Tusipotoshane, kulikuwa na sababu za msingi kabisa kwanini Marais waliopita hawakununua ndege kama awamu hii ya tano ilivyofanya

Ununue ndege wakati raia wako taabani Kiuchumi njaa, maji, malazi, mavazi, ajira, biashara hakuna. Watu wako taabani Kiuchumi, wanakunywa matope wewe unanunua ndege kisa teni pasenti.
 
Huwa nachukia sana ninaposikiliza viongozi wetu wakitumia cheap propaganda na kutamba juu ya mafanikio yao kwa kujilinganisha na viongozi waliopita. Kwa mfano, mara kadhaa nimesikia tamko kwamba awamu zilizopita hawakuweza kununua ndege kama awamu ya sasa.

Watu wanaoeneza hizi propaganda huwa hata hawashughulishi ubongo wao kwa kujiuliza kwa nini awamu zilizopita hawakununua ndege kama awamu hii ya tano. Wanasahau kuwa hali za sasa na wakati ule ni tofauti kabisa na kwamba kila raisi anakuwa na vipao mbele vyake, hivyo huwezi kufanya huo ulinganifu.

Tumchukulie Nyerere kwa mfano. Kumbuka wakati fulani, kulikuwa na wimbi la kuanzishwa vituo vya television. Nyerere alipopewa pendekezo la kuanzisha television ya taifa alikataa. Akasema, kwanza ni nani watakaokuwa na uwezo wa kununua television nchini, hawa wakulima na wafanya kazi wetu? Pili akauliza, hizo gharama za kuendesha television ya taifa, tutazimudu vipi pamoja na kuhakikisha inapatikana nchini kote ikiwa radio tu inatupa shida kuna sehemu za nchi inasikika kwa taabu? Kisha akamalizia kwa kusema kuwa na television ya taifa kwa wakati huo hakukuwa jambo la msingi la kupewa kipao mbele, lakini itafika wakati muafaka wa kuwa na television ya taifa. Zanzibar wao walisema wangeanzisha, wakidai gharama yao isingekuwa kubwa kutokana na udogo wa kisiwa.

Sasa fast forward. Katika hali yetu hii ya sasa, fikiria Mwalimu Nyerere ndiye angekuwa Rais wa Tanzania, halafu unatoa pendekezo kwamba Tanzania tununue Dreamliner, Airbus na Bombardier, kwa kuwa fedha za walipa kodi zipo za kuweza kununua ndege hizo. Kumbuka ni Nyerere yule ambae alikuwa akisema ushindani wa kibiashara na mataifa makubwa ni mgumu sana, watatumia kila mbinu kukufanya usifanikiwe na wewe kwa umasikini wako utakuwa huna la kufanya. Hata aliwahi kuuliza, hivi mnafikrir benki yetu ya Taifa NBC inaweza kwenda Uingereza na kufungua tawi pale London ikafanikiwa kirahisi tu? Lakini wao wakitaka kuja kwetu, kwanza wanakupa masharti, ivunje NBC vipande vipande kwanza ili tushindane nayo!

Ni Nyerere huyo huyo, miaka ya 1983 - 85 dhahabu ya Bulyanhulu lipogunduliwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni za Outo Kumpu na Kone Corp aliwakatalia kugawana faida kwa 49% Tanzania na wao 51% akawaambia Tanzania iwe na 51% na wao 49%. Walipokataa akawaambia kama hawataki waondoke, akisema iacheni hiyo dhahabu ikae huko shimoni, kwani itaoza? Akasema wazi wakati muafaka ukifika tutaichimba hiyo dhahabu, hata kama ni vizazi vyetu vijavyo. (Kwa kusikitisha baadae Mkapa alikubali 5%, wala sio ile 49% aliyokataa Nyerere ili tupewe 51%).

Sasa tumia akili zako na za kuambiwa kutambua Nyerere angekupa jibu gani; sawa tukanunue ndege, au hapana si wakati muafaka?

Kwa hiyo kabla ya kufanya hizi cheap propaganda kuwa viongozi huko nyuma hawakununua ndege kama awamu hii, tujiulize kwanza kama hao viongozi wa huko nyuma wangekuwa ndio maraisi leo hii wangenunua ndege au la, na kwa nini.
Hizo ndege zimenunuliwa Mara tu Awamu ya tano ilipoingia madarakani ikimaanisha kuwa hizo pesa zilikutwa zimehifadhiwa mahali. Hii ina maana ni viongozi waliopita ndo walizalisha na kuhifadhi hizo pesa kwa mahitaji muhimu ya baadaye. Mahitaji muhimu, kwa viongozi wastaafu na Mimi, haikuwa pamoja na madege ambayo yalikuwepo yakafa kwa sababu zilizopo mpaka sasa na kesho. Inachekesha viongozi wa sasa na wajinga wengine kujisifu kutumia pesa na kuwabeza waliozalisha na kuhifadhi ili wananchi wote wanufaike wakati ukifika. Matonya, mgogo, angepata pesa hiyo angeshindww kuitumia kununua ng'ombe akarudi kijijini akarudi kijijini akaachana na ombaomba? Viongozi wetu wanahamia Dodoma wakuta maziwa tele!
 
