BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,886
Tusishangae ya Jeetu Patel, wajinga ndio waliwao
Johnson Mbwambo Januari 23, 2008
Raia Mwema
MWAKA 1995 mgombea urais wa chama cha NCCR-Mageuzi, Augustine Mrema alianzisha mjadala mkubwa alipotamka, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni, kwamba haoni sababu kwa nini Wahindi wagombee nafasi za uongozi katika Tanzania.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani, mjini Dar es Salaam, Mrema aliwataka Wahindi wakagombee uongozi kwao India.
Kama alivyoshambuliwa Christopher Mtikila kwa kuwaita Wahindi Magabacholi, Mrema naye alishambuliwa kila kona na wafuasi wa CCM kwa kauli yake hiyo dhidi ya Wahindi; huku akiitwa mbaguzi mkubwa wa rangi na mtu asiyefaa kuwa Rais.
Lakini walikuwepo pia maelfu ya vijana kote nchini ambao waliwaunga mkono Mrema na Mtikila kwa misimamo yao hiyo dhidi ya Wahindi. Kwa hakika, walichokifanya Mrema na Mtikila ilikuwa ni kuamsha tu hisia za muda mrefu zilizokuwa zimelala miongoni mwa Watanzania, hususan vijana, dhidi ya Wahindi.
Vijana hao ni wale wanaoamini kwamba sio tu kuwa Wahindi wamejitenga na kujibagua kwa miaka yote tangu walipoletwa hapa Afrika Mashariki kujenga reli, lakini pia baadhi yao wamethibitisha jinsi wasivyokuwa waaminifu kwa nchi hii kwa mambo wanayoyafanya.
Achilia mbali kwamba wengi wao wameendelea kuwa na uraia wa nchi mbili, baadhi wamejitokeza kuwa wahujumu wakubwa wa uchumi; huku wakiwavuta kama sumaku watawala wetu wenye tamaa ya kuishi maisha ya ubilionea na kuwashawishi kushirikiana nao katika vitendo vya ufisadi vya kuwaibia wanyonge wa nchi hii pesa zao.
Ni kweli kwamba katika dunia ya sasa huwezi kuwa na mtazamo mkali (wa kibaguzi) dhidi ya Wahindi, Waarabu, au hata Wazungu, ukafika mbali kisiasa; na hivyo Mrema na Mtikila nao hawakufika mbali kisiasa.
Lakini swali la kujiuliza ni hili: Je, hisia zile za vijana dhidi ya Wahindi, zilizoamshwa na kina Mtikila na Mrema katika miaka ile ya tisini, zimekufa moja kwa moja au zimelala tu zikisubiri mtu mwingine wa kuziamsha, au kitu kingine cha kuziamsha?
Majuzi nilikuwa katika baa moja maarufu hapa Jijini Dar es Salaam ambako niliweza kusikiliza mjadala mkali wa kikundi kidogo cha wanywaji kuhusu kashfa ya ufisadi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Ingawa wafanyabiashara wanaotuhumiwa na ufisadi huo ni wengi, ilikuwa ni dhahiri katika mjadala wa kikundi kile kuwa hasira zao zilielekezwa zaidi kwa mmojawao ambaye ni Mhindi Jayantkumar Chandubhai Patel, maarufu kwa jina la Jeetu Patel na mwingine ambaye sina hakika kama ni Mhindi au burushi.
Nilijiuliza kwa nini hasira za kikundi kile zisielekezwe kwa Daudi Ballali ambaye ndiye aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu wakati pesa hizo zikichotwa? Kwa nini hasira zisielekezwe kwa watuhumiwa wengine wasio Wahindi, au hata kwa Daniel Yona na Basil Mramba, waliokuwa Mawaziri wa Fedha au Benjamin Mkapa aliyekuwa Rais wakati mapesa hayo yakichotwa Benki Kuu? Kwa nini hasira zielekezwe kwa Jeetu Patel tu na wengine wasio wazawa?
Lakini ni kweli kwamba Jeetu Patel peke yake anamiliki kampuni nane kati ya 13 zilizotajwa katika taarifa ya Ernest & Young kuwa zililipwa Sh. bilioni 90.3 za akaunti ya EPA ya Benki Kuu kwa kutumia nyaraka batili na zilizoghushiwa.
Ni kweli vilevile kwamba unapozungumzia rushwa kubwa kubwa au ujambazi wa kiuchumi hapa Afrika Mashariki, majina yanayojitokeza ni ya Wahindi. Ukifikiria majina kama Chavda, Akasha, Pattni, Sailesh Vithlani au Tanil Somaiya, utaelewa ninachokizungumzia kuhusu baadhi ya Wahindi tulionao Afrika Mashariki.
