Tusitegemee fedha kuleta maendeleo

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
523
239
Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza
kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka
nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili.
Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo
zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani
ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga
viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo.
Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote
zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa
msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata
katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili
zisaidie Serikali kuondoa dhiki.
Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza
kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo

maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania,
matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza
mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo
yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili
kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna
Serikali ya Dunia nzima. Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa
huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe.
Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom