Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Nasikia huko Jamhuri ya watu wa kusadikika wamekagua benki kuu yao wakaona hakuna pesa za kigeni. Yani reserve ya pesa za kigeni ni ndogo sana kiasi kwamba haitoshi kufanya purchase nje kwa miezi kadhaa ijayo. Kwahiyo wameamua kwenda kuzitafuta kwenye maduka ya kubadili fedha. Wanaamini zimefichwa huko. Kwamba wenye maduka wamezibana na hawataki kuziachia. Kwahiyo wameamua kwenda kuzisaka kwa mitutu ya bunduki. Songombingo za Kaboka mchizi.!
Ngoja niwape shule kidogo. Sababu za msingi za kupotea kwa 'dola' katika nchi hiyo ni hizi hapa.
#Mosi; nchi huwa inapata pesa za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje. Lakini nchi ya kusadikika imezuia kuuza mazao nje. Nasikia huko mahindi yanaozea ndani, mbaazi ndo kwisha habari yake, tangawizi hata ukitupa watu hawaokoti. Hivyo vyote vilikuwa vina soko kubwa nje ya nchi na vinaingizia nchi hiyo pesa nyingi za kigeni. Lakini mfalme wao akapiga marufuku wasiuze nje. Leo wanamtafuta mchawi. Maajabu.!
Koro-show nasikia nayo imezuiwa kuuzwa nje. Serikali ktk nchi ya kusadikika imesema itanunua yote. That means hakuna pesa zozote za kigeni nchi hiyo itaingiza. Kama makampuni binafsi kutoka nje yangeruhusiwa kununua yangekuja na 'dola'. Wangechange na kupata madafu ya kulipa wakulima. Hayo 'madola' yaliyochenchiwa yangeingia kwenye mabenki na hatimaye benki kuu. Kwahiyo serikali ingeongeza reserve yake ya pesa za kigeni. Lakini wameamua kununua koro-show zote wenyewe, leo wanatafuta dola kwa mitutu?
Na mfalme wao amesema akikosa soko atamwambia kila mtu kwenye nchi hiyo ale ratili mbili za koro-show. Hizo ratili mbili kwa kila raia zinanunuliwa kwa pesa ya madafu na zitaliwa na raia wa humohumo ndani. Kwahiyo koro-show zote zinaweza zikaisha bila kuingiza hata dola moja kwenye nchi hiyo. Hii ni biashara kichaa ktk historia ya biashara duniani.!
#Pili; nchi inapata pesa za kigeni kupitia mikopo na misaada mbalimbali ya kimataifa kama vile kutoka Benki ya dunia, IMF, na mataifa wahisani kama Marekani, Umoja wa Ulaya etc. Sasa nasikia Benki ya dunia imesitisha mikopo na misaada kwenye nchi hiyo. Baadhi ya mashirika ya kimataifa nayo yamesitisha shughuli zake huko. Umoja wa Ulaya nao unafikiria kusitisha misaada yote kwa nchi hiyo, na tayari balozi wao ameshafurushwa. Kwahiyo hakuna 'foreign grant wala loan' ambayo inaingiza pesa za kigeni kwenye nchi hiyo kwa sasa. Lakini wanaenda kutafuta pesa za kigeni kwa AK47 kwenye maduka ya kubadili fedha. Hekaya za Abunuasi.!
#Tatu; Nchi inapata pesa za kigeni kwa kukaribisha wawekezaji wa kigeni kwa wingi (Foreign investors). Mwekezaji akienda kujenga kiwanda katika nchi fulani haendi na pesa za madafu, anaenda na dola. Akifika huko hizo dola anazibadili na kupewa madafu. Dola zinaingia kwenye system na kuongeza reserve ya pesa za kigeni.
Lakini kwenye nchi ya kusadikika foreign investors wanafokewa na kunyang'anywa passport. Kiongozi akishashiba 'ugali tembele' anaropoka tu 'mnyang'anyeni passport'. Matokeo yake wawekezaji wanahamisha mitaji na kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine. Leo nchi ya kusadikika iko busy kutafuta nani kaficha pesa za kigeni kwenye sandarusi. Harakati za pimbi.!
#Nne; nchi inaingiza pesa za kigeni kutokana na jinsi inavyouza utaalamu wake nje ya nchi. Lakini kwenye nchi ya kusadikika wataalamu wamezuiwa kwenda kufanya kazi nje. Serikali yao imesema mtu yeyote anayepata kazi nje ya nchi inabidi aombe kibali kwanza akiambatanisha mkataba wa ajira. Na serikali inaweza kumruhusu au kumkatalia. Leo serikali hiyohiyo ipo 'busy' kutafuta dola kwenye maduka ya wahindi. Futuhi.!
#Tano; Njia nyingine ya kumaintain pesa za kigeni ni kuregulate kiwango cha kununua na kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi. Unatakiwa kuuza zaidi kuliko unavyonunua. Hakikisha unanunua nje vitu vya muhimu tu. Vingine vitengeneze mwenyewe. Hii ni kwa sababu kila unapoagiza bidhaa yoyote nje ya nchi unapunguza reserve yako ya pesa za kigeni. Lakini kanchi ka kusadikika kanatumia reserve yake ya pesa za kigeni kununulia hadi toilet paper, halafu leo kanatafuta pesa zilikofichwa. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.!
Malisa GJ