Tusiogope Kifo, maana ukiwepo inamaana kifo hakipo, kama kifo kipo kimekutokea inamaana haupo, mnakwepana

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,467
2,000
Penye kifo chako haupo, na kama upo basi hakuna kifo chako,

Hii dhana ya watu kuogopa kufa nadhani hofu utokana na uoga tu,

Ni wachache sana wanaowaza kwamba watoto wangu au majukumu ambayo sijakamilisha atayafanya nani, wengi uogopa tu kwakuwa wanakufa na kuogopa tu kifo,

Unajua wanaokufa hawasikii maumivu yoyote huko walipo? Kama watakuwapo kweli,

Sijawahi kufika huko lakin najua na sioni sababu ya kufanya mtu ateseke huko aendako,

Hivi ni sababu zipi zinapelekea we msoma Uzi huu kwamba hupaswi kufa muda huu au kufa muda wowote,

Tujiandae, uoga wa kufa uwafanya watu waache mambo bila kuyaweka kwenye utaratibu,

Ukifa we hutaumia ila watakaoumia ni wale wanaobaki wakijilazimisha kulia kwasababu yako uliyeondoka,
 

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,467
2,000
Ufunuo wa Yohana : Mlango 14

13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.Kuvuna Mavuno ya Nchi
Umetisha kumbe mambo ya bible uko vizuri?
 

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,056
2,000
Sababu kubwa ya kuogopa kifo ni DINI zetu. Aisee zina vitosho sana yani mtu wawaza ndo naenda kutana na moto wa milee eti? Mana kama Peponi ndo kama dini zinavyosema hakuwa wa dunia ya leo anatimiza sheria zake zote
 

Stephen Chelu

Verified Member
Oct 31, 2017
5,409
2,000
Kifo kama usingizi, ukiwa macho unajua utalala ila wakati umelala hujui kama umelala, utajua kuwa ulilala ukishaamka. kwa hiyo kwa kuwa kifo ni enfelevu basi hutajua kuwa umekufa. ila unajua kuwa utakufa kwa kuwa upo hai. Kuna mstari mmoja wa biblia unasema walio hai wanajua watakufa ila wafu hawajui lolote. Huo ndio mtazamo wangu mimi mlevi mmoja.
 

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,467
2,000
Kifo kama usingizi, ukiwa macho unajua utalala ila wakati umelala hujui kama umelala, utajua kuwa ulilala ukishaamka. kwa hiyo kwa kuwa kifo ni enfelevu basi hutajua kuwa umekufa. ila unajua kuwa utakufa kwa kuwa upo hai. Kuna mstari mmoja wa biblia unasema walio hai wanajua watakufa ila wafu hawajui lolote. Huo ndio mtazamo wangu mimi mlevi mmoja.
sawa kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom