Tusishangae ya Shigela. Ni Matunda ya Uongozi Mbovu wa Mwenyekiti wa Chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusishangae ya Shigela. Ni Matunda ya Uongozi Mbovu wa Mwenyekiti wa Chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Mar 25, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaJF,

  Watu wengi nilioongea nao kuhusu sakata la Shigela na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Sumaye wamesikitishwa sana na matamshi ya shigela. Wanasema kuwa bwana mdogo ameonesha utovu mkubwa wa nidhamu. Ongea yake ya jeuri inaonesha kuwa kuna mamlaka inayompa nguvu na kwa maoni ya wengi wanasema nguvu hiyo ni mwenyekiti wa chama. Kwa maneno mengine, tabia ya shigela ni matunda ya uongozi mbovu wa mwenyekiti wa chama.

  Siju wengine mnasemaje?
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  FREDDY SUMAYE HEBU WAPELEKE NA HAWA HUKO ULIKOSOMA MAJUZI NAO WAPATE KUBADILIKA NDIPO URUDI TUKAJADILI WEWE KUTAMANI KUWA RAIS WANGU

  Kwa watu makini, hata bila kumona uso kwa uso huyu aliyekua Fundi Mitrekta Freddy Sumaye aliyeishi siasa zetu chafu hapo kipindi cha nyuma na ukachukua wala dakika chache kumlinganisha na Mheshimiwa Fredrick Sumaye tuliemsoma moja kwa moja akiripotiwa na Invisible kwenye Press Conference aliyojiitishia pale Courtyard Hotel basi bila shaka utagundua kwamba kweli darasa bila DESA imetusaidia kwa kiasi kikubwa kupangusa uzuri kopo ambalo sie wengine tulishalitupa kwenye jalala la kule Vigunguti na sasa lafaa kuchotea tena maji ya kunywa kumpelekea mgeni rasmi (wapigakura) sebuleni!!

  Kwa msingu huo nilitamani hata naye huyu Fisadi wa Kimaasai tukimpeleka tu shule huko ma-Ughaibuni mbona hizi siasa za fitina fitina na kutembeza senti tano mitaani ataziacha tu!!

  Ila hili lingine ambalo akimuingiza mtu kwenye BLACK BOOK yake basi mpaki kifo ndicho kije kuwapatanisha nasema hata tungempeleka shule za kule nchi ya ya Mzee Shaaban Robert (Kusadikika) wala huo ukoko wa sias za Chuki, Visasi, Vinyongo, Umimi, Upwani, na mambo mengine kama hayo kamwe hayawezi kumtoka.

  Shule hutakasha bwana usiombe; hebu muone yule Fundi Mekanika wa mitrekta aliyesome SUA, Freddy Sumaye, leo hii MBA ya ukweli ilivyompiga jiki kichwa na kuondoa yale mi-oili chafu yote ya mitrekta mbovu; hata anapozungumza siku hizi mtu unaweza ukapata cha kwenda kumsimulia mtu wa pili na wala hana tena ile LUGHA YA MAFUNDI tuliokua tumzoea nayo huko nyuma.

  Mhe Sumaye, japo kwenye mahesabu yetu ya kuwa rais wa nchi hii na wewe wala haumo lakini hebu chonde mfanyie mpango huyu ndugu Eddu wa Monduli naye aende huko ulikoenda kula Kitabu walau akabadilike. Maana, kwa kusema ukweli, mtu ukimtazama kwa karibu Ndugu Lowasa, Mrema Augustino, Rostam Aziz, Seif Shariff Hamad, Nchimbi, Malisa, Ridhiwani Kikwete, Makamba Junior, Hussein Mwinyi, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe ... na wengine wengi tu hapa nchini na kweli kabisa utakuta ni watu wenye uwezo mkubwa sana tu ambao taifa letu limebahatika kuwapata isipokua tu wanakosa sana kati ya mambo haya matatu:

  (1) PERSONAL ETHICS AND LEADERSHIP INTEGRITY

  (2) SOUND EDUCATION BACKGROUND, VISIONARY & READINESS TO LEARN AT ALL TIMES, and

  (3) EXPOSURE FAR BEYOND THEIR OWN NEIGHBOURHOODS

  Hivyo nasema hapa kwamba laiti viongozi wetu wangelikua ni watu wa kukosolewa wakakosoleka, wasikivu na wenye kujitathmini wenye tu japo hata mara moja katika ngazi ya nafsi yake mwenyewe, basi ni kwamba mtu utagundua kuna mikasoro ya kufanyia kazi. Lakini pale ambapo mwanasiasa ni ni Mbumbumbu (hata kama kapata vijidarasa vichache tena kwa KUDESA TU OPEN UNIVERSITY pale Kinondoni) na kwamba hana habari kama kweli yeye ni mbumbumbu, na kwamba bado yuko tayari hata kutafuta umbumbumbu wake huo kwa kutumia VIJISENTI MITAANI ili umbumbumbu wake huo uonekane kwamba ina mng'ao sawa tu na Almasi zetu toka kule Mwadui, basi hadi hapo ndipo taifa zima mjue kwamba tunalo MZIGO MKUBWA SANA TENA GUNIA LA MISUMARI YA MOTO kuubeba wakati wote mgongoni.

  Ningeendelea sana kuomba Shule alikoenda yule Fundi Sumaye na lugha / fikra za kwenye mi-gereji tu kichwani hadi leo hii karudi nyumbali mtu ambaye si lazima akutangazie kama kaongeza darasa bali kwa nidhamu tu ya lugha yake, direction thabiti kwenye maelezo yake (japo mie sijayanunua bado) na kwenda kwa stepu bila uswahili na fitina mingi ni dalili tosha kwamba kweli mwenzetu huyu kapata shule BILA KU-DESA na kwamba shule hiyo hakika imemkomboa hivi sasa!!

  Jamani kiongozi wa ngazi yoyote akiwa na walau sifa hizo tatu hapo juu basi kazi huwa ni nyepesi mno lakini the vice versa ni kiama. Ndio maana wataalam wetu wote wanaofanya kazi chini ya madiwani katika jiji, manispaa na halmashauri mbalimbali nchini KIKUKWELI NAWAHESHIMU MNO maana mazingira yao ya kazi ni ngumu kupita kiasi kwa sababu mabosi wao ambao ni madiwani waliowengi ni watu ambao ni MBUMBUMBUMBU WA KUDUMU KWA KUJICHAGULIA!!!

  Na wala usiniulize kwa nini Mambumbumbu wa jiji la Dar es Salaam nao waliona kero sana baada ya CCM nacho kuligundua tatizo hili ninalolizungumzia na kuamua kuwaletea diwani PhD Masaburi na watu tukasikia in a chorus mambumbumbu wa jiji wakigoma kabisa kumkaribisha huyu mtu aliyeona mwanga, kusafiri sana ila kama anayo personal ethics na leadership integrity bado nasubiri kwa hamu kuona PRACTICAL RESULTS jijini na wala si mi-ripoti mizuri mizuri na takwimu yasio na maana yalioandaliwa kwa utaalam mkuba.

  Mhe Sumaye, wahimize wanasiasa waende shule zisizoendekeza KUDESA, WACHANJE MBUGA MBALI NA VIJIJI WALIKOZALIWA ILI WAJUE KWAMBA KUMBE KWINGINEKO KUNA MPISHI MZURI ZAIDI AMBAYE WAZAZI WETU WANGEENDA NAO KUJIFUNZA. Chonde wasaidie maana katika hizo points tatu hapo juu viongozi wetu wamegawanyika katika mix ambazo ni so interesting.

  Kwa mfano, na ninasema kwa nia njema kabisa, Zitto Kabwe anayo good education background bila DESA ila hana personal ethics wala leadership integrity.

  Mheshimiwa Lowassa anayo very UNIQUE IN-BORN TALENT of both Social and Business Enterpreneurial Mind lakini hajaruhusu ikapigwa msasa hii talanta imekua naexcesses nyingi mno katika jamii. Jambo ambalo linatushawishi ku-question his genuine education background so far, na his personal ethics and leadership integrity is REALY WANTING.

  Mheshimiwa Mrema ni mtu mmoja ambaye otherwise ni LULU KWA TAIFA LETU. Watu wa aina yake huwa hawazaliwi wengi sana ndani ya kipindi kifupi. Watu wa aina yake ambao nao ni lulu ni akina Mwalimu Nyerere, Dr Ali Mohamed Shein, Salim Ahmed Salim, Everist Kaigaruki, Magufuli, Moringe Sokoine, Mama Nkya ... lakini a mark of an UNTRACEABLE SOUND EDUCATION background inamuangusha sana ila Personal Ethics ni Average na Leadership Integrity imesimama mpake arudi kwa muumba wake.

  Julius Mtatiro anayo personal ethics and leadership integrity ya hali ya juu (hata kama bado hajajaliwa fedha wala haonyesha uharaka wa kuzikimbilia), huyu bwana kwa UDSM pale wenzake waliosoma naye wanamheshimu kitaaluma ila dosari yake kubwa ni kwamba hajui lolote zaidi ya mipaka ya Tanzania basi!!

