Tusitegemee kupata katiba mpya na hata iliyopo itanajisiwa.

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,344
Kwa namna mambo yanavyoonekana, watanzania tutegemee kuishi katika awamu ya utawala ambao hautakuwa wa haki wala sheria, tuendelee kucheka tu lakini baadaye tutasaga meno.

Kauli nyingi zinazotolewa na mkuu wa nchi hivi sasa zinaonyesha dhahiri huko tuendako hakutakuwa na utawala wa kisheria, anayebisha asubiri atajionea.

Na kwa msingi huo huo nina imani tusahau habari ya kupatikana kwa katiba mpya ya wananchi kama tulivyotegemea, na kama utatokea muujiza ikapatikana katika awamu hii basi itakuwa katiba mbaya kuliko ile iliyopendekezwa.

Viashiria na ushahidi wa jambo hili uko wazi kwa kila anayefuatilia kwa makini siasa za nchi yetu, hasa yanayofanywa na wakuu wa wilaya, mikoa mpaka kwa viongozi wa ngazi ya kitaifa.
 
Back
Top Bottom