Tusipojua tunataka nini kwenye elimu yetu, tutakuja kupangiwa na watu wa nje

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
Naona kama kwenye education system bado tumelala sana. Hivi huwa najiuliza. Wananchi wa tanzania wanataka watoto wao waelimishwe kuhusu nn. Elimu bora imefafanuliwa vipi kwa wazazi.

Tuna mpango endelevu kweli wa kujua watoto wetu wanahitaji kujua nn mashuleni utakao husisha kubadilishwa kwa syllubus.

Je, wanahitaji kujua kingereza kizuri?
Je, wanahitaji kujifunza juu ya uzalendo wa afrika?
Je, wanahitaji kujifunza discipline?
Je, wanahitaji kujifunza technology?
Je, wanataka ipad na sio chaki?

Lakini swali linabaki palepale, watoto wetu wanataka nini?

Naongea hivi kwa sababu tukishindwa kujua watoto wetu wanataka nn. Kuna mtu atatokea sehemu, inaweza kua ulaya au sehemu yoyote na kutuletea chochote kwa watoto wetu na atadai kuwa hicho alichokileta ndo kinafaa kwa watoto wetu.

Watu wataniuliza, kwanini watu watoke nje watuletee sisi elimu ya watoto wetu na kutuelekeza jinsi ya kuwalea. Je, kuna kitu wanafaidika?

Of course yes, kwenye kila move inayofanywa na mtu ambae ni tofauti na jamii yetu lazima kuwe na ufaidikaji. Inaweza kua ni long term plan ya ku miseducate watoto.

Ndo maana nauliza tena, wana community wa Tanzania. Je, tunataka watoto wetu wapate nn mashuleni? Tuna sababu zozote za kubadili syllubus. Na kama zipo, tunampango gani za ku-implement. Maana zao la watanzania tulionao na matatizo yaliyopo limechangia sana na impact ya elimu yenye makosa mengi.
 
Elimu ni kitu Universal dunia nzima.

Mabadiliko kwenye syllabus ni kidogo tu kuufanya i-fit in kwenye mazingira yetu.

Hatuwezi kujifungia kubuni elimu ambayo haieleweki kwasababu elimu siyo kwaajili yako tu na taifa lako.

Museveni, Joseph Kabila wamesoma UDSM.

CEO wa Aliphabet (Google, YouTube) amesoma India.

Ila wanafanya kazi universally kutokea sehemu ambazo hawakusoma.

Ukitaka kubagua elimu utakuwa binadamu wa maonesho kama Masai na Mhadzabe.
 
Elimu ni kitu Universal dunia nzima.

Mabadiliko kwenye syllabus ni kidogo tu kuufanya i-fit in kwenye mazingira yetu.

Hatuwezi kujifungia kubuni elimu ambayo haieleweki kwasababu elimu siyo kwaajili yako tu na taifa lako.

Museveni, Joseph Kabila wamesoma UDSM.

CEO wa Aliphabet ( Google, YouTube ) amesoma India.

Ila wanafanya kazi universally kutokea sehemu ambazo hawakusoma.

Ukitaka kubagua elimu utakuwa binadamu wa maonesho kama Masai na Mhadzabe.
Issue sio kubagua. Issue ni kwamba elimu yetu ni ya toka mkoloni. Kuna update nyingi zinatakiwa zifanyike. Otherwise kama hatutapita huko ku update hata dunia unayoisemea itatuacha.

Kuna mambo mengi ya kubadili kwenye syllubua pia kuna mambo ya kuongezwa.

Kwa mfano. Elimu inapaswa kumpa mtoto confidence na spirit kua hata yeye kama muafrika anaweza kua the great. Na imfafanulie vizuri ukoloni in a positive way bila kuua spirit yake.
 
Confidence inaanza na malezi. Na malezi yanaanza na mzazi.

Wazazi ni madikteta usitegemee mtoto atakuwa na confidence.

Mfano: Adhabu ya viboko ni sababu mojawapo ya mtoto kupoteza confidence.
 
Kwa akili yako kabisa elimu hii inatufaa? Abu acha zako usijifanye hujui, mfumo wa elimu tulionao mbovu na haufai kabisa..achilia mbali silabasi yake.

Mosi tu chague lugha moja kama ni kiingereza au kiswahili..sio mwendo huu wa lugha gongana.

Pili miaka ipunguzwe tunatumia muda mrefu sana kwenyw basic education yani kuanzia lakwanza hadi alevo.

Tatu tujikite zaidi kwenye ufundi na ubunifu, mambo ya kukaririshana madesa hayana maana.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenye uwezo English schools
Kayumba type kwa lugha ya taifa inayopewa jina la uzalendo
Katu sitoruhusu wanangu wasome shule za kayumba..hizo shule zimewekwa mahususi na ccm kwaajili ya kutengeneza wajinga wasio hoji waendelee kuiweka madarakani.

