MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Nimejiuliza maswali mengi baada ya kumewasikia wachangiaji karibu wote kwenye kusanyiko linaloitwa ‘’ kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ wakitoa mchanganuo wa maisha ya Mwl. Nyerere kama raia wa kawaida na Kiongozi Mkuu wa Tanganyika na Tanzania.
Miaka 29 ni mingi sana tokea Mwalimu Nyerere alipoachia ngazi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na kuwa mwananchi wa kawaida. Hii ina maana kuwa mtu mwenye miaka 28 hapa nchini hakuwahi kuona utendaji kazi wa Mwalimu Nyerere serikalini na ndani ya CCM. hili ni kundi la vijana ambalo kwa sasa lina watoto wenye umri wa miaka 11 kisheria kwa sababu umri wa kuanza kufanya mapenzi nchini ni miaka 18.
Kama wale wachangiaji niliowaona kwenye kongamano ndio tunawategemea sana katika mawazo yao kwenye kulijenga taifa basi hili taifa litaendelea kugubikwa na unafiki mkubwa ambao ni sumu kwa maendeleo chanya.
Bila kuondoa unafiki na kuwa wakweli hatuwezi kujua madhaifu yaliyolifanya taifa hili kupiga hatua za kusua sua katika nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Tunajua sheria za maumbile(laws of nature)zimetupa angalizo kuwa ili kitu kiwe kamili lazima kiwe na pande mbili. Hata nguvu za kifizikia ziko za aina mbili mbili ambazo ni hasi na chanya.
Nakumbuka wakati nikisoma shule ya ‘’ngumbalu’’ tulikuwa tunafanya makongamano na midaharo ambayo lazima iwe na pande mbili zinazoitwa wanaokubaliana (The affirmative or Aff) na wasiokubaliana (the Negative or Neg).Hii yote ni kukamilisha takwa la sheria za maumbile ambayo ndani yake kuna fikra.
Kamusi ya kiswahili sanifu inasema, kongamano/mdahalo ni majadiliano yanayofanywa na pande mbili zinazokinzana kuhusu suala fulani kwa kueleza sababu na ithibati ya msimamo wao tofauti na kufikia hitimisho la pamoja.
Kile kilichoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ hakikuwa na kiwango kinachokidhi kuitwa kongamano kwa sababu wachangiaji wote walikuwa wanaonyesha upande mmoja wa Mwl. Nyerere katika maisha yake.
Mimi sina tatizo na kazi zilizofanywa na Mwl. Nyerere bali tatizo langu ni kuendelea kuchora/kutendeneza picha yake kama vile Mwl. Nyerere hakuna binadamu kwa maana kuwa hakuwa na mapungufu ya kibinadamu na kiuongozi.
Nadhani wale wanataka kumjua vizuri Mwl. Nyerere hawakuweza kupata upande wake wa pili kama ulivyobainishwa katika maandiko mengi na hasa kutoka kwa Mtanzania aitwaye Ludovic S. Mwijage katika maandiko yake kwenye vitabu mbali mbali ambavyo baadhi ni;
1)Dark side of NyerereLegacy-1996.
2) Julius K. Nyerere: Servant of God or Untarnished Tyrant?-2010.
Watu kama Ludovic Mwijage walitakiwa pia watoe michango yao katika kongamano hili ili upande wa pili wa Mwl. Nyerere ueleweke na kueleweka kwa upande wa pili ungesaidia kutoa fundisho zuri kwa vizazi vijavyo.
Waandaaji wa kongamano walishindwa vipi hata kumualika James Brennan ambaye amefanya utafiti na kukusanya mawazo ya watu mbali mbali kuhusu Mwl. Nyerere na kuyaweka katika kitabu kinachoitwa , Nyerere through the Eyes of His Critics, 1953-2013
Wangeweza hata kumualika mwanaJamiiforums mwenzetu, Mzee Mohamed Said ambaye ni mwandishi na mhariri wa maandiko mengi yenye mlengo wa kushoto kuhusu Mwl. Nyerere.
Tuache kuufanya mijadala kama hii iwe niya kinafiki kisiasa kama sehemu ya kuifundisha jamii yetu bali tufanye mijadala yenye pende mbili zenye mitazamo tofauti kama sehemu ya kuchambua ''pumba na mchele'' katika kuujua ukweli kwa sababu ukweli hujenga.
Walioandaa kinachoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ haikuwa ni kongamano bali ni mkusanyiko wa wapiga propaganda zenye unafiki.
Tuache unafiki, tulitendee haki taifa letu na vizazi vijavyo!