Tusitamani kulirejesha taifa letu kwenye ukingo wa kuwa jumuhuri ya ndizi (banana republic). Tuhuma zote zidhaminike kisheria

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,540
46,080
Jamuhuri ya ndizi ni jina lilioibuliwa karne ya ishirini kuyaelezea mataifa yaliyokuwa na uchumi legevu wenye kutegemea zao moja na yaliyokuwa na rushwa pamoja na matatizo mengi ya kisiasa yaliyokoshea utulivu huko Latini America.

Leo hii matumizi ya jina hilo yamepanuka kujumuisha zaidi mataifa yenye serikali katili zisizozingatia utawala wa sheria na haki za watu (tyrannical governments).

Katika jumuhuri za ndizi haki za watu haziamuliwi kwa muda sahihi katika mahakama huru kupitia michakato sahihi ya kisheria na yenye kuonyesha haki imetendeka.

Ishara mojawapo kubwa ya jamuhuri ya ndizi ni watu kukamatwa kwa mashinikizo ya kisiasa badala ya weledi wa vyamba usalama na uchunguzi, dhamana kutumika kama silaha na serikali na kesi kupigwa dana dana ili zikae muda mrefu mahakamani.

Inashangaza kuona kuna taifa letu lina watu wenye roho mbaya kiasi cha kutamani watu wasweke tu magerezani kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo bila kesi zao kuamuliwa na mahakama.Hawa wamefungua nyuzi wiki hii yote wakikijeli hatua za awamu ya sita kupitia DPP na kuawaachia watuhumiwa wenye kesi za miaka mingi waliokuwa wanasota magerezani kwa kigezo cha ushahidi kutokamilika.

Hatua aliyoichukua DPP ni sahihi sana lakini serikali iende mbele zaidi kuruhusu dhamana kwa tuhuma zozote zile.Hili ni jambo rahisi sana kwa sababu hakuna mtu anayestahili kufungwa kwa kutuhumiwa tu bila mahakama kutoa hukumu.
 
Kwa nchi za ki-africa kuweka makosa yote yae na dhamana ni kutengeneza taifa gumu na lisilotawalika.

Sometimes Sheria ngumungumu zinapunguza mengi.

Chukulia mfano tu pamoja na hayo makosa kukosa dhamana bado watu wanayafanya kwa kiwango Cha juu, fikiria Sasa wakiondoa dhamana hali itakuaje?
 
Kwa nchi za ki-africa kuweka makosa yote yae na dhamana ni kutengeneza taifa gumu na lisilotawalika.
Sometimes Sheria ngumungumu zinapunguza mengi.
Chukulia mfano tu pamoja na hayo makosa kukosa dhamana bado watu wanayafanya kwa kiwango Cha juu, fikiria Sasa wakiondoa dhamana hali itakuaje?
 
Tofautisha kati ya kushtakiwa na kupewa dhamana. Polisi wanaweza kumfikisha mtu mahakamani wakamshataki, akapewa dhamana na kesi yake ikaendelea bila kukaa gerezani muda wote kesi inaposikilizwa.
Yes umesema yote, yaani kwa kifupi mwenye hela Kamwe hatakaa ashtakiwa kwa Kuwa anadhaminika na mtu yoyote
 
Back
Top Bottom