Tusitawaliwe na ushabiki wa itikadi za vyama vyetu tunawaomba Wana CCM!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Tunawaomba wana CCM muwe watulivu tuweke tofauti za kisiasa pembeni kwanza tumuachie Rais Jakaya na Team yake wapitie mapendekezo ya CHADEMA kuhusu rasimu ya mswaada uliopelekwa kwake Jana tunaomba tusilete unafiki wakisiasa kwani hii katiba inayotakiwa kutengenezwa siyo ya CHADEMA pekee, bali niyetu sote watanzania na vizazi vyetu!Tuna amini Rais Jakaya Kikwete ni mtu mwelewa na siyo mtu wakusikiliza wambeya wa mtaani hivyo nibudi tukampa nafasi ya kutafakari zaidi juu ya mapendekezo ya CHADEMA juu ya rasimu ya mswaada wa kutengeneza katiba mpya (Road Map),ili hata kabla ya kuusaini mswaada huo ulio wasilishwa kwake hivi karibuni.Nimatumaini yangu kwamba baada ya majadiliano yatakayo anza leo saa Nnne asubuhi ya tarehe,28/November/2011.Nidhahili Rais atakaa na na wana CCM na serikali yake watayajadili waliyoyakuta kwenye Mapendekezo na watayatolea majibu yatakayo kidhi kihu ya walio wengi kwani tumeona sehemu yote ya nchi wakilalamikia juu ya upitishwaji wa rasimu jinsi ambavyo haukuzingatia matakwa ya wengi!! ila mimi ninachowaomba wasitawaliwe na itikadi au kuona kama wamekosolewa na upinzani nakuona wameshindwa japo wao walishinda kule bungeni,Hivyo ushabiki wa vyama uwekwe pembeni tutawaliwe na Uzalendo hii ni Tanzania yetu sote.
Mimi hiyo ndiyo Rai yangu kwa Asubuhii ya leo.
 
Back
Top Bottom