Tusisubiri vyombo vya Magharibi viseme

babumapunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
4,636
2,000
Tusisubiri CNN Waiambie Dunia Mchango Wa Tanzania Kwa Ukombozi Wa Afrika...!

Kazi hiyo tuifanye sisi wenyewe.

nilimwona Rais wa
Ghana John Dramani Mahama akihojiwa na CNN kuhusiana na
Mandela. Mara tatu Rais huyo wa Ghana aliutaja mchango wa
Tanzania katika ukombozi wa Afrika ikiwemo Afrika Kusini ya Nelson
Mandela.
-Hivi ni wangapi wanajua kuwa kiongozi wa kwanza wa chama cha
ukombozi katika nchi huru ya Kiafrika ambaye Mandela alikutana nae
anaitwa John Mwakangale. Huyu alikuwa kiongozi katika TANU na
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
-Hivi ni wangapi wanajua kuwa Mji wa kwanza katika nchi huru ya
Kiafrika ambayo Mandela alikanyaga ardhi yake unaitwa Mbeya. Hivyo
basi, Tanganyika ndio nchi huru ya kwanza ya Kiafrika ambapo
Mandela alikanyaga ardhi yake.
- Hivi ni wangapi duniani wanajua, kuwa Julius Nyerere ndiye Rais wa
kwanza katika nchi huru ya Kiafrika ambaye Mandela alikutana nae. Na
ni Julius Nyerere baada ya kumkubali Mandela, ndiye aliyemsaidia
Mandela kwa kumtambulisha kwa Mfalme Haille Selassie wa Ethiopia?
Haikuwa ajabu, kuwa baada ya kutoka gerezani, kwa Mandela
Tanzania ikawa nchi ya kwanza kuitembelea.
Kumbukumbu hizi muhimu za kihistoria na nyinginezo Watanzania
hatupaswi kuisubiri CNN na vyombo vingine vya habari vya
kimagharibi viitangazie dunia.

Ni jukumu letu wenyewe.
 

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,147
2,000
Ngoja JK atoke South tum PM aende makao makuu ya CNN kuipigia promo TZ! Lakini naomba kuuliza swali ya kuudhi kidogo... What is so spesho Mandela kuitembelea Tanzania at first?
 

NYAREMA

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
362
500
Let bygones be bygones wewe suala la mandela limekwisha. Usipende misiba sana isiyokuhusu kwani alipokuja Tanzania so what?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom