Tusipotoshe umma, Tanzania ni Nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi, sio lazima Wapinzani kuchaguliwa kuwa Wabunge

Bora mimi sikuchagua binadamu asiye na tone la huruma ingawa ni mkatoliki anayesali sala ya baba yetu inayomuomba Mungu atusamehe makosa yetu Kama na sisi tunavyo wasamehe wale walio tukosea.Tukiikataa sauti ya wengi twaikataa sauti ya Mungu,Tukijichagua ilhali Mungu hajatuchagua basi tujue tunakwenda kuharibu vitu vingi Sana ambavyo vitawaathiri Watanzania wote bila kubagua chama chochote.Kundi Dogo la wapumbavu linasahau hicho.Fikiria mazingira ya Mbunge ambaye amekerekwa na utendaji mbovu atawasilishaje hoja zake katika mazingira ya kibabe Kama haya.CCM mjue mmemuibia Mungu na hamtabaki salama mtajitafuna wenyewe kwa wenyewe ndicho kifuatacho amini usiamini time will tell.
 
"Mkichagua upinzani sitawaletea maendeleo"!

"Nikulipe mshahara halafu utangaze mpinzani kashinda"!

Kauli hizo hazijawahi kutolewa na kiongozi yeyote anayeheshimu misingi ya kidemokrasia!

Wananchi wanapaswa kuwa huru kuchagua! Na sio kutishwa kama ilivyotokea!

Mfumo wa Tanzania bado hautoi fursa kwa demokrasia kuchukua mkondo wake!

Sasa angalia ni kamata kamata ya wapinzani ndiko kunakoendelea!

Kwani upinzani mlifungwa midomo kutoa ahadi zenu.. si nanyi mngesema hayo hayo kama wao.. simnajijua mulivyo geza geza..

Mgombea wenu kapata aliyopata.. musherekee.. wabunge waliotanguliza pinga pinga.. tumewapumzisha.. bora wa CCM.. tunajua watasimamiwa vyema..

Miaka nenda rudi.. wengine tumeona upinzani wa TZ.. hauvutii kabisaaaa..

Pongezi kwa 💚💛💚💛💚
 
Kwa Coronavirus pia,
Magufuli aongeze hata miaka kwa kweli alitenda jema. Nchi nyingi bado zinateseka nayo
 
Kwani upinzani mlifungwa midomo kutoa ahadi zenu.. si nanyi mngesema hayo hayo kama wao.. simnajijua mulivyo geza geza..

Mgombea wenu kapata aliyopata.. musherekee.. wabunge waliotanguliza pinga pinga.. tumewapumzisha.. bora wa CCM.. tunajua watasimamiwa vyema..

Miaka nenda rudi.. wengine tumeona upinzani wa TZ.. hauvutii kabisaaaa..

Pongezi kwa 💚💛💚💛💚
Wala hakuna shida,maisha yanaendelea na serikali ndiyo hiyo mmechukua CCM kuanzia mitaa,madiwani,wabunge hadi Rais!
Hakuna tena ile kusema tulishindwa kuleta maendeleo sababu mlichagua upinzani!
Natabiri awamu hii ndiyo itakuwa hovyo zaidi kuliko iliyotangulia!
 
Hakuna nchi watu wavivu wanajiletea maendeleo yao kwanza.. wenyewe.. kuna vitambulisho vya 20K.. baada ya muda.. mtu unadili na TRA.. acheni kulalamika.. inajulikana tulitaka Rais kama JPM.. tumpe nafasi apumue.. afanye mazuri mengine tunayoyaona..

Ovyo na iwe kwako.. muache kufikiria pesa za mikato za bure.. maisha lazima muntu kusukuma mwenyewe..
 
Relevance!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hoja ni uchaguzi haramu uliogubikwa na unajisi wa Demokrasia, uibaji wa kura, kura feki, kubadilisha matokeo, kuwazuia mawakala na ushenzi mwingi wa aina hii. Hoja sio wapinzani wangapi wamechaguliwa.
 
Wapinzani hawalalamikii idadi ya wabunge...wanalalamikakia zoei la uchaguzi.....
Mimi sio mpinzani lakini kama kuna namna wanaona haikuwa sawa, wasikilizwe...
Kuanzisha mada kama hizi unatakiwa ueleze upande wako wa kisiasa ili ueleweke vizuri..
Kivipi?
 
"Mkichagua upinzani sitawaletea maendeleo"!

"Nikulipe mshahara halafu utangaze mpinzani kashinda"!

Kauli hizo hazijawahi kutolewa na kiongozi yeyote anayeheshimu misingi ya kidemokrasia!

Wananchi wanapaswa kuwa huru kuchagua! Na sio kutishwa kama ilivyotokea!

Mfumo wa Tanzania bado hautoi fursa kwa demokrasia kuchukua mkondo wake!

Sasa angalia ni kamata kamata ya wapinzani ndiko kunakoendelea!
Demokrasia ipo, watanzania wamejifunza kutochagua utopolo.
 
Hoja ni uchaguzi haramu uliogubikwa na unajisi wa demokrasia, uibaji wa kura, kura feki, kubadilisha matokeo, kuwazuia mawakala, na ushenzi mwingi wa aina hii. Hoja sio wapinzani wangapi wamechaguliwa.
Baada ya wananchi kuchagua CCM na CHADEMA kukosa wabunge ndio ndio mnaleta hoja za kuibiwa kura wakati mlikuwa na mawakala.
 
Nimekuuliza maswali kadhaa hapo juu hujajibu hata moja.Mimi siyo mpenzi wa porojo,kama wewe ni muumini wa porojo kaa mbali kabisa na mimi.Narudia tena kukuuliza,nani kasema kuwa uchaguzi huu una kasoro kwa sababu ya chadema kukosa ubunge?Au umejitungia tu kauli hii ili kujifurahisha wewe pamoja na nafsi yako?Una reference ya kiongozi yoyote wa chadema ambae ametoa kauli ya kikhanithi kama hii?Hii dhana ya kikhanithi umeitoa wapi?
Porojo au unaambiwa ukweli? Kwani mtu hawezi kutoa kauli impliedly? Au sababu wewe ni mburula huna akili ndio unadhani kila mtu ni mburula.
 
Back
Top Bottom