Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Kufuatia yanayoendelea hapa nchini hasa ya kutekana na watu kupotea kimya kimya ni dhahiri kuwa kuna tatizo kutokea juu, juu kwa waliopewa madaraka makubwa kabisa ya vyombo vya ulinzi na usalama au juu kabisa kwenye ofisi yetu kubwa.
Niliwahi kuishi Iraq kipindi fulani , huko ukitaka kuvuka barabara kwenye maeneno ya public unatahadharishwa kwanza utazame mkono wa kulia, halafu utazame wa kushoto kama hakuna gari kisha tazama juu kama hakuna rocket karibu.
Ukijirishisha kuwa hakuna yote hayo basi ni lazima utazame nyuma kama hakuna terrorist na baadaye uwe makini sana kuhakikisha kuwa unapokanyaga hakuna Bomu la kutegwa, baada ya hapo unaruhusiwa kuvuka barabara, lakini kwa mwendo wa kwa zigizaga kukwepa risasi yoyote kama kuna mshambuliaji mahali, maana lolote laweza kutokea.
Baada ya kuvuka unatahadharishwa tena kuhakikisha hakuna gari lolote tinted mbele yako ambalo linaweza kuwa na mtu ndani anayetegea kukunyakua pindi utakavyovuka barabara.
Kwa hali ilipofikia sasa ndani ya Tanzania ukitaka kuvuka barabara angalia sana kama kuna gari tinted imepaki mahali, usije ukadakwa na wenye nguvu zao.