? Usije kuwa wamekuwa compromised kiasi kwamba hawajui karatasi za kura ziko wapi na isije kusababisha kufutwa kwa uchaguzi mkuu kwa kisingizio cha karatasi za kura kuibwa.

IGP Sirro na wenzako hapa ndio mnatakiwa kuwafanya vijana watulie. Tayari wapi walioanza kuhamaki.

halahala mti na jicho.

Tusitengeneze taharuki na hamaki isiyo ya lazima.
Za siku nyingi Kaka Mkubwa. Umepotea Sana.
 
Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,589
2,000
Amini kuwa zimetengenezwa ili kuchafua uchaguzi,, we hujiulizi kwann unapata picha za kura tu ila za aliyekamatwa nazo hupati?
Wewe jamaa bhana na yule aliye kimbia na box la kura kwa pikipiki nae ni upinzani wamemtengeneza?
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,576
2,000
Kama kweli umeandika hii kwa makusudi kabisa bila kukusudia kupotosha basi you are out of touch with reality.

Kura feki ni kura zilizopigwa (i) nje ya kituo na/au (ii) ndani ya kituo zisizo halali.

Nje ya kituo ni zile ambazo zimepigwa tayari zinazoingizwa ndani ili zijumuishwe na kura halali.

Hizi ni same ballot paper na hizo halali hivyo huwezi kusema ni “fake” zikishachanganywa na kura halali.

Njia rahisi sana ya kudhibiti hii ni kupekua wote wanaoingia na mifuko au mabegi kwenye vituo mbele ya mawakala wote.

Hii haifanyiki. Kwanza mawakala wanakamatwa na kufukuzwa vituoni. Wengine hawaruhusiwi kuingia vituoni.

Hakuna anayepekuliwa akiingia kituoni.

Inaonyesha kuna watu wana access na ballot papers na wameshazitumia kabla ya siku ya uchaguzi leo.

Kura zisizo halali ndani ya kituo ni pale vituo vinapofungwa na kukosekana mawakala wa upinzani. Karatasi zilizobaki zinapigwa kura feki na kujumuishwa.

Kama upo Tanzania na umeenda kituo chochote utaona hizi weakness. Kama umekutana na wakuu wa wilaya au wakurugenzi wa uchaguzi kituoni utaelewa hili.

They are above the law. Mbaya zaidi kuna watu wamekamatwa na kura feki.

Ni jambo moja kushabikia mtu au chama, ni jambo lingine kukemea uovu.
Kura feki CCM walipiga jana usiku, wakaziweka kwenye mabegi halafu walipofika asubuhi mapema kwenye vituo wakaingiza ndani ya vituo, ndio kama Zitto anavyokwambia alikutana na mtu kabeba sanduku limejaa kura anazitoa kama vile watu walishapiga zikajaa,kumbe ni uongo saa moja asubuhi hilo sanduku limejazwa na nani wakati wapiga kura walikuwa bado hawajafika?!

Au kwa kesi ya Mdee, yeye alizunguka kwenye vituo asubuhi akazikuta tayari hizo feki ziko ndani, maana yake either ziliwekwa jana usiku au mapema sana leo asubuhi, halafu kutekeleza huu mpango vizuri, mkurugenzi akawaambia mawakala watazikuta barua zao za utambuzi vituoni, ili mkurugenzi achelewe kupeleka barua then CCM wapate muda wa kupeleka kura zao feki, na mawakala wakija wazuiwe kwa kukosa barua za utambulisho.
 
DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
483
1,000
Ni muhimu Sana wakati huu kuwa makini na taharuki au hamaki. Madai ya uwepo wa "kura feki" hata Kama yanatolewa na watu makini na wenye akili ni lazima yachukuliwe kwa uzito unaostahili. Hata hivyo yasichukuliwe Kama yanavyotolewa bila kuyahoji.

1: Hizi kura feki zimekutwa au kukamatwa wapi? Chumba cha kura, gari la kula, kwa mtu, mitaani, mtu kazificha kwenye begi au mfukoni?

2: Ni nani kakutwa na kura hizo? Msimamizi wa Uchaguzi, Kiongozi wa chama, wakala, kiongozi wa serikali, mgombea, Polisi? Huyo aliyekuwa nazi anaweza vipi kuziingiza chumba cha siri?

3: Hizi kura feki siyo zile zenye alama za "SPECIMEN"? Au ni makaratasi ya mfano?

4: Kama hizi karatasi ni halali NEC kwanini wanachelewa kutoa maelezo na kuondoa taharuki? Usije kuwa wamekuwa compromised kiasi kwamba hawajui karatasi za kura ziko wapi na isije kusababisha kufutwa kwa uchaguzi mkuu kwa kisingizio cha karatasi za kura kuibwa.

IGP Sirro na wenzako hapa ndio mnatakiwa kuwafanya vijana watulie. Tayari wapi walioanza kuhamaki.

halahala mti na jicho.

Tusitengeneze taharuki na hamaki isiyo ya lazima.
Wewe jamaa siku zote ni mnafiki tu. Toka enzi zile ukiwa CHADEMA. Mimi ni mwana CCM, ila haki kwanza.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,576
2,000
We nawe kwani hujawahi kusikia watu wamekuwa na mihuri ya taasisi mbalimbali za serikali....
Wacha ubishi we babu, ushahidi wote wa kimazingira unaonesha CCM ndio wahusika wa hizo kura feki, usilete ubishi wako hapa wa majibu ya kuokoteza kujiokoa na hilo chama lako feki.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,576
2,000
Kama kigogo anaeza access habari nyeti za serikali, mbona muhuli ni kitu kidogo sana kuupata. Hizo kura wametengeneza wao wenyewe CHADEMA.
Kura watengeneze Chadema halafu wampigie mgombea wa CCM?!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom