Tusiopenda kufanya mazoezi tuna hoja, sababu na visingizio vya msingi sana; Tuvumiliane Tafadhali

Mimi nimechemka kabisa kufanya mazoezi, kuna kioindi nilijaribu kila weekends nifanya wiki ya 1 na ya pili tu nikashindwa kila nikisema sasa najipanga kuanza nashindwa.

Nilichigundua kufanya mazozi ni upako kama huna utabaki kutamani tu na hutaweza
 
Harakati zangu za mazoezi zilianza tangu Enzi za ujana huko chuo hadi sasa mtu mzima, Lakini hazijawahi kudumu japo kwa wiki mbili.

Nakumbuka enzi hizo; Niliwahi andaa Jogging kuanzia mliman chuo, kupitia Ubungo > Magomeni > Morocco > Mwenge

Tuliondoka vizuri tu lakini nilipofika Manzese Nilichemsha kwakweli, ikabidi Nipande zangu daladala hadi Mwenge!

Sikurudia tena kufanya kwanza nikaanza kujifariji; Sina hela ya kula vizuri mazoezi ya nini, nikaachana na mazoezi uchwara!

Nilivyomaliza chuo; Mzuka wa mazoezi ukaanza tena; nikawa siku za weekend naenda kunduchi beach, lakini napo sikudumu sana kwasababu ya visingizio vya kukosa nguo za mazoezi,

Mungu si Athumani, nikanunua raba na pensi ya michezo, nikarudi ulingoni! Kulekule Kunduchi Beach, siku za weekend, siku ya kwanza nikakaza fresh, siku ya pili pia nikakomaa, Siku ya tatu nikawaza: Ya nini kufanya mazoezi alfajili mwisho nikabwe bure? NIKAACHA!

Maisha yakaendelea miaka na miaka, nikawaza huenda mazoezi mazuri ni yale ya GYM, wacha nikajiandikishe.

Nililipia GYM mwezi mmoja, katika mahudhurio yangu pale GYM nakumbuka nilifika siku tatu tu nikaghairi; kwanza nikawaza, mazoezi gani sina hata gari aaah? ...Nikaachana na GYM
Miaka ikasonga! Niliponunua gari, nikarudi tena GYM kujiandikisha, nikahudhuria siku mbili nikaopoa mrembo mmoja; sikurudi tena mazoezini, na mazoezi nikaacha tena. Kwanza nikawaza napoteza pesa na mafuta bure.

Nikajisemea wacha nikija jenga nyumba yangu nitaweka chumba cha mazoezi.

Miaka ikasonga, nilipojenga, nikaweka chumba cha mazoezi, lakini nakumbuka nilifanya wiki moja tu, nikawaza tena labda wacha ninunue mashine kabisa za mazoezi zitanisaidia!
Mwaka jana nilifanikiwa kuzinunua lakini nimezitumia siku chache tu nikaona miyeyusho! NIKAACHA

Hadi leo chumba cha mazoezi nimekigeuza STOO!

Mazoezi yana wenyewe! Tuwaachie mazoezi yao EBOOOH!!
hahaaaa hujawa na nia ya dhati kabisa ya kufanya mazoezi aisee!
 
Huu uzi umepata promo ya mods, nimekutana nao Telegram
 
Kipindi nasoma O level ile miaka minne yote niliitumia kucheza Mpira na mazoezi ya karate.

Lakini baada ya kumaliza tu mitihani nilivyorudi home nikabaki nafanya mazoezi ya mpira Mara chache sana.

Baada ya miaka 20 kupita na kuwa na tumbo kama nimeweka mitambala niliaanza kujinyima kula ili kushape vizuri tumbo nikawa napungua mwili tumbo lipo vile vile nikashauriwa nipige push up daily.

Hivyo nimeanza sasa hivi Nina week ya tatu naona matokeo si mabaya sana.

Leo Juma pili hii mpaka sasa hivi nipo kitandani naperuzi JF sijapiga push up hata moja.
 
Mkuu hata mm nilikuwa kama ww lakin ..kikafanya nachokipenda ,nikajiunga na timu ya vijana hapa mtaan kaz zangu za usiku so napata mda wa mazoez japo wananicheka lakin natoka josho ...
wanakucheka hicho kitambi au?
 
Mazoezi ni wito,yanataka ujisacrifice vinginevyo utajiambia mwenyewe kama Sikiri "nakufa hapa kwann wakati Sadiki ashiba chakula kingi kwa baba..",?? Utajirudia zako home mdogo mdogo huku Uvivu ukikupa tulizo la nafsi na burdani isiyoisha..Mazoezi yanataka ujikatae

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Morogoro
Mungu Ibariki Gairo
Mungu ibariki Chato
 
Nilianza mazoezi ya kuweka tumbo flat last week nkasema ntakua napga pull up 50 kila siku yani 25 asubuhi na 25 jioni nkirudi kazini..siku ya kwanza nkaanza nkapga 25 ila kufika 25 nikanogewa nikaona mbona rahaa so nikaenda hadi 70 kwa ile asubuhi tu.

Jioni ikafika nikasema kwakua nilipiga asubuhi nyingi saivi hata nkipiga 20 ntakua nishafikisha lengo langu la siku,nikaanza piga 1 2 3 nikaenda hadi 20 nikanogewa nikaenda had 47 hv..nikafurahi sana.

Kesho yake asubuhi nikarudi kupiga tena nikaanza 1 2 3 nikaenda kwli kwa mbinde sana had 25 nikaamka nikaenda kuoga nikavaa nikaenda job,jioni ikafika kurudi home ile nimelala tu chini Tumbo misuli inauma hata kulala vizuri nikashindwa.

Nikajaribu kuinuka ila maumivu yake sikuweza kwakweli..nikainuka sikupiga pull up hata moja nikaenda kuoga..nikiwa kazini nikicheka mbavu zinauma Aseee nkawa siwez hata kucheka vizuri kwa sababu ya maumivu.

Jioni nimerudi nyumbani nikasema acha nishtue nijikaze ila this time around kukaa chini tu Nilishindwa halafu nikijitahidi niweze tu kulala pale kwenye sakafu USINGIZI unakuja sio wa nchi hiii...sikuendelea tena hapa nawaza njia nyingine ya kuweka flat tumbo...Nadhani hizi chipsi mayai na serengeti lite na vimishkaki sio vizuri ndio natakiwa kuviacha.

Bora nifanye mazoezi ya kula kwa ratiba ila sio mazoezi aseee...Yamenishinda LABDA niki pata kampani ila peke angu ishanshinda.
 
Kwa mujibu wa research za madaktari na sio wewe kilaza huna degree yoyote ya medicine!

Na reports zipo!

Tukusikie wewe mavi kunuka tukupeleke wapi?

Bulaza mbona unatumia nguvu nyingi sana, kwa mujibu wa hizo unazoita research.... Kobe anaishi muda mrefu kuliko Simba.
 
binafsi nilianza mazoezi mwezi novemba mwaka jana nikadumu nayo kwa muda wa miezi kama mitatu hivi.
ilivyofika januari nikaacha ghafla kwa visingizio vingi sasa nimepania kuanza leo.
nimeanza kwanza kwa kunywa dawa za kuendesha japo mzigo umegoma kutoka mpaka sahizi kilitoka choo cha kawaida ili angalau niwe mwepesi lakini nafikiri wacha nianze kwakuwa nishakuwa waduara tena.
 
Back
Top Bottom