Kwa upumbafu wetu hata hatushituki..uliona mtoto wa kiongozi gani anasoma kayumba?

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu yetu ijikite zaidi kwenye juwafanya wahitimu kuwa na uwezo wa kufikiri sawasawa na kujifunza vitu vipya kwa haraka tofauti na hapo hatuna chetu kwenye hii dunia inayobadilika kwa speed ya mwanga
 
Issue wala.sio mfumo wa elimu yetu .Mimi niana issue ni makuzi na malezi ya watoto wetu.Nina rafiki zangu wamataifa mengine na watoto wao wanasoma shule hizi hizi kitu nilichokiona tofauti kwao ni wazazi wa kitanzania akishampeleka mtoto shule mwalimu na serikali inaachiwa kila kitu.Wahindi wako tofauti ,mtoto anaanza kufundishwa vitu very basics vya misingi ya dini na maisha.Sisi waswahili tukijitahidi tunamwachia mtoto wa kazi.System ya elimu yetu hata ibadidishwe vipi haiwezi kukidhi utandawazi au ukuaji wa maendeleo duniani kwani wazazi wamebaki kuwaachia watu wengine wawalee watoto na kudhani elimu ya darasani inatosha.Mtoto anamaliza chuo hata kufagia nyumba hawezi,kupika chai hajui unafikiri hata akipata kazi ofisini hataweza ni mvivu wakuyengenezwa.Mtazamo wangu tu.Wazazi tubadilike,shule ni asilimia 40 tu ya maisha ya binadamu .Mzazi 55 na dini 5 .Jaribu hiyo utaona mabadiliko
 
Unataka kunambia mfumo wa elimu hauna impact kabisa kwenye jamii. Unataka kunambia mashuleni watoto wafundishwe elimu mbovu haitakua na impact. Na unalaumu malezi.
Elimu ina impact kuliko malezi. Sababu mtoto anatumia mda mwingi shule kuliko nyumbani. Na hata kama ana malezi mabaya bado akirudi shule atakuwa exposed na wenzake na atajifunza.
 
Katu sitoruhusu wanangu wasome shule za kayumba..hizo shule zimewekwa mahususi na ccm kwaajili ya kutengeneza wajinga wasio hoji waendelee kuiweka madarakani.

Kwa upumbafu wetu hata hatushituki..uliona mtoto wa kiongozi gani anasoma kayumba?

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Niitajie vitu vitano ambao hawajasoma kayumba wameviunda/kuvumbua/ innovate.

Kama havipo basi watakuwa wamevumbua kingereza, na hizo shule bado hazitatui tatizo la elimu duni Tanzania bali ni kujidangnya tu eti engl medium school ni shule bora huku wanatumia mtaala duni unaowasilishwa kwa kingereza.

kama shule za private zingeweza kuruhusiwa kubiresha mitaala yao walau kwa 40% basi zingekuwa bora ila kwa mtaala uleule wanaenda kujifunza kuongea kingeraza.
 
Mimi ukiniuliza mabadiliko kwenye elimu yetu, basi nitapendekeza Lugha ya Kiingereza itumike kufundishia elimu ya msingi hadi chuo kikuu.
 
Sisi waswahili tukijitahidi tunamwachia mtoto wa kazi.System ya elimu yetu hata ibadidishwe vipi haiwezi kukidhi utandawazi au ukuaji wa maendeleo duniani kwani wazazi wamebaki kuwaachia watu wengine wawalee watoto na kudhani elimu ya darasani inatosha
Mtoto akitoka asubuhi anakwenda shule
Akirudi jioni kucheza rede
Akirudi nyumbani amechoka anakula analala, homework hafanyi atajuana na mwalimu wake kesho
Weekend mtoto anarandaranda na kwenda kwenye vigodoro
 
Unataka kunambia mfumo wa elimu hauna impact kabisa kwenye jamii. Unataka kunambia mashuleni watoto wafundishwe elimu mbovu haitakua na impact. Na unalaumu malezi.
Elimu ina impact kuliko malezi. Sababu mtoto anatumia mda mwingi shule kuliko nyumbani. Na hata kama ana malezi mabaya bado akirudi shule atakuwa exposed na wenzake na atajifunza.
Hakuna elimu mbovu kama imepitishwa na serikali.Shida ni mapokeo na exposure.
Kwenye elimu hiyo hiyo kunawanaotoboa na hawajawahi kujutia .Sisi baba yetu alitufundisha kazi za nyumbani,ujasiriamali na darasani tulitoboa.Wengine hawakutaka kuajiriwa kabisa na wengine waliajiriwa.Ninachitaka kusema elimu sehemu kubwa mtu asikudanganye ni wazazi na jamiii inayokuzunguka.Sisi waliojiajiri ,sio kwamba walikosa ajira no waliamua hivyo na wametoboa.Baba yangu was teacher wa University na kila wakati alisisitiza elimu kubwa hutoka kwa wazazi .
 
Back
Top Bottom