Na jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba wote hao wana uraia wa nchi mbili au nne hivi. Mbali ya uraia wa Tanzania unakuta pia kuwa ni raia wa Uingereza, India, Canada, Marekani au Australia. Ukimuuliza kati ya nchi zote hizo ambazo yeye ni raia, mapenzi yake ya dhati yako kwa nchi gani, hatakujibu.
Kwa hiyo, naielewa hasira ya kikundi kile cha wanywaji dhidi ya kina Jeetu Patel. Wenzetu hawa Wahindi (ingawa wapo wengine waaminifu na wazalendo kweli kweli) wamekuwa wanaishi Tanzania kama sehemu ya kuchuma tu mali na mahali pa kuishi pa muda tu wakati wanajiandaa kwenda mahali pa kudumu pawe Uingereza, Canada au Marekani.
Hata baadhi ya wale ambao kwa vipindi tofauti wamejiita Watanzania au makada wa CCM na hata kuvishwa majoho ya ukamanda wa vijana wa chama hicho, baadaye walibadilika na kuondoka nchini baada ya kuwa wameona wamenufaika vya kutosha kwa kuupata utajiri hapa nyumbani, mara nyingi kwa njia zisizo halali. Wako wapi, hivi sasa, kwa mfano, kina Chavda na kina Gulamani?
Kwa ufupi, mienendo yao wenyewe (Wahindi) ndiyo inayofanya hisia zile zilizoamshwa na kina Mtikila na kina Mrema, miaka ile ya tisini, zisife kabisa miongoni mwa Watanzania wazawa, hususan vijana. Kwa hakika, baadhi ya Wahindi wamefikia hata hatua ya kuingiza ubaguzi wa rangi katika ajira.
Hebu soma tangazo hili lililotoka, wiki iliyopita, kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti la Majira (toleo la Januari 18, 2008):
Urgently Required: Sales person male/female for a pharmacy at Shoppers Plaza. Should be: Form 1V/V educated. Fluent in English. Tanzanian of Asian Origin. Please contact 0754-673586.
Kwa tangazo hilo, mzawa hawezi kupata ajira hiyo hata kama ana sifa zote, kwa sababu anayetakiwa ni Tanzanian of Asian Origin; yaani Mhindi!
Binafsi, naamini kwamba wakati mwingine ni Wahindi wenyewe wanaojiponza. Laiti wangebadilika na kuifanya Tanzania ni nchi yao kweli kweli, na kuacha kuwahujumu wanyonge wa nchi hii, nina hakika fikra hizo zingekufa kabisa na kuzikwa, lakini kama nilivyoshuhudia katika gumzo lile la wanywaji kwenye baa, bado hazijafa kabisa!
Na wala sisemi jibu lipo katika kuwafukuza. Ukiachilia mbali ukweli kwamba kufanya hivyo ni kukiuka haki za binadamu, lakini Wahindi pia ni nguvu kuu ya uchumi hapa nchini; achilia mbali kwamba wanaajiri ndugu zetu wengi tu kuanzia majumbani mwao, madukani mwao, maofisini mwao na viwandani mwao.
Kwa mtazamo wangu, jibu lipo sehemu mbili. Kwanza, jibu lipo kwa Wahindi wenyewe. Ni lazima wenyewe, kama jumuiya, wabadilike kama kweli wanataka hisia hizo za baadhi ya Watanzania dhidi yao zife na kuzikwa.
Ni mabadiliko gani ninayoyazungumzia? Yapo mengi, lakini kubwa ni kufanya juhudi za kweli ku-integrate na Waafrika (wazawa). Ku-integrate kuna maana pana, lakini hebu chukulia mfano mmoja tu wa ndoa. Haiwezekani kwamba hawa jamaa wamekaa nchini mwetu miaka yote hiyo, na bado tusione idadi ya kutosha ya Wahindi waliooa/kuolewa na Waafrika au Waafrika waliooa/kuolewa na Wahindi.
Ni rahisi hapa nchini kuona machotara wa Kiarabu na Kiafrika (nina maana ya Watanzania weusi) au wa Kizungu na Kiafrika kuliko kuona machotara wa Kihindi na Kiafrika au hata wa Kihindi na Kizungu au Kihindi na Kiarabu.
Kuna imani kwamba binti wa Kihindi au kijana wa kiume wa Kihindi, akizaa mtoto na moja ya makundi hayo niliyoyataja, hutengwa na jamii. Waliopata kuiangalia filamu ya Mississippi Masala (Denzel Washington) wanalielewa hili vizuri.
Kwa hiyo, Wahindi lazima wajisaidie kwanza wao wenyewe kumaliza hisia hizo za chuki dhidi yao ambazo baadhi ya Watanzania wanazo. Na moja ya njia za kujisaidia ni kuanza ku-integrate na Watanzania weusi katika nyanja zote. Mpaka sasa integration tunayoiona ipo kidogo katika siasa na katika michezo, na hiyo, ukichunguza, ni kwa manufaa binafsi ya hao wachache waliojitosa humo.