Mie naweza nisiwe na tatizo sana kuhusu Tanzania kununua ndege, ikiwa tuna mikakati madhubuti ya kujiendesha kwa faida na sio tu kutafuta sifa ya kununua Dreamliner mbili. Kinachonikera na kunishangaza ni pale ambapo tunaambiwa hawa waliopita hawakuweza kununua ndege!

Hawa waliopita walikuwa na dhamira safi kiasi kwamba wasingeweza kuvumilia kununua ndege dhidi ya vipao mbele vingine. Nyerere siku zote alikuwa anajiuliza faida na hasara ya kufanya kitu fulani - na hata kama ni faida, ni faida kwa nani, majority au minority?

Huyu Nyerere ambae aliekataa watu kununua salon cars kama Benz na BMW na kuwataka wanunue pick up, leo unaweza kudiriki kusema hakununua ndege kama awamu ya tano? Huyu ambae alisema viongozi watatumia Land-Rover 109? You have to be a psychiatric case kumfikiria Nyerere hakununua ndege kwa kuwa hakuweza kama inavyofanyika sasa. For Nyerere it was always a matter of calculated choice, not just financial capability.

waliopita walikuwa wapuuzi tu na wapiga dili,,,,hawakuwa na lengo lolote la kutaka kuendeleza nchi.
 
Kuna mamia ya mipango kaikutaRais Magufuli ikiwa imeanzishwa na Jakaya mf. ujenzi wa kuiunganisha Katavi-Tabora,Katavi-Kigoma, Katavi-Sumbawanga leo ikikamilika sifa kwa Magufuli.

Upanuzi wa uwanja wa ndege Dar, leo unauliza mimi nimenunua ndege wao walikuwa wapi? bila kuelewa kuna mamia ya miradi ilifanyika pia ambayo leo hii wewe unapata urahisi wa kufanya mradi 1 maana mingine ishafanywa
Kwa mfano, asingetimiza hayo yalioanzishwa. Ingekuaje?
 
Watanzania hawajaenda shule. Reasoning kwao ni mtihani.

Ndio maana kila ujinga unasemwa majukwaani na watu wanajichekesha tu.

Miaka nenda rudi mnasoma vitabu kama cha Walter Rodney cha How Europe Underdeveloped Africa. Wakati waafrika wenyewe kwa wenyewe mnanyimana maendeleo.

Unanunua ndege wakati barabara zimekatika watu wamelala njiani, kuna sehemu watu hawana maji safi na salama, elimu duni, afya ndo hohehae.

Hata hao wanaotengeneza hizo ndege hawafanyi hiyo biashara moja kwa moja. Either wananunua hisa kidogo au waachia sekta binafsi ihusike na risk zote wao wanabaki kama regulators.

Usimlaumu beberu kwa ujinga wako wa kukosa maendeleo manake hata Australia, Singapore, Japan, Brazil walitawaliwa kama nyie ila wao wakawa na vipaumbele vinavyomake sense. Wakafika hapo walipo.

Wanasema afrika ni kama jungle. Mnaishi kama wanyama.
Wewe uliyekwenda shule unaganga njaa hapa JF, kichekesho cha mwaka.
 
Budget yaki hata bila kununua ndege haitoshi kufanya yote hayo.

Kujikwamua na misaada tunafanya ujasiliamali wa ndege.

Watz wengi tunajali kula kuliko investing
Kununua madawati ni kula ? kununua dawa na vifaa vya hospitali ni kula ? kuwapa wanafunzi wa elimu ya juu wasio na uwezo wa kujilipia ada na gharama za masomo ni kula? Tunatengeneza nchi ya namna gani?
 
kula kwa maana haizalishi (spending/consuming).

Logic ni kwamba ukimaliza kufanya hayo na huna source nyingine ya income unafanyaje?
Ama TRA kukamua zaidi mtaani?

Kupata hayo uliyoyataja we need to have chanzo cha pesa. Ndio business concept.

Unahisi umetaja vitu muhimu Yes ila budget yetu ni asilimia ngapi kwa maana ya mapato ya ndani?

Busara inaonesha before hujawaza kula kwa mahitaji hayo muhimu waza vikiisha what next? wafadhili?

tunatengeneza nchi ya namna gani jibu tusipowekeza tunatengeneza nchi ya ombaomba kwa wafadhili.

Yet kama priority hospitali zinajengwa na elimu bure na mikopo etc.

Thanks kwa wachumi wetu kwa kuwaza vyote at the sametime. Kula kwa kujibana na kuwekeza.

Labda nikuulize wewe unajenga taifa gani lenye kutoa huduma za muhimu bila kuwa na sources za kipato?

Hata hivyo ntazidi kuluheshimu kama great thinker

Soma vizuri dhana ya maendeleo na indicators zake, no a single developed country iliignore kwanza maendeleo ya wananchi wake na kwenda kuinvest kwenye manunuzi ya ndege ambayo kimsingi zinajiendesha kihasara ., maendeleo yana stages na yanaanza stage ya chini kabisa ngazi ya an individual, family level na kuendelea .. tukiweza kusomesha vijana wetu vizuri , wamama wajawazito wakajifungua hospitali zenye vifaa, access to clean water na vitu vingine muhimu ndipo tutakuja kuachieve maendeleo.. usimlazimishe mtoto anaetambaa kutembea utamuumiza tu.
 
hauoni hayo yanafanyika?
Ama family level kila nyumba igawiwe kilo za sembe?
ama ni siasa za kukosoa ndege?

Ndege zinaendeshwa kwa hasara unaelewa? ama full of ukinzani?

Hasara inapungua kuelekea Break Even Point.

Ujinga ni kwamba kila zuzu anajifanya mchumi..
Soma vizuri dhana ya maendeleo na indicators zake, no a single developed country iliignore kwanza maendeleo ya wananchi wake na kwenda kuinvest kwenye manunuzi ya ndege ambayo kimsingi zinajiendesha kihasara ., maendeleo yana stages na yanaanza stage ya chini kabisa ngazi ya an individual, family level na kuendelea .. tukiweza kusomesha vijana wetu vizuri , wamama wajawazito wakajifungua hospitali zenye vifaa, access to clean water na vitu vingine muhimu ndipo tutakuja kuachieve maendeleo.. usimlazimishe mtoto anaetambaa kutembea utamuumiza tu.
 
Elimu bure inatolewa na hospitali zinajengwa..
maendeleo ya individual.. kapangeni mistari kwa mtendaji wa kata kila individual apewe kiloba cha unga..

Kapumzikeni
Soma vizuri dhana ya maendeleo na indicators zake, no a single developed country iliignore kwanza maendeleo ya wananchi wake na kwenda kuinvest kwenye manunuzi ya ndege ambayo kimsingi zinajiendesha kihasara ., maendeleo yana stages na yanaanza stage ya chini kabisa ngazi ya an individual, family level na kuendelea .. tukiweza kusomesha vijana wetu vizuri , wamama wajawazito wakajifungua hospitali zenye vifaa, access to clean water na vitu vingine muhimu ndipo tutakuja kuachieve maendeleo.. usimlazimishe mtoto anaetambaa kutembea utamuumiza tu.
 
tunatengeneza nchi ya namna gani jibu tusipowekeza tunatengeneza nchi ya ombaomba kwa wafadhili.

Yet kama priority hospitali zinajengwa na elimu bure na mikopo etc.

Thanks kwa wachumi wetu kwa kuwaza vyote at the sametime. Kula kwa kujibana na kuwekeza.

Labda nikuulize wewe unajenga taifa gani lenye kutoa huduma za muhimu bila kuwa na sources za kipato?

Hata hivyo ntazidi kuluheshimu kama great thinker
emoji3.png
BTW kupeleka watoto shule wapate elimu
Elimu bure inatolewa na hospitali zinajengwa..
maendeleo ya individual.. kapangeni mistari kwa mtendaji wa kata kila individual apewe kiloba cha unga..

Kapumzikeni
You mean elimu bure not only in delivery but also content? hio ya watoto kukaa kwenye vumbi au kusomea chini ya miti? hebu take your time upite shule hasa za rural areas uone hali ilivyo., kwa hio kupewa kiloba cha unga ndio maendeleo to you? LOL
 
zilitakiwa zifanane na marekani ama?
one step at a time.

Serikali inafanya both... toa huduma na kuwekeza/invest.. koz ubora wa shule na elimu na hospitali inahitajika pesa.

Kwa miaka kibao tulimudu only 50% ya budget... Then we doing something to improve it.

Ni kama mnataka tubaki tulipo milele bila kusogea kwa ngonjera za maendeleo ya watu sio vitu.

BTW kupeleka watoto shule wapate elimu

You mean elimu bure not only in delivery but also content? hio ya watoto kukaa kwenye vumbi au kusomea chini ya miti? hebu take your time upite shule hasa za rural areas uone hali ilivyo., kwa hio kupewa kiloba cha unga ndio maendeleo to you? LOL
 
@"Synthesizer,

Sio kwamba hawakutaka, bunge lilikua bishi kuruhusu matumizi yaliyokua na mwelekeo wa hasara. Ndo maana kuna waziri mmoja aliwaambia wananchi wale mchicha ili ndege ya raisi inunuliwe
Ndio genge la hao hao Mashetani wa rangi ya kijani . Ndege na radar zilizokuwa screpa na bado wakafanya ufisadi wa kutisha kupitia hayo manunuzi .

Danganyika ni mfano madhubuti wa Shithole countries zenyewe ambazo Trump alikuwa anaziongelea .

A Shithole nation
 
Usafiri wa anga ni kama kichocheo unakaribisha uwekezaji ila akili za wengi hawaelewi hilo
Acha kuandika pumba , kila siku mnahujumu mashirika binafsi waduwanzi nyie . Mmeua fast jet na bado mko kwenye mission ya kuimalizia precision air .
 
Back
Top Bottom