Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,968
Siku ajali ikitokea mfano ikachinja mamia ya watu ndio kila mtu utamsikia anavyokurupuka kutoka shimoni mara kamata yule, funga yule, mara utasikia marufuku kibao. Lakini saa hivi yanafanyika makosa makubwa ya kujaza abiria kwenye mabasi yale na treni hakuna anayesema. Yale mabasi ya mwendokasi ni kama kusema hayana kiwango cha abiria mapaka wajae hadi milango ishindwe kufunga ndio basi linaondoka. Tunachezea moto!Mara zote tunasubiri ajali zitokee ndo tuchukue hatua,
Nimebahatika kuyapanda mabasi ya mwendo kasi Kivukoni - Kimara,
Gerezani- kimara,
Kwanza Utaratibu ni mbovu kuliko mabasi yetu ya zamani ya foreni,
Mle watu wanakimbilia, watu wanagombana kuingia ,mpaka unajiuliza kumbe sisi mazuzu tunaacha ya 400 wanayokaa vizuri tu, unakimbilia la 650 ambalo huna hewa , wanajaza mpaka hakuna mfno,
Hapa nawahurumia watoto wadogo, mama wajawazito, wazee, walemavu na wagonjwa, hawez kupanda mwendo kasi akiwa kimara asubuhi, wala hawez panda mwendokasi akiwa gerezani kariakoo jion, ni fujo na vurugu,
Hapa ilibidi uwepo Utaratibu wa kuwa monitor abilia kwa idadi anayekuja akiwa wa Kwanza ndo apande akiwa wa kwanza,
Nimeyapanda mwezi wa Sita nikaona kumbe tulio mbali tunarushiwa picha kuonesha yalivyo kumbe huduma zao mbaya mno,
Wao wako busy kukusanya Hela,
Kwa Treni ya Stesheni mpaka pugu huko wanajaza kupita kiasi, narudia tusitake kukaa tunaomboleza
Britannica