  Mhe Sumaye wasaidie wenzio waenda NDANI YA DARASA ulikoenda wewe (japo swala la wewe kuwa rais wangu tutaujadili siku nyingine) ili wakome kuwa miziko yetu kifikra na matendo yao!!!

  [​IMG] Originally Posted by Ntemi Kazwile [​IMG]
  Dah kumbe shule nzuri bwana, tangu amalize MBA yake siku hizi Sumaye anaongea point, nimeshitushwa kidogo maana nilizoea kumsikia akitoa point zilizokuwa tata sana enzi za uwaziri mkuu wake.

  Hongera Sumaye
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hilo dude lako mbona una weka kila sehemu sasa?
  Afu hamna anae lisoma unachosha watu tu!
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Like a father like children!
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dogo kaonesha kukosa busara sana. Hajui namna ya kujibu siasa.
   
 6. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  True, huyo bwana mdogo ana back-up ya kikwete. Hawezi kuongea "utumbo" huo bila kuachwa.
   
 7. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu umenena tukirudi nyuma Hawa jamaa wanataka kupotesha mila na desturi za afrika so, kijana kuwa na majibu kama yale na isitoshe kwanza ni mkuwa kwa ki umri hata kimadaraka na si yeye tu hata kina sita so inakuwa je hawa wanowatuma watoto kuwakashfu wazee je wanawafundisha nini? kwanza tuachane na siasa or vyama embu tuwanyooshe vidole hawa watoto na ikiwezekana wapotezwe kabisa kwenye jamii
   
 8. m

  mwantavangale Member

  #8
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri kuna haja ya kujua m,ambo hadi tufikie kuwa shigela ana nguvu inatomsukuma nyuma,binafsi naona hayo ni mawazo mafinyi sana,shigela ana mhimili wake ambao unaongozwa na baraza kuu.chini ya mwenyekiti wake.pia ni mjumbe wa sekretarieti ta ccm na MMNEC,

  Ambapo nafikiri Mh sumaye ndio mtovu wa nidhamu kwani ameshindwa kukaa na viongozi hawa au hata kukaa kimya ili kuonesha ukomavu wa kisiasa kwa jamii.kwani anapoenda katika vyombo vya habari ndio anatatua tatizo? baba mwenye maadili hawezi kutoka nje na kuanza kushindana na wanawe barabarani ni lazima ake kitako ili aweke mambo sawa,

  kwa hiyo naomba tusiwe wafinyu wa mawazo kwa kumhusisha Mh jakaya kama mwenye kiti wa chama na malumbano ya wajumbe wa halmashauri hawa?
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Si kweli, hana back-up ya JK pamoja na kuwa ndiye aliyemteua mara ya kwanza kuwa DC na baaddae ktk Uktabu wa UVCCM..Shigela anapokea amri toka Monduli. Angalieni magazeti yote yaliyoandika bila kumtaja EL hajayakanusha na hayajafuata hilo azimio alilosema lkn kutajwa kwa EL na Raia Mwema na MwanaHalisi katoa tamko.

  Shigella anajua alikotoka, arudi polisi kujibu tuhuma za kughushi nyaraka za Ikulu kabla ya kuteuliwa kuwa DC Lindi
   
 10. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nawewe umefanya Yaleyale kwanini umefanya quatation ya kila kitu badala hata ungeedit baadhi ya Maneno kwenye hiyo Post"Mnatuchosha bhana"Kufanya scrolling ya such post mnatupotezea muda.
   
 11. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  KUNYUKANA MTINDO MMOJA.
  Nimeona vipande vya press conference ya Sumaye na Shigella akijibu.
  Ninachokiona mimi ni kuwa Sumaye ana hasira na matope aliyopakwa mwaka 2005 na wan mtandao.Aliandika maelezo yake mara na mara kwa mara alikuwa akisoma hii inaonyesha ya kuwa alikuwa anajitahidi asije akavuka mpaka.
  Shigela amedhihirisha ya kuwa suala la Uraisi ndilo chimbuko kubwa kwani ametaja hata mashamba alonunua/kuchukua Sumaye,hii ni katika kuhakisha ya kuwa hata kama Sumaye ataoga kwa sabuni gani hasafishiki.Tahadhari kwa Shigela ni kuwa kama anampigania EL ajaribu kuuliza tu kuwa katika Ranch za Taifa zilizouzwa amechukua kiasi gani?Wamepiga mawe wakiwa ndani ya nyumba ya vioo wakae standby!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...