Sambamba na hilo, Wahindi ambao ni raia wema na wanaoipenda nchi hii kwa dhati (wapo wengi wa kutosha), lazima nao wachukue hatua za makusudi kabisa za kuwasema wenzao wanaohujumu uchumi wa nchi hii masikini ili waache kuwaibia wanyonge pesa zao.
Maana, ni kweli wanatuibia. Pesa zinazoaminika kuibwa na kampuni za Jeetu Patel na zile za skandali ya Chavda na ya ununuzi wa rada inayomhusisha Sailesh Vithlan, tunaambiwa, zinatosha kujenga zaidi ya shule 1000, na bado walalahoi nchini wanachangishwa na Serikali kwa nguvu pesa za kujenga sekondari!
Hivyo, Wahindi ambao ni raia wema wanaweza kutumia jamatini zao na misikiti yao au jumuiya zao nyingine kuwaweka kiti moto kina Jeetu Patel na kina Chavda na kuwaambia kwamba wanachokifanya si kitu chema mbele ya Mungu, na kwamba kinawafanya wao (Wahindi) wachukiwe na wazawa. Hili, naamini linawezekana na likifanyika litapunguza kuibuka kwa wingi nchini kwa kina Jeetu Patel, Chavda, Sailesh na kina Pattni.
Lakini jibu la pili ambalo ndilo la msingi, ni kwa sisi wazawa (Watanzania weusi) kutokubali kuwapa uongozi wazawa wenzetu wenye tamaa ya kupindukia ya kuwa mabilionea. Hawa, huwa rahisi kugeuzwa wajinga na kina Jeetu Patel. Viongozi wetu wakishageuzwa wajinga na kina Jeetu Patel na kina Chavda, basi, sisi sote katika ujumla wetu, tunakuwa wajinga wa wenzetu hao!
Nasema hivyo, kwa sababu Jeetu Patel asingeweza kufanikisha kuunda kampuni sita kwa nyaraka za kugushi, moja baada ya nyingine, na kila moja kujichotea mapesa hayo BoT, bila kushirikisha viongozi na watawala wetu (ambao wote ni wazawa) wenye uchu mkubwa wa kuwa mabilionea.
Alichotumia Jeetu Patel, Chavda, Sailesh na wengine kadhaa, ni udhaifu wetu sisi Watanzania kuchagua viongozi na watawala wasiojali miiko ya uongozi, viongozi ambao lengo lao kubwa kuingia madarakani si kutumikia wananchi na kuwapunguzia umasikini, bali ni kuusaka utajiri kwa udi na uvumba. Hao ndiyo wanaotufanya Watanzania wote tuonekane ni wajinga tu mbele ya kina Chavda.
Hao ndiyo wanaowakubali na kuwaamini kina Chavda na maburushi wengine kuwa ni wafadhili wa Chama huku ufadhili wenyewe ukitokana na pesa walizotuibia. Mtu anakuibia kijanja mapesa yote hayo katika benki ya umma, na kisha kesho akijenga kisima kwa ajili ya kijiji fulani, au shule ya sekondari au akitoa pesa kidogo kusaidia Chama, tunachekelea kwa furaha huku tukimwita mfadhili mkubwa wa Chama na mzalendo wa kweli!
Anayekuibia kwa kutumia mkono wa kulia na kukurejeshea kidogo alichokuibia kwa kutumia mkono wa kushoto; huku akijitia ni mfadhili, utamwitaje mzalendo wa kweli? Huyu mahali pake ni jela!
Hivi sasa naambiwa kwamba, kama ilivyokuwa kwa Chavda, Sailesh na Gulamani, Jeetu Patel naye hayupo nchini katika kipindi hiki ambacho kashfa ya ufisadi ya BoT inachunguzwa ili wahusika wakamatwe.
Popote pale walipo huko nje, nina hakika kina Jeetu Patel, kina Chavda na kina Sailesh, watakuwa wakicheka njia nzima wakati wakienda benki (Swiss Bank?) kuchukua mapesa waliyochota kwetu, mapesa ya Watanzania masikini.
John Nolan, yule mwekezaji wa Ireland aliyataka kuighilibu Serikali ya Mkapa imruhusu kufungua mashamba ya prawns ambayo yangeiharibu kabisa Delta ya Rufiji, alipata kusema kwamba; Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Mzungu, Mhindi au Burushi anaweza kuingia akiwa na dola tano tu mfukoni na kuondoka miaka mitano baadaye akiwa milionea! Kweli wajinga ndiyo waliwao!
Email: mbwambojohnson@yahoo.com