Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Wakuu, nawasalimu kwa jina la Bwana wa Majeshi.
Wote tunajua jinsi uhuru wa Tanganyika ulivyopatikana. Kwa kifupi ulipatikana kwa njia za majadiliano na diplomasia.
Ningependa sana kuona kila tunapokaa kusherehekea uhuru wetu, tukumbushane jinsi gani majadiliano, ustaarabu na diplomasia inavyoweza kuwa chachu ya kuimarisha uhuru wetu na kutuletea maendeleo.
Kuna kirusi kimeingia katika fikra za uongozi nchi hii zinazofanya viongozi wawe watawala. Wananchi hawasikilizwi tena wanataka nini, amri zimetawala na maamuzi ya hovyo yanafanyika na hakuna kuwajibishana.
Kutishana kumezidi sana nchi hii. Hakuna kati yetu mwenye milki ya nchi hii, haijalishi tofauti zetu za kisiasa, kiimani, kikabila wala kipato.
Turudi kwenye kusikilizana na tutoke kwenye kuumizana. Hapo ndiyo uhuru wa nchi hii utakuwa na maana kwa kila mmoja